DOKEZO IGP Wambura, Waziri Masauni futeni ufisadi wa kundi hili la raia ndani ya Jeshi la Polisi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania kuna Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) ambacho kinaundwa na raia, I mean wale ambao siyo police officers but wapo ndani ya Jeshi la Polisi.

TUGHE ina matawi mengi, that’s why nimeeleza kwa ufafanuzi kuwa ninaowazungumzia hapa ni wale walio ndani ya jeshi hilo na wapo chini ya mamlaka ya jeshi letu japokuwa wao siyo maofisa wa polisi.

So ndani ya chama hicho kuna watu wamejitengenezea ufalme wao na wanafanya vile wanavyotaka wakiamini hakuna wa kuwafanya chochote na wanatumia mgongo wa polisi kufanya mauchafu yao.

Kwa faida ya wale ambao hawaelewi vizuri about this issue ni kuwa, alipokuwa madarakani Rais Magufuli aliagiza raia wote walioajiriwa kwenye Jeshi la Polisi watolewe na majukumu yao yawe handover to police officers.

Hilo lilifanyia but not 100%, walibaki wachache baada ya kuonekana kuna pengo lililoachwa, wakabaki wachache na sasa hivi wakati wa mama, ajira hizo zimeendelea kama kawaida.

Hapo kati kuna kundi liliingia kwenye idara hiyo ya raia na ndilo linalofanya ufisadi, kati yao kuna ma-HR wanne ambao wote wapo ofisi moja hapa Dodoma. Kibaya zaidi wanashirikiana na wale viongozi wa TUGHE walioingia madarakani njia ya kukaimu uongozi mwaka 2019.

Hapo kati kuna tume iliundwa ikaenda kuzungumza na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Simbachawene, akaelezwa kuhusu upuuzi unaofanywa na kikundi cha watu hao ambao ni viongozi wa kiraia, akasema atashughulikia lakini hadi anabadilishiwa nafasi hakuwa amefanya hivyo.

Hao ma-HR tuliyonao Dodoma ni wanaendekeza majungu na wanaamini hakuna wa kuwazuia. Safari zote wanajipangia wao, hawataki mtu ambaye siyo member wao aguse maslahi yao, ukiona wametoa nafasi kwa mtu mwingine basi jua ni mwenzao hata kama hayupo karibu nao.

Upande wa viongozi wa michezo nao ni walewale wakiongozwa na Farida, ni wapigaji kama wote na wanakwambia ukileta kidomodomo wanakupiga fitna mpaka utang’oka.

Tunaambiwa kuwa jeuri yote hiyo ni kwa kuwa wizarani kuna mtu mkubwa ambaye ndiye anayewasimamia shoo, hivyo hata kukitokea malalamiko yamefika wizarani, mkubwa huyo anajua jinsi ya kutuliza na kupotezea malalamiko hayo kisha wanakurudia wewe ambaye umepeleka malalamiko.

Mwaka jana, kama kawaida yao walijiingizia fedha kwenye mashindano ya michezo, wenzetu kadhaa wakalalamika kwa viongozi wa polisi, ikabidi waitwe wakapewa onyo, kibaya zaidi ni kuwa mwaka huu wamefanya yaleyale tena.

Nashauri mamlaka zichunguze viongozi akaunti za miamala ya viongozi wa TUGHE wa Dodoma, kilichoingia kwenye akaunti zao Oktoba 2021 na kilichotokea mwaka huu pia miezi miwili iliyopita.

Wafanyakazi wengi raia ni waoga kusema, wanabaki wanasema chinichini, japokuwa nawaelewa kwa kuwa ukiweka mdomo tu wakikujua basi ujue hauna ajira.

Tarehe 30 mwezi huu November kuna kikao cha wafanyakazi raia kinafanyika hapa Dodoma, kama itawezekana IGP na Waziri waanzie katika mkutano huo.

Nimekumbuka kitu, hata siri ya wao kufanya vikao kila mara hapa Dodoma ni kwa kuwa wana percent zao kutoka kwa wamiliki wa mahoteli, ndiyo maana hawataki kufanyia mikutano nje ya mji huu kama wenzetu wengi wanavyofanya.

Nimalizie kwa kuziambia mamlaka kuwa hiki nilichoandika hapa siyo majungu, kwa kuwa malalamiko yalishawahi kufika mezani kwao basi IGP Camillus Wambura na Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Yussuf Masauni angalieni doa hili, haliwagusi maofisa wa polisi moja kwa moja lakini kuna ule msemo samaki mmoja akioza.

Imani yangu jambo hili litafanyiwa kazi na pole kwa kuandika barua ndefu.
 
Gazeti refu sana, ila sijaona jambo linalotakiwa kuchunguzwa zaidi ya mwandishi kuonyesha chuki dhidi ya watendaji wasio raia. Uliichagua kazi unayoifanya, ifanye kwa moyo.
 
Gazeti refu sana, ila sijaona jambo linalotakiwa kuchunguzwa zaidi ya mwandishi kuonyesha chuki dhidi ya watendaji wasio raia. Uliichagua kazi unayoifanya, ifanye kwa moyo.
Mzee wao au ndugu yako wa karibu angekuwa amepigwa kitu na MAFISADI hao usingeongea hayo madudu
 
Polisi uwezo wenu mdogo kufanya kazi hasa za kitaalamu! sina uhakika kama kuna hata CPA holder jeshi la polisi! ndio maana raia wanakuwepo ila sio raia kama mnavyowaona nyie! jichanganyeni tu
 
Back
Top Bottom