UNHCR yakumbwa na pengo la makazi kwa ajili ya wakimbizi, asilimia 5 tu ndiyo walipata makazi 2019

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
42a190513b440627dcb47e7deb8c2ac3

Chini ya asilimia tano ya wakimbizi wanaohitaji makazi ya dharura kote ulimwenguni, walipata makazi mapya mwaka jana kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia Wakimbizi UNHCR.

Takwimu zilizotolewa leo na shirika hilo zinaonyesha kuwa huku watu milioni 1.4 wakihitaji makazi mapya lakini 64,000 pekee ndio waliopata maakazi, kuna pengo kubwa kati ya mahitaji ya makazi na maeneo yaliyotengwa na serikali mbalimbali kote ulimwenguni.

Zaidi ya watu milioni 70 walipoteza makazi yao kote ulimwenguni mwaka jana kutokana na vita au mateso, ambapo watu milioni 30 walikimbia nchi zao.

Mwaka wa 2019, Marekani iliichukua idadi kubwa ya wakimbizi, ikifuatiwa na Canada, Uingereza, Sweden na Ujerumani.

Miongoni mwa waliopewa makazi mapya mwaka jana, watu wengi walitokea Syria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Myanmar.
 
Back
Top Bottom