Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,840
2,000
36EF381F-4EDC-4F5C-8A82-FB314AD4EE36.jpeg

Mzee wa upako, Athony Lusekelo ameitwa kufungua kwa sala na kabla anatoa maneno machache ikiwemo kutaka watanzania kuiamini chanjo kwani Serikali imejiridhisha.

Pia ameongelea kauli ya Magufuli na kusema hakukataa bali alitaka tahadhari, Mwisho amesema wakristo kuna mambo wanakubaliana wote kwa pamoja.


WAZIRI WA AFYA, GWAJIMA
=>
Leo ni siku ya kihistoria ambayo tunachukua silaha za kisasa kwenda kupambana na Uviko

= > Hayati Magufuli alisema wizara ya Afya isikimbilie machanjo bila kujiridhisha, leo kuna watu wanapotosha.

=>Huko, Vifo vilikuwa vinafika 3000 mpaka 4000 kwa siku sasa hali imebadilika

=> Eti chanjo inavuruga utu wa mtu, ni uongongo, tutalieleza. Wa HIV ndio angeenda kupangua huo utu.

=> Maabara tunazo, wataalam tunao. Watanzania wasiwe na hofu. Vitu vyote hakuna visivyo na madhara lakini tunaoutways faida kuliko madhara. Mbona ukinywa Quinene kichwa kinauma, fragile ambae ni malkia wa maumivu ya tumbo pia ina madhara.

=> Mie ndio waziri wa Afya nimeapa, siwezi kumshauri Rais vibaya, naomba wanahabari mzingatie maadili yenu, wale mnaokata ujumbe usiojitosheleza kuongeza followers Mungu anawaonaWAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA
=>Nikiwa mwenyekiti wa kamati inayoratibu ugonjwa wa Covid, tukuhakikishie tunaendelea kukaa pamoja, kuratibu na kushauri pia tumeendelea kupokea miongozo ya kitaalam kutoka kwa wataalam wetu.

=> Hatua mbalimbali zimechukuliwa duniani kote, tumepata uzoefu ikiwemo uchanjaji na leo tumeanza kuhamasisha watu kuchanja kudhibiti ugonjwa huu. Wataalam wamepata elimu ya kutosha ndani na nje ya nchi.

=> Mie nimekubali kuungana nawe kuchanja kuonyesha Serikali haina nia mbaya kwa wananchi wake, Mheshimiwa Rais ameapa kulitumikia Taifa hili, tunachokileta kwenu kimetokana na utafiti, sisi tuko pamoja nawe na maamuzi haya tunakupongeza sana.

=> Huku tumefanya mambo mengi, Mheshimiwa Rais leo ni siku yako.


RAIS SAMIA SULUHU
=> Juzi kupitia ubalozi wa Marekani tumepokea chanjo hizi, leo baada kuthibitishwa na wizara ya Afya tunaanza kuzitumia. Niwashukuru wote mlioko hapa kuniunga mkono kuonyesha chanjo sio balaa

=> Kuna ambao wanalikataa lakini wengi wanalikubali, jana nilikuwa na mazungumzo na CDC na alinieleza jinsi umoja wa Afrika tulivyojipanga kukabiliana na jambo hili na jana alitaka tuweke oda yetu ya chanjo, tumetengeza fungu la fedha na jana tumeweza kuweka oda yetu

=> Jitahada zitafanywa kwa wale wote ambao wako tayari kuchanjwa kuhakikisha inapatikana. Kwenye mwili wangu nina chanjo tano na leo ya sita, madhara yalikuwepo wakati ule lakini tulipona na tupo tunaendelea, chanjo ni imeni na kwa wale wenye imani potofu wizara mfanye kazi

=> Pamoja na chanjo nirudie wananchi kuchukua tahadhari, wasanii wamesema vizuri.

=> Kama haujaguswa na maradhi unaweza sema unavyoweza, ila walioguswa na wanatamani kupata chanjo hata sasa hivi

=> Johnson & Johnson ni chanjo moja tu, zile nyingine ndio unachoma mbili. Mtakaochoma leo, msiache kujilinda kwa kuwa wengine hawajachanja bado.


VIDEO: HOTUBA YA RAIS SAMIA SULUHU

 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,753
2,000
Mzee wa upako ameitwa kufungua kwa sala na kabla anatoa maneno machache ikiwemo kutaka watanzania kuiamini chanjo kwani Serikali imejiridhisha. Pia ameongelea kauli ya Magufuli na kusema hakukataa bali alitaka tahadhari, Mwisho amesema wakristo kuna mambo wanakubaliana wote kwa pamoja
Mzee wa upako kaitwa amjibu gwajimahaya mambo haya..raha tupu wallah
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom