Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,673
- 22,264
Haya ndiyo mambo muhimu sana kwenye kudhibiti ajali za barabarani;
~ Iwekwe sheria ambayo itahakikisha kabla ya anayetaka leseni ya udereva pamoja na mafunzo anapimwa macho na dakitari wa polisi au wa hosipitali ya serikali, madereva wengi wana tatizo la mtoto wa jicho ambalo husababisha uono hafifu wakati wa usiku hasa macho yanapoangalia mwanga wa taa, tatizo hili ndilo chanzo cha magari kugongana yanapopishana.
~ Trafiki wapige marufuku matumizi ya diski za breki zinazochongwa mitaani na kubandikwa kwa gundi za viatu, hawa ajali ikitokea husingizia breki ilifeli kumbe gundi iliyeyuka na kusababisha breki isifanye kazi.
~ Mwisho matairi ya kuchongwa, matairi haya kwa hapo Dar yanachongwa karibu na kituo cha polisi Chang'ombe Temeke. Matairi haya huchongwa kurudishia mifereji (kashata) iliyokwisha, uchongaji huu husababisha tairi kulainika na gari kuyumba litembeapo pia kushindwa kusimama haraka breki ifungwapo.
Ninaamini endapo mambo haya niliyoyataja yatatekelezwa yataweza kusaidia sana kupunguza ajali kwani madereva wengi wanaona vizuri nyakati za mchana lakini wanauono hafifu sana usiku.
Sijui uhakiki wa leseni ni nini, leseni husika hupitia mikononi mwa trafiki na mtoaji ni TRA, sasa wanahakiki nini! Labda watueleze kama zipo leseni zinazotengenezwa mitaani.
Kuhusu vyuo, vingi havina walimu, mabasi na malori ya kufundishia madereva, wengi wao huanzia udeiwaka kwenye daladala kisha kwenye mabasi na utawakuta kwenye malori.