Zaidi ya watu 1,000 wamekosa makazi, baada ya nyumba 237 kubomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma.
Wakazi walioathirika kutokana na mvua hizo ni wa Wilaya ya Bahi, huku miundombinu ya barabara ikiharibiwa.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahamisi Munkunda...