Mbeya: Jeshi la Polisi linawashikilia askari wake watano kwa kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu

BUSHU3

Member
Apr 8, 2021
71
72
POLISI WEB .jpg

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia Askari watano wa Jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia kuwapeleka nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amethibitisha kukamatwa kwa Askari hao.

Aidha Kuzaga ametoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Chanzo: EATV

=============

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia Askari Polisi watano kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu Raia wa Ethiopia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amethibitisha Askari hao kukamatwa ambao ni ASP Thomas Bwire, Beda Moriss, Saimon Billia, Mohamed Ndunguru na Joseph Manumbu.

Kamanda kuzaga amesema Octoba 20 majira ya saa 10: 45 asubuhi huko kituo kidogo cha Polisi Uyole jijini Mbeya, Askari hao walikamatwa wakiwa na wahamiaji haramu sita Raia wa Ethiopia wakiwa ndani ya gari yenye namba za usajili T. 946 BTT, Toyota Cresta ambayo ni mali ya Askari Billia kufuatia taarifa kutoka kwa msiri kuwa walikuwa walikuwa wakipanga njama za kutaka kuwasafirisha wahamiaji haramu kwenda nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu Kyela.

“Natoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu na litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo bila kujali cheo chake," amesema Kuzaga.

Mwisho.
 
Hamna lolote hapo, nisawa na kujitekenya mwenyewe alafu uanze kucheka.
 
Tena wachukuliwe hatua kali, wasipewe hata dhamana, maana wanaliaibisha Jeshi letu la polisi.

Kuna polosi wachache wanao litia doa Jeshi letu. hao wachache wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo.

Kama huna maadili hufai kabisa kuwa askari ni bora ukatafute kazi nyingine.
 
Kuna kqzi isiyohitaji maadili? Hao ni kuwashughulikia tu kimidhamu.
 
Wahamiaji haramu Kwa nchi hii ni maigizo ebu fikiria HAO wahamiaji haramu waliokiteka Kikosi kizima cha Polisi ni wale wanaovuka kwenda nchi za mbali na wanatumia siku chache tu Lakini wapo WALIOBOBEA na kuishi Nchini wakiwa wameiteka Serikali ya Kijiji na Kupewa vitambulisho vya taifa na kuruhusiwa kununua Ardhi za watanzania kinyume na sheria za nchi HAO hawakamatiki ni Rushwa KWENDA MBELE.
 
Mtuhumiwa ni ASP, kwa cheo hicho atakuwa ndiye mkuu wa kituo.

Wengine ni mashahidi tu. Na wataachiwa.

Rejea kesi ya wale polisi wa mwanza /geita walioeskoti dhahabu akiwemo rco.

Jpm alivoisimulia ndg wa wale asikali tulijua wanakatwa vichwa.
Machz wapo huru.
 
Utajiri ulio na shaka pamoja na umiliki wa mali kharamu ni vitu ambavyo kama askari polisi wamejihalalishia.Wakumbuke na fedha za Zumaridi milioni 19 walipora.
 
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia Askari watano wa Jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia kuwapeleka nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amethibitisha kukamatwa kwa Askari hao.

Aidha Kuzaga ametoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Chanzo: EATV

=============

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia Askari Polisi watano kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu Raia wa Ethiopia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amethibitisha Askari hao kukamatwa ambao ni ASP Thomas Bwire, Beda Moriss, Saimon Billia, Mohamed Ndunguru na Joseph Manumbu.

Kamanda kuzaga amesema Octoba 20 majira ya saa 10: 45 asubuhi huko kituo kidogo cha Polisi Uyole jijini Mbeya, Askari hao walikamatwa wakiwa na wahamiaji haramu sita Raia wa Ethiopia wakiwa ndani ya gari yenye namba za usajili T. 946 BTT, Toyota Cresta ambayo ni mali ya Askari Billia kufuatia taarifa kutoka kwa msiri kuwa walikuwa walikuwa wakipanga njama za kutaka kuwasafirisha wahamiaji haramu kwenda nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu Kyela.

“Natoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu na litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo bila kujali cheo chake," amesema Kuzaga.

Mwisho.

Hao jamaa wanavyotoa hela ndefu walah hata mie nawasafirisha
 
Tena wachukuliwe hatua kali, wasipewe hata dhamana, maana wanaliaibisha Jeshi letu la polisi.

Kuna polosi wachache wanao litia doa Jeshi letu. hao wachache wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo.

Kama huna maadili hufai kabisa kuwa askari ni bora ukatafute kazi nyingine.
polisi wanaolitia doa jeshi la polisi ni wengi kuliko walio wasafii
 
Ukiona polisi wanafikia mpaka hatua ya kukamatana wenyewe kwa wenyewe, basi utambue fika wamepata shinikizo kutoka kwa wanasiasa; mfano Mkuu wa Wilaya, au Mkoa!

Kinyume na hapo, ni kulindana tu.
Saivi kila sehemu kuna vyanzo vya usalama wa taifa so ukifanya baya mwenzako anakuripoti na mnakamatwa wote mwisho wa picha yeye anaachiwa huru nyie mnahukumiwa..msicheze na vyombo vya dola
 
Back
Top Bottom