chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania Marekani kuanza utoaji wa chanjo ya COVID mwanzoni mwa Desemba

    Marekani inataraji kuanza utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa juu wa afya katika serikali ya Marekani. Kuanza kutolewa kwa chanjo kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika mapambano ya virusi hivyo ambavyo...
  2. Red Giant

    JamiiForums Tanzania Afrika inatakiwa tujenge taasisi yetu ya kutafuta tiba na chanjo

    Habarini wakuu. Iko hivi, utafiti wa dawa hadi ikaingia sokoni ni gharama kubwa sana na una mlolongo mrefu balaa. Hugharimu mabilioni ya dola na makumi ya miaka. Makampuni mengi kabla ya kufanya utafiti wa dawa kwanza huangalia kama italipa? Je wanaoumwa wanaweza kununua dawa? Hii imepelekea...
  3. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania WHO : COVID-19 bado tishio licha ya mafanikio ya majaribio ya chanjo

    Tedros Adhanom Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema kuna kazi kubwa inayohitajika kupambana na janga la virusi vya corona licha ya kuwepo na habari nzuri wiki hii kuhusiana na mafanikio ya majaribio ya chanjo. Akizungumza kutoka Geneva...
  4. Sam Gidori

    JamiiForums Tanzania Guterres: Hatutakiwi kuyasahau hata maisha ya mtu mmoja aliyetutoka

    Vifo vinavyotokana na maabukizi ya virusi vya corona vimezidi watu milioni moja, kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha John Hopkins, huku Shirika la Afya Duniani likionya kuwa idadi hiyo inaweza kuwa ndogo zaidi ikilinganishwa na uhalisia kutokana na changamoto katika upatikanaji wa takwimu...
  5. beth

    JamiiForums Tanzania Urusi yaidhinishwa chanjo ya kwanza ya CoronaVirus duniani

    Rais Vladimir Putin ametangaza kuwa Urusi imeidhinisha rasmi chanjo ya COVID19 iliyotengenezwa na Taasisi ya Galameya iliyopo Mji Mkuu wa nchi hiyo, Moscow Akizungumza na Mawaziri kupitia mtandao, Rais Putin (67) amesema hii ni mara ya kwanza kwa chanjo dhidi ya CoronaVirus kuidhinishwa duniani...
Back
Top Bottom