Napenda kupongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi kuwatimua vijana zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanywa na Q NET wakipewa ndoto za utajiri wa haraka na wao kuombwa kiasi cha milioni 5 ili kutajirika.
Sasa iko hivi, hawa Q NET wana ka mtandao kengine wanakaita Rythim Foundation...
Ndugu wa mwanamke anayedaiwa kujinyonga akiwa mahabusu jijini Dar es Salaam wameliburuza mahakamani Jeshi la Polisi na Hospitali ya Taifa Muhimbili wakitaka uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.
Stella Moses (30) alifariki usiku wa Desemba 20, 2020 akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi...
Shtaka la Maafisa saba wa Jeshi la Polisi wanaotuhumiwa kumuua mfanyabiasha wa madini, Musa Hamisi, aliyekuwa mkazi wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi limesomwa leo Juni 16, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara.
Watuhumiwa wote walifikishwa Mahakamani hapo ambapo shtaka lao limepangiwa...
Wanabodi,
Kati ya Taasisi zinazopaswa kufanya kazi kwa weledi mkubwa bila mihemuko ni Jeshi Letu la Polisi.
Kuna baadhi ya issues ambazo jeshi letu la polisi, zinazishughulikia sio issues za kipolisi, ni issues za kijamii na kifamilia.
Kwanza msikilize Kamanda Polisi Huyu
Kisha isome taarifa...
Habari wanajamvi.
WIKI HII inayoishia leo 21 May 2022 Nilikuwa nimekaa mahali usiku nikasikia kwenye radio kwa mbali ilikuwa ni taaarifa ya habari nikawa interested kuisikia lakini bahati mbaya ikawa imepita.
Nimejaribu kuitafuta kwa bidii kwenye mtandao nimeikosa.Inaelekea haina intrest...
Inaonekana hizi risasi zinazotumika kwenye silaha zetu nyingine ni fake au zina tatizo flani. Mara kadhaa imetokea Polisi wanapiga Risasi Juu kutawanya watu. Yenyewe inakata kona na kwenda kumfuata mtu aliye chini.
Kuna haja Serikali iangalie hizi zinatengenezwa wapi. Isije ikawa ni za Kichina...
Wafanyabiasha vinara wa dawa za kulevya aina ya Mirungi kutoka Nchini Kenya waliokamatwa na magunia 15 mei 14 mwaka huu katika Mji wa Namanga, wanadaiwa kuachiwa katika mazingira ya utata, usiku wa manane huku gari lililokuwa likisafirisha mihadarati hiyo likitoweka kituo cha polisi ...
Hotuba ya Msemaji wa sekta ya Mambo ya Ndani ACT Wazalendo Ndg. Mbarala Abdallah Maharagande kuhusu bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Utangulizi:
Jana Alhamisi tarehe 5 Mei 2022 Wizara ya Mambo ya Ndani iliwasilisha bungeni hotuba ya bajeti kwa mwaka wa fedha...
Labda wengi wenu hamkumbuki jinsi Steve Biko wa Afrika Kusini alivyouwawa na Jeshi katili la Afrika Kusini. Kwa kifupi basi, ni kwamba baada ya kupigwa sana kwa ajili ya harakati zake za Black Consciousness Movement , akiwa na majeraha, Steve Biko alifungwa pingu na kuwekwa katika Land Rover na...
Naamini IGP Sirro anakaribia kustaafu utumishi wake kwenye jeshi la polisi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30. Japo amefanya mengi lakini yapo ambayo bado ananyyoshewa kidole kwayo. Japo ni mengi lakini naomba niwasilishe swala hili moja tuu kwa leo. JESHI LA POLISI CHINI YA SIRRO limeshindwa...
Muda mfupi baada ya RC wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuandika mtandaoni kuwa kuna makundi matano yanamuwinda ili kumuua, Jeshi la Polisi limesema kama kweli ana hofu anatakiwa aende kutoa taarifa Kituo cha Polisi.
Akizungumza na Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Kamanda wa Polisi...
Afande pokea taarifa kuhusiana na mahojiano yaliyofanyika leo Tarehe 04/04/2022 baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa makosa ya utapeli David Damas Otieno @ MAJOR GENERAL MRAI miaka 39, kabila mjaruo, kazi mkulima, dini mkristo mkazi wa Dar es salaamu ambaye amekamatwa leo Tarehe 04/04/ 2022...
Kwa sisi ambao ingalau tumepitia JKT, tuliopata mafunzo kamili ya infantria miaka kabla tu ya Vita ya Kagera, matukio ya miaka ya karibuni yanatutia wasiwasi sana na hili jeshi letu la Polisi. Malamiko madogo madogo ya utesaji, ubambikaji kesi, hata wizi na rushwa yalianza kuwa malamiko ya...
Tukiwa JKT kwa mujibu wa sheria tulifundishwa mambo mengi yakiwemo Uvumilivu, Nidhamu na Utii.
Ukiwa jeshini unatakiwa utumikie nafasi uliyopo kwa weledi na uzalendo uliotukuka na kuwatii Viongozi wako pamoja na kuwaheshimu walio chini yako.
Jeshini hutakiwi kutamani nafasi ya mtu bali juhudi...
Nimeona kabla ya kufika tarehe 1/04/2022 niwakumbushe Wana JF ya kuwa hilo hapo ni kaburi la kijana wetu mtoto wetu Akwilina Akwilin aliyefariki kwa kupigwa risasi Na Askari polisi aliye kuwa anazuia maandamano ya Chadema.
Polisi alifyatua risasi na kuua mwananfunI ambaye hakuwa hata kwnye...
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema kuanzia sasa Madereva wanaoendesha magari kwa mwendokasi na kusababisha ajali watawekwa mahabusu na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na siyo kulipa faini tena.
Kamanda wa Polisi Wilbroad Mutafungwa amesema hayo wakati wa mazungumzo yake...
Katika nchi ya Pueto rico Rais analalamika akilisema jeshi la Police halifanyi kazi vizuri anajibiwa na IGP / Mkuu wa Jeshi la Police wa Pueto rico.
Naomba kunukuu maneno ya Rais wa Pueto rico ' Wewe uamini vyombo vyako ohooo ohoooo' alisikika Rais wa Pueto rico akilalamika kitendo cha utovu wa...
Binadamu tumeweka siasa Mbele maisha ya watu na utu wao nyuma. Katika kipindi chote ambacho matendo maovu ya Jeshi la Polisi yanafanyika hakuna aliyewahi kusikia Chama cha Mapinduzi wakikemea.
Tumesikia namna mwanachama wa CCM Bwana Sabaya alivyokuwa anakamata walinz wake nakuwapiga Kisha...
Taarifa ya Kamati ya uchunguzi wa matukio ya mauaji yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya askari mkoani Mtwara inadaiwa kubaini Jeshi la polisi lilishindwa kuteleza wajibu wake wa kulinda usalama wa Raia na mali zake badala yake likageuka kumpora fedha mfanyabiashara wa madini.
Pia soma
- Mtwara...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.