Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,187
- 42,011
Wasalaam wana jamvi.
Mimi ni mmoja wa watu ambao kusema kweli nilitamani kabisa swala la chanjo liwe kwa lazima kwa kila mtanzania na hili lilipaswa kuwekwa wazi kabisa na Mh Rais pale alipotangaza ujio wa chanjo hiyo kwani ingesaidia sana kupambana na watu wanaopinga chanjo hiyo.
Nakumbuka hivi karibuni Mh Mbowe aliweka wazi kabisa kuwa anataka serikali itoe chanjo kwa watanzania wote kwa lazima lakini alipata upinzani mkubwa kutoka kila upende na watu tukasahau kuwa kuna wamba watatumia huo mwanya wa chanjo ya hiari kuipinga chanjo na kuwatisha na kuwahamasisha wengine wasiende kupata chanjo kwani sio lazima. Kwa hiyo mtu akishawishiwa kutokwenda na asipo kwenda hakuna kosa kwani ni hiari Mtu akishawishiwa kwenda na akafanikiwa kwenda bado hakuna kosa lolote.
Madhara ya chanjo ya hiari ndiyo haya lazima watazuka watu kutoa maoni yao na watazuka watu kuwahamasisha watu kutochanjwa hivyo ni lazima tukubali kuwa watu wameamua kuutumia mwanya uliotengenezwa na mamlaka zenyewe hatupaswi kuwatisha bali nasisis tuwashawishi wengine wakachanjwe lazima kuna mmoja wetu atafanikiwa.
Kuwashambulia watu ambao tumewapa uhuru sisi wenyewe kwani ni sisi tuliosema kuwa chanjo ni hiari kwa hiyo kamwe hatupaswi kusema kuna watu wanapotosha bali tunatakiwa kutoa elimu juu ya chonjo na kuwashawishi watu wakachanjwe.
Ukweli ni kwamba watu walipaswa kupewa elimu kuhusu chanjo lakini kwakuwa serikali haikutoa elimu kuhusu chanjo basi tumetoa mwanya wa watu kufundishwa na watu ambao pengine tusingependa na hayo ndio madhara ya chanjo ya hiari.