chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. chakii

    JamiiForums Tanzania Mbona Serikali imetugawa katika chanjo ya COVID-19?

    Leo katika hotuba ya MH Rais amesikika akisema wameshakubalia taasisi mbalimbali kuagiza chanjo za aina wanayoitaka wao, taasisi mojawapo ni ya Mzee Azim Dewji. Najiuliza mbona suala kama hili la chanjo Serikali inashindwa kuwa na kauli moja ya aina ya chanjo itakayowafaa Watanzania ukizingatia...
  2. N

    JamiiForums Tanzania Ushauri wangu kwa Serikali, Naomba Chanjo iwe lazima hatutaki kuangamizwa na wapuuzi wachache

    Tuko tunapambana kuona ni jinsi gani janga la Corona linaisha kabisa tuendelee na mambo mengine, tumechoka kuzika viongozi kila mwezi. Haya mambi ya kubembeleza watu ambao wameshaungua akili yamepitwa na wakati. Haiwezekani wengine wachanjwe wengine wakatae waendelee kusambaza maambukizi huu...
  3. C

    JamiiForums Tanzania Ikulu, imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?

    Au sisi wengine ni washamba jamani? --- Rais wa USA, Joe Biden akichomwa chanjo === Wizara ya Afya watoa ufafanuzi kuhusu hoja hii, soma hapa chini: -...
  4. Patrick Girigo

    JamiiForums Tanzania Haki ya kila Mtanzania kupata Chanjo ya COVI 19 sawa na Ibara ya 12 na 13 za Katiba yetu ya 1977

    Nampongeza Rasi na Waziri wa Afya kwa kufanikisha upatikanaji wa chanjo ya covid 19 angalau dose 1,000,000 sio haba. Kwa kuwa kila Ofisi ya Umma huanzishwa kwa mujibu wa sheria/Katiba na kwa kuzingatiakuwa kila Kiongozi huapa kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Katiba ya Tanzania ya 1977...
  5. J

    JamiiForums Tanzania Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

    Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo. Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo. Askofu Gwajima amewataka wafuasi...
  6. L

    JamiiForums Tanzania Mkanganyiko wa chanjo ya Corona

    Baada ya mheshimiwa Rais Samia kutoa mwelekeo wa taifa kuhusu mapambano ya Corona zimeibuka hoja nyingi sana hasa kuhusu hizi chanjo. Jana nilipata nafasi ya kumtembelea rafiki yangu hapa Morogoro. Nilichokisikia sikuamini. Watumishi wengi wa kada moja iliyopewa kipaumbele cha kupata hawataki...
  7. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Uviko-19 na chanjo zake

    #SisiTanzania #WeTanzania 28/Julai/2021. UVIKO19 NA CHANJO ZAKE. Habari yako mtanzania. Unafahamu kuhusu UVIKO19 na chanjo zake? UVIKO19 ni gonjwa lililoikumba Dunia nzima na kuiacha mdomo wazi mwishoni wa mwaka 2019 ikianzia mabara jirani na kuingia Afrika kwa kasi mwaka 2020. Mpaka sasa...
  8. Nawatania

    JamiiForums Tanzania Chanjo ya covid-19 inatolewa hospital gani nikachanjwe?

    Wakuu hospital gani hapa dar inatoa chanjo na masharti gani yanatakiwa ili nipate chanjo? Mwenye kujua anipe utaratibu.
  9. G

    JamiiForums Tanzania Wasioitaka chanjo ya korona Tanzania hawa hapa

    Pita sehemu mbalimbali hapa Tanzania ambako kuna ulazima wa kuvaa barakoa. Kisha angalia idadi ya watu waliovaa barakoa kwa hiari yao. Ni wachache sana. Ukiangalia makanisani, misikitini, viwanja vya michezo, masokoni, harusini, vyombo vya usafiri , minqdani, n.k watu hawana habari na barakoa...
  10. Leak

    JamiiForums Tanzania Rais ulifanya makosa makubwa kuifanya chanjo kuwa hiari, ulipaswa kukubaliana na Mbowe kuwa chanjo lazima ili tuweze kupambana na Gwajima

    Wasalaam wana jamvi. Mimi ni mmoja wa watu ambao kusema kweli nilitamani kabisa swala la chanjo liwe kwa lazima kwa kila mtanzania na hili lilipaswa kuwekwa wazi kabisa na Mh Rais pale alipotangaza ujio wa chanjo hiyo kwani ingesaidia sana kupambana na watu wanaopinga chanjo hiyo. Nakumbuka...
  11. Meneja Wa Makampuni

    JamiiForums Tanzania Msiingize uchama kwenye suala la chanjo, chanjo si mali ya chama

    Jamani chondechonde msiingize swala la chanjo kwenye uvyama chanjo sio mali ya chama. Waelimisheni watanzania wote vile ambavyo wewe unaelewa kuhusu chanjo. Mtu akizungumza jambo tusikurupuke kuanza kuliingiza kwenye mambo ya chama hapo tunakua hatutumii akili zetu sawa sawa. Ukiona mtu...
  12. mshale21

    JamiiForums Tanzania UVCCM: CCM imchukulie hatua Askofu Gwajima kwa kuhamasisha Watanzania kukataa chanjo ya Uviko-19

    Dodoma. Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19. Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa...
  13. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Kassim Majaliwa: Hakuna mtu aliyelazimishwa kuchanja chanjo ya UVIKO-19

    WAZIRI MKUU WA TANZANIA, NDUGU. KASSIM MAJALIWA: HAKUNA MTU ALIYELAZIMISHWA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19. Awataka wananchi wapuuze upotoshwaji unaoendelea mitandaoni WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haijamlazimisha na wala haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya ugonjwa wa...
  14. J

    JamiiForums Tanzania #COVID19 NIMR: Chanjo zitakazotolewa Nchini ziko salama kwa asilimia 99.9

    Baada ya ufafanuzi mzuri wa kisayansi uliotolewa na Mkurugenzi mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya kupitia Clouds tv sitashangaa kumuona Askofu Gwajima akibadili mawazo na kutimba Ikulu kupata chanjo hapo kesho. Prof Yunus Mgaya amesema chanjo ya Johnson & Johson inaweza kuwaathiri watu 4 tu...
  15. Suley2019

    JamiiForums Tanzania Viongozi wa dini wakubali kufata maelekezo ya Wataalamu wa Afya katika kukabiliana na Covid-19

    Viongozi wa umoja wa dini mbalimbali umesema msimamo wao katika mapambano ya ugonjwa wa Covid-19 ni kusikiliza sauti za wataalamu na wanasayansi ikiwemo maamuzi ya chanjo ya kupambana na ugonjwa huo. Kauli ya viongozi hao imekuja siku chache baada ya chanjo zaidi ya milioni 1 za Covid - 19...
  16. Richard

    JamiiForums Tanzania Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia

    Utangulizi- Nawaomba Mods msihamishe uzi huu. Mchungaji Josephat Gwajima asimamia maeneo mawili katika hoja yake. Kwanza, kilichomo kwenye chanjo na pili chanjo dhidi ya wanajeshi na walinda usalama wa nchi. La kwanza kuhusu kilichomo kwenye chanjo au (content). Mchungaji Gwajima anadai ni...
  17. R

    JamiiForums Tanzania Mbona hamjahoji kuhusu Panadol, Aspirin na ARVs kuwa wazungu wanaweza "kutufanyizia"?

    Makelele mengi kuhusu chanjo ya corona, mbona hamjahoji au kukataza dawa/chanjo tunazozitumia hospitalini leo hii? Aina za chanjo ambazo kila mtoto wa Kitanzania anazipata na zinatoka west/USA BCG (Bacile Calmette-Guérin) DTP au DPT (Dondakoo, Pepopunda na Kifaduro) Surua Polio Magonjwa haya...
  18. beijing_07

    JamiiForums Tanzania Gerson Msigwa: Watanzania wawasikilize wataalamu, chanjo za COVID-19 zinahakikiwa na TMDA na Mkemia Mkuu

    Mtangazaji: Tuanze na suala la chanjo, tumepata taarifa kesho Rais Samia Suluhu atazindua utaratibu wa chanjo na yeye atachanjwa. Utaratibu utakuwaje kama umeshawekwa na Serikali? Msigwa: Baada ya kuwasili dozi za chanjo zaidi ya milioni 1, kesho asubuhi mheshimiwa Rais atazindua zoezi la...
  19. S

    JamiiForums Tanzania Mapokezi ya chanjo ya Covid-19 yapo hasi sana kwa Watanzania

    Ukiacha Gwajima kuchafua hali ya hewa kuhusiana na chanjo ya Corona lakini tayari watanzania walishaaminishwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati Magufuli kuwa chanjo ya Corona sio salama kabisa na hivi huku hayati akisema kuwa chanjo ya Korona inayopigiwa debe na mabeberu kama alivyokuwa anasema...
  20. Hance Mtanashati

    JamiiForums Tanzania Ofisi nyingi hazitaruhusu watu kuingia bila kuwa na chanjo

    Japo kwa sasa wanasema chanjo ni hiyari, lakini ninapenda kuwahakikishia huko mbeleni hakuna ofisi yoyote ya Serikali utakayoweza kuingia bila ya kuwa na kibali cha chanjo. Kwa namna moja au nyingine itatulazimu na sisi tusiotaka kuchanjwa tuchanje bila kupenda maana hatutakuwa na jinsi. Kwa...
Back
Top Bottom