Madhara ya mvua Babati: Kaya zaidi ya 400 zakosa makazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Zaidi ya ya Kaya 426 Wilayani Babati Mkoa wa Manyara hawana makazi baada ya Nyumba zao kuanguka na nyingine kuzingirwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo huku pia mashamba na miundombinu ya barabara ikiathiriwa vibaya.

Vijiji vilivyoathiriwa ni Moyamayoka ambako nyumba 10 zimezolewa na upepo mkali ulioandamana na mvua, kijiji cha Mwada ambapo nyumba 4 zimeanguka kabisa huku 32 zikizingirwa na maji lakini pia mazao yakiathirika hivyo kuleta wasiwasi wa upatikanaji wa chakula. Maeneo mengine ni kijiji cha Gichameda ambapo taarifa ya kijiji imeonyesha kuwa nyumba 390 zimeathiriwa 10 zikianguka kabisa 176 zikizingirwa na maji maeneo hayo hayakufikika kirahisi.

Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu ametembelea maeneo yaliyoathiriwa na kujionea hali ilivyo ambapo miundo mbinu ya barabara kuelekea magara hadi mbulu imeharibika.

Lakini adha hii inahusishwa kuanza miaka ya hivi karibuni kufuatia ubharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi wenyewe.
 
kumbe ni jirani yangu,poleni
 
Back
Top Bottom