mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
795
1,000
Dodoma. Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema

Source: Mwananchi
 
Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
636
1,000
1627389167808.png

Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema
 
Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,366
2,000
Kumpoteza chamani mtapata hasara kubwa sana.

Mlimnunua kwa gharama ya rushwa ya kupora jimbo kwa nguvu. Kura zikatapakaa ktk hili jimbo kwenye mabegi halafu mumpoteze hivi hivi hapana!

Gwajima ni mtu wa kubadilika badilika na uzuri haoni hata aibu. Leo ni wa baridi kesho ni wa moto, jumapili yuko mimbarani akihubiri injili, jumatatu yuko kwenye kikao cha ndani cha kupanga wizi wa kura nk.

Ati apeleke malalamiko kwenye vikao vya ndani? Hawezi yule kuna siku ataamka amtukane mwenyekiti matusi ya nguoni kama alivyofanya kwa kadinali Pengo.

Hakuna namna kaeni nae hivyo hivyo tu!
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,766
2,000
CCM na Serikali yake inamuogopa sana Askofu Rashid Gwajima na haina uwezo wa kumfanya lolote,huu ndiyo ukweli wenyewe na akitaka anaweza kuisambaratisha kabisa CCM kwa masaa 24.
Hujui ulisemalo, kama Bashite tu aliweza kumlaza ndani sembuse serikali nzima ikiamua? 2015 aliwekwa ndani na Kikwete akazimia mahabusu! Mnapenda sana kuwaoverrate matapeli.
 
BoyOfGod

JF-Expert Member
Jan 3, 2019
303
500
Aisee yaani mtu kaongea kanisani like a pastor na sio mwanasiasa wamuadhibu kwa lipi

And by the way hata wafanyeje chanjo mma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom