Mafuriko yawaacha bila makazi wananchi 4,500 Mkoani Lindi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
1580117191103.png

Picha haihusiani na tukio

Zaidi ya wananchi 4500 wa vijiji sita wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 27, 2020 mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Kilanjelanje, Nanjirinji A Ruatwe, Njinjo, Nakiu na Nanjirinji B.

Amesema mbali na nyumba kubomoka, mashamba na mifugo ya wananchi hao nayo imesombwa na maji.

“Mafuriko yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu mfululizo,” amesema Ngubiagai.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema timu ya uokoaji imekwenda eneo lililokumbwa na mafuriko kwa boti kunusuru maisha ya wananchi, kwamba wananchi hao watapelekwa katika maeneo yaliyotengwa.

Amewataka watu wa kada mbalimbali kutoa msaada kwa wananchi hao.

“Tunaendelea kuwaokoa na kuwapeleka maeneo ambayo tumeyatenga. Tunahitaji msaada wa chakula, dawa, nguo na vitu vingine muhimu,” amesema Ngubiagai.

CHANZO: Mwananchi
 
Back
Top Bottom