Recent content by GJ Mwanakatwe

  1. G

    Muungano umeathiri zanzibar kukuwa kimaendeleo-Mbunge

    Mbunge kama huyu mwenye mawazo mgando, mawazo ya sisi wazanzibar wao watanganyika, sisi waunguja wao wapemba hatufai, ni mzigo kwa taifa. Badala ya kuzungumzia kipi tufanye kuijenga tz yetu yeye anazungumzia mambo ambayo hata utafiti hajayafanyia,namuomba kipindi hiki kikiisha apumzike asirudi...
  2. G

    Aliyeanzisha Udini Tanzania ni Nyerere

    Sasa kama angepandikiza udini miaka hamsini iliyopita hilo zao la udini liko wapi mbona hatulioni, wacha fikra za udini weye.
  3. G

    Viongozi wa dini: Tumechoka wageni kunufaika na rasilmali za Watanzania

    Ni kweli kabisa waliyosema viongozi wa dini kwamba wageni wanafaidi resources zetu na kutuacha sisi maskini wa kutupwa. Hali hii inahatarisha usalama wa taifa letu, na mfano ni tarime. Hivyo ni vizuri serikali ikachukua hatua za haraka kurekebisha hali hii kabla mambo hayajaharibika kabisa la...
  4. G

    Hamad, Cheyo, Mrema: WanaCCM ndani ya Upinzani...

    Tanzania ni nchi tajiri sana ila ina umaskini mkubwa wa kuwa na viongozi bora, tatizo haina viongozi bora.
  5. G

    Kampeni Kupinga 'chenji' ya fedha za Radar wasipewe tena Serikali

    Hamna kitu kama hicho, fedha zile ni za serikali ya Tanzania, ni lazima zirudi kwenye mikono ya serikali, kama serikali ikizifanyia ufisadi hilo ni suala lingine, lakini kwanza zirudi serikalini hiyo ni hatua ya kwanza. BAE hawana mamlaka na fedha hizo, kwanza hata BAE ni wezi, sasa vipi fedha...
  6. G

    Hivi ni kweli Wabunge wa CCM hawajui kwamba wanajimaliza!

    Kwa mwendo huu maendeleo ya tanzania ni ndoto milele, wafanyakazi wa kawaida hasa walimu mishahara kiduchu, halafu upande wa pili posho moja tu sawa na mshahara wa mwalimu wa mwaka mzima, haki hapa ipo wapi? hapana kitu hiki ni lazima kikomeshwe.
  7. G

    J.K Nyerere na siasa za maji taka

    Wacha hiyo, Nyerere huwezi kumdhihaki kwa sababu zisizo na sababu, alikuwa ni kiongozi bora hakuna mfanowe mpaka sasa. Kambona alikuwa anataka ubepari nyerere ujamaa, ndo tofauti yao na ndicho kilichomkimbiza kambona nje. Kama mpaka sasa nchi haipo na haikuwa tayari kwa ubepari, vipi wakati ule...
  8. G

    Naomba Mungu Rev. Msigwa ashindwe kuthibitisha

    Afadhali kinachotakiwa kuthibitishwa kingekuwa kinahitaji ushahidi kweli, kwa kuwa mengi ya yanayohitajiwa kutolewa ushahidi yapo wazi, sasa ushahidi wa nini? ni kupotezeana muda tu.
  9. G

    CHADEMA, kama Pinda analipwa per diem ni wizi mkubwa zaidi

    Kwani takukuru waliishia wapi na uchunguzi wao wa wabunge kulipwa posho mara mbili? au ilikuwa ni gia ya kuwatishia wabunge ili waache kumtaka mkurugenzi huyo ajiuzulu? Tanzania inabomolewa na watanzania wenyewe, hasa wanasiasa na watumishi wa umma.
  10. G

    CHADEMA watoana macho Bungeni

    Hiyo ndiyo demokrasia, sio lazima kila kitu wakubaliane wote, na hii siyo kwa upinzani tu bali hata kwa chama tawala hawatakiwi kila kitu kupinga kwa kuwa kimetoka upinzani au kuunga mkono kila kitu kwa kuwa kimetoka chama tawala, no, wote wanatakiwa kupinga au kukubali hoja baada ya kuichambua...
  11. G

    Fidel Castro:Mbuyu uliowashinda wamarekani

    ni kweli huyu ni kiongozi shupavu, anapaswa kuigwa na viongozi wa afrika, ambao kwa ujumla wapowapo tu hata hawaeleweki wanalofanya.
  12. G

    Utendaji wa Jeshi la Polisi Nchini Ukoje?

    Tusizunguke, kwa ujumla utendaji wa jeshi la polisi upo chini ya kiwango, yaani hauridhishi kabisa. Polisi wamegeuka kuwa kero badala ya msaada kwa wananchi, akili zao zote zipo kwenye rushwa. Nafikiri mafunzo wanayopata vyuoni kwao ni duni, na pia malahi yao duni na makazi mabaya huenda...
  13. G

    Kituko kingine cha Pinda

    Anachofanya ni kuvuta muda tu, kwani wezi hatua muafaka ni kuwashtaki tu, ushauri gani anataka?
  14. G

    Msaada: Faida za kusoma masters Ulaya/USA

    Faida yake ni kwamba utasoma kwa kutumia teknolojia na mazingira rafiki basi, hamna zaidi.
  15. G

    Waasi wa Libya wameishiwa ngawira!

    wAJINGA SANA hawa waasi, wanabomoa nchi yao kwa maslahi ya marekani na nchi za magharibi, hawajui kwamba shida ya hao jamaa ni mafuta tu hamna kingine.
Back
Top Bottom