Samia: 70% wanalinyooshea kidole jeshi la polisi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,888
Tumpongeze rais Mama Samia kwa kuwa na ujasiri wa kulisemea hili.

Screenshot_20230131-160633.jpg


Hii ni 180° tofauti na mtangulizi wake aliyekuwa akiwamwagia sifa wasizokuwa nazo kinyume cha matarajio ya wengi.

Taasisi isiyokubalika kwa kiwango hiki ni ya nini? Kwanini taasisi hii isivunjwe ikasukwa upya na ikibidi ikaanza na watu wapya?

Screenshot_20230131-160707.jpg


Kwanini kuendelea kuwalea madhulumati hawa wanaojulikana kana kwamba hawajulikani?

--------
Source: Rais Samia aichambua magereza, jeshi la polisi ‘linavyonyooshewa kidole’
 
Duh😳😳😳

Wanaojulikana kana kwamba hawajulikani!!!

Kiongozi wetu atakuwa aliusoma Uzi wa PASCO!!!
 
Kibogoyo akijidai kwa ukali wa meno yake wewe mpe muda wa utekelezaji ndio umpe sifa zake
You are right. Polisi wakianza kusimamia maadili wasije wakaanza tena kuwavuta upande wao.

Misingi ya utendaji wa polisi kwa 70% imeshajihishwa na chama cha ccm sababu mwenyekiti wa ccm ndio anateua na kufanya mawasiliano ya karibu na IGP.
 
Unafikiri yanajali sasa, sanasana utayakuta yapo ubaoni yanaimba "Yatapita" ya Diamond.... huku wengine wakipiga Radio call kusikilizishana hilo song kwa kufarijiana!!!
Yaani imenena sawa.
Comrade Kinana alitoa ushairi trafiki mjini wapungue barabarani. Wakatii kwa muda mfupi sana.
Sasa wamerudi kama Mbogo alie jeruhiwa.
Kama Arusha utadhani askari wote wana vaa nguo nyeupe.
Wamejaa kila mahali hadi kero.
Hivi sasa Arusha kuendesha gari ni adhabu.
Rais kama anataka kutusaidia asafishe jeshi la polisi. Walioko madarakani kwa sasa vichwa vyao ni vigumu mno.
 
Hiki nikikundi cha kigaidi alikiacha Jiwe kila siku kuonea raia mwema,kupanga njama zakuangamiza viongozi wa upinzani, kuteka ,kuua,kupora n.k ..hivi kamanda Badluck na Kaigai wako wapi? mama isuku Jeshi nzima kama vipi livunje kabisa tubaki tuu na JWTZ.
 
Hakuna ubishi kwamba wapo Polisi wabaya lakini Pia tusipofushwe macho kwamba Polisi wazuri wapo.

Tatizo la Polisi wanapambana na MAKUNDI makuu mawili Mlalamikaji Kwa upande mmoja na mlalamikiwa Kwa upande wa pili na Kwa vyovyote vile lazima mmoja ashinde na yeyote atakaye shinda lazima atakayeshindwa awachukie Polisi lakini Pia majumu Yao ya kukamata yanaongeza maadui wao kila siku mfano ukimkamata Baba yangu Kwa kosa lolote Lile lazima Mimi na familia nzima tuwachukie Polisi wote. Kwahiyo hakuna wakati wanaweza kuwafurahisha Pande zote na hiyo ndiyo sababu ya kuwachukia na kusingizia kwamba wanabambikiza kesi hovyohovyo.

Sababu nyingine ni Serikali kutokuwekeza Kwa Jeshi la Polisi wakiwaacha watumie fursa za kuombaomba ukitaka mtoto wako awe na TABIA mbaya mruhusi aanze kuishi Kwa kutegemea majirani.
 
Kusema hivyo tu ndiyo ujasiri wa kupongezwa?

Ni sawa na kumpongeza mzazi kwa kutambua mwanae hana daftari.

Watu tushasikia mambo mengi ya kutumainisha kutoka kwa wanasiasa na yakaishia hukohuko majukwaani!

Kuna waliopongeza hii pia.

 
Back
Top Bottom