Watu 18 wamekufa na wengine wapatao 200 Wamekosa makazi katika jimbo la New South Wales kutokana na moto uliotokea nyikani

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
WATU 18 wamekufa na wengine wapatao 200 kukosa makazi katika jimbo la New South Wales nchini hapa kutokana na moto wa nyikani, uliotokea hivi karibuni. Polisi imethibitisha kutokea vifo hivyo.

Watu wawili walikutwa katika magari tofauti jana asubuhi. Pia yupo baba na mtoto ambao walibaki kwenye nyumba yao. Mwingine ni mfanyakazi wa kujitolea wa kikosi cha zimamoto ambaye alikutwa na mauti, baada ya upepo kupuliza mashine yake ya kuzimia moto.

Vyombo vya habari vya nchini hapa, vimeripoti vifo vingine kutokea katika eneo la Victoria. Miongoni mwa nyumba zilizoharibiwa, 43 ni katika eneo la East Gippsland, Victoria na 176 ni katika jimbo la New South Wales.

Awali, kikosi cha zima moto kilisema nyumba 916 zimeharibiwa. ` Mamlaka zililazimika kuweka zuio kwa maeneo kadhaa ya kujivinjari hususani wakati wa msimu wa sherehe katika mwambao wa pwani kati ya miji ya Sydney na Melbourne kutokana na moto huo.

Awali, Gavana wa Jimbo la Victoria, Daniel Andrews alisema meli huenda zikatumwa kupelekea waathirika wa moto huo chakula, maji na umeme kwenye maeneo hayo. Alisema baadhi ya watu waliotengwa, wanaweza kufikiwa kupitia bahari. Moto wa nyikani katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo, ulitokana na ongezeko la viwango vya joto, upepo mkali na radi.

Habari Leo
 
Back
Top Bottom