#COVID19 Haki ya kila Mtanzania kupata Chanjo ya COVI 19 sawa na Ibara ya 12 na 13 za Katiba yetu ya 1977

May 30, 2020
48
125
Nampongeza Rasi na Waziri wa Afya kwa kufanikisha upatikanaji wa chanjo ya covid 19 angalau dose 1,000,000 sio haba. Kwa kuwa kila Ofisi ya Umma huanzishwa kwa mujibu wa sheria/Katiba na kwa kuzingatiakuwa kila Kiongozi huapa kuilinda, kuihifadhi na kuitetea Katiba ya Tanzania ya 1977; Nimesikiliza hamasa ya Viongozi wa Dini wote leo walioalikwa na serikali yetu kujenga imani kwa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo; Nami nakubaliana na maneno yao na maelekezo ya serikali,
Kwa kuzingatia ibara ya 12 ya Katiba kwamba Binadamu wote ni sawa na huzaliwa huru na ibata ya 13 kuwa Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki ,bila UBAGUZI wowote ,kulindwa na kupata HAKI sawa mbele ya sheria, napenda kujua mikakati ya serikali kuagiza CHANJO zingine angalau milioni 15 kwa ajili ya wananchi wa Tanzania ili kuwakinga na huu ugonjwa mbaya.

Viongozi wa Kiroho wametoa kauli nzuri zenye kujenga imani na umuhimu wa Chanjo na kwa kauli hizo, nami nimeshawishika kuhakikisha mama na baba yangu wakiwa huko Kijijini kwetu wanafikiwa na chanjo bila kuchelewa.
Kwa kuwa ni kweli kuwa ugonjwa huu ni hatati na unaua na unahitaji kutokomozwa kwa njia zozote, na kwa kuwa AFYA za watu ni muhimu kuliko MAJI,BARABARA,UMEME, nk ni wakati sasa wizara yetu ya afya kuja na Mkakati dhabiti wa kuagiza chanjo zaidi ya milioni 15 kwa ajili ya wakazi wa Vijijini hasa huko ambako hakuna hata Hospitali,Vitup vya Afya, Zahanati ili kuokoa Uhai wa wazee wetu waliopambana kuijenga Nchi hii katika hali zote.

Kuna dhana inayoitwa DEMAND CREATION= kwamba chanjo milioni 1 zilizotolewa kwa watu milion 1 zitaamsha ari na uhitaji mkubwa wa wananchi kutaka kukingwa Afya zao hasa wale ambao ni SENIOR CITIZENS 15 to 20 Milions. Kadri tunavyoamsha demand creations kwa wananchi kuhitaji na kuiamini KINGA ya Covid 19, ni wakati sasa Wizara kuweka namna ya SUPPLY SIDE ya chanjo zingine kwa watumiaji wengi.

Nilikuwa Kijijini kwetu kwa siku 14 na nilipata fursa ya kuongea na watu/wazee ambao wana zaidi ya miaka 50, wengi wanakubaliana na CHANJO na wameona athari za covid19 hasa kwa watu wao wa karibu, aidha wapo pia wachache ambao wanaamini NYUNGU,KUJIFUKIZA na kula Malimao au Tangawizi, hao nao wapo japo wakipata facts za Kisayanis wataungana na wataalam kupata chanjo.

Hivyo basi, kwa misingi ya Kikatiba, kwamba watu wote ni sawa, na hakuna ubaguzi wowote na kwa kuzingatia maelekezo ya serikali na viongozi wa Dini, naomba SUPPLY SIDE iimarishwe na utolewe ufafanuzi wa lini wale walioko pembezoni watafikiwa kukinga afya zao; issue ya ubora/efficacy ya chanjo sio hoja kubwa kwa wazee wetu au wananchi wanaopata madhila ya UVIKO.


Ibara ya 29 inasema kuwa Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa jamii,kama zilivyofafanuliwa katika ibara ya 12 hadi 28 za sehemu hii ya sura hii ya Katiba.

Joshua 24:24 inasema kuwa chagueni hivi leo mtakayemtumikia, ila Mimi na Nyumba yangu tutamtumikia MUNGU, na kwa namna hiyo pamoja na wazazi wangu tupo tayari kuwashawishi wapate chanjo,nao wapo tayari.


So Demand side must be = supply side

Tutaishinda covid19 kwa pamoja na kwa umoja pamoja na Bwana
 

Hadrianus

JF-Expert Member
Feb 19, 2020
1,173
2,000
IMG_20210728_111238_711.JPG
 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,621
2,000
Muhimu ni ile form tu ambayo unajaza kuwa litakalokupata baada ya kudungwa hilo chanjo ni juu yako, hilo ndio muhimu mengine yote ni makelele tu.
 
May 30, 2020
48
125

Mens sana in corpore sano= Healthy BODY health MIND


Hakuna ushahidi wowote uliotolewa hadi sasa na watu wanaopinga chanjo kuwa covid19 sio ugonjwa? Je watu hawafi/hawapati madhara na huu ugonjwa? Je huu sio ugonjwa bali ni VITA ya Kiroho- a Spiritual warfare? Kwa kuwa bado binadamu ni mtu mwema mbele za MUNGU kwa kuzingatia kuwa tunapaswa kuwajibika mbele za JAMII na mbele za MUNGU kwa maisha na matendo yetu, ni wazi kuwa JUKUMU mojawapo la mtu mwenye AKILI timamu ni pamoja na kujilinda dhidi ya vitu vinavyohataisha UHAI wake au wa familia yake, ikiwa ni pamoja na kunywa MAJI safi na salama, kulala mahali safi, kupata MLO KAMILI, kulala ndani ya chandarau au kuzuia Mbu kuingia ndani, kujiepusha na wanyama wakali kama Nyoka nk,
Hizo zote ni juhudi za kujiweka salama ili tuweze kutimiza Kusudi la MUNGU la kutuumba kwa SURA na MFANO wake, hivyo basi CHANJO ni miongoni mwa juhudi za kupambana na vitu viovu vyenye kuhatarisha maisha/Uhai wa binadamu ambaye ni kiumbe mwema wa Mungu.
Biblia ni SAUTI ya Mungu na imeweka wajibu mkubwa wa Mwanadamu kuitunza na kuilinda Bustani pamoja na Mwili wake ambao ni hekalu la Roho wa Mungu; Wote wanaoipinga chanjo kwa hoja za Kidini bado hawana hoja zozozte zenye utukufu mbele za Mungu zaidi ya hofu na wasiwasi wao wenyewe. Marko 15:16 inasema hata mkila vyakula vya kufisha au mkishika nyoka,Nge havitawadhuru kwa sababu tunalindwa na nguvu za Mungu mwenye huruma,upendo,msamaha na wa HAKI pia.


Sin.jpg
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,783
2,000
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom