Hivi ni kweli Wabunge wa CCM hawajui kwamba wanajimaliza!

Amiliki

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,085
1,004
Enyi Wabunge wa CCM, hivi hamjui kwamba mnachezewa kete ya hatari na Chadema ili mbele ya macho ya Watanzania muonekane kwamba hamna maana! Siku mtakapokuja kustuka itakuwa too late! Wanachokifanya Chadema ni kuleta hoja ambazo zina-reflect kilio cha Wananchi lakini nyie kwa Upofu wa kusahau wajibu wenu kama wabunge, mmeingiza ushabiki wa Kichama kwa kutetea kila kitu cha Serikali wakati wajibu wenu ni kukaa upande wa Wananchi waliowachagua ili kuibana Serikali. Kwa kufanya mnachokifanya kumepelekea sisi wananchi kuona kwamba kuna Watetezi wetu ambao ni Chadema wapo upande wetu wananchi tukipambana na Serikali wakisaidiwa na Wabunge wa CCM kwa upande wa pili. Kwa kifupi mnadhani mnajenga kumbe mnabomoa.

Ngojeni matokeo mtayaona 2015.
 
Tatizo lao bado wana amini watapita kwa kuchakachua.


"Tutaipigiania haki yetu kwa ajili yetu na vizazi vyetu...Tanzania ni yetu sote sisi na vizazi vyetu na wala si ya CCM na vibaraka wao..Ni heri kufa kishujaa lakini historia mpya ikiwa imeandikwa kuliko kufa kinafki" Ng'illy 8[SUP]th[/SUP] June, 2011
 
Mkuu sikio la kufa halisikii dawa. Hawa wakuda akili yao iko kwenye POSHO TUUUUUUUUUUUUUU
 
Baadhi ya wabunge wa CCM walitamani kutopitisha hii budget,lakini kwa kuwa ilikuwa ni kula ya uwazi, wakaona noma kusema hapana, maana baada ya bunge wangesutwa ndani ya chama, hata hivyo kwa mimi nawaona kama sio majasili, kwani katika kutetea haki ya wanachi hupaswi kuogopa, kwani miongoni mwa wanachi wanao suffer na life wamo, ndugu zao wengi. 2015 it will be their judgement, let wait and see what gonna happen,Eeh Mungu naomba unipe uhai ili ifikapo 2015 niweze kushuhudia yatakayo tokea.
 
labda Mungu kaibua haya mambo ili watu waashtuke, nadhani jeneza lipo tayari linasubiri sisi kuligongea msumari wa mwisho 2015 na magamba watakuwa rasmi chama cha upinzani.
 
Kwa mwendo huu maendeleo ya tanzania ni ndoto milele, wafanyakazi wa kawaida hasa walimu mishahara kiduchu, halafu upande wa pili posho moja tu sawa na mshahara wa mwalimu wa mwaka mzima, haki hapa ipo wapi? hapana kitu hiki ni lazima kikomeshwe.
 
Unachosema ndugu yangu ni kweli tupu. Wazee wa CCM wanaonekana kuitetea serikali pindi wawapo bungeni, ndiyo maana wabunge machachali tuliowaamini zamani wa CCM kama vile mama Marcela, Ndesambulo nk. sasa hivi hoi. Inawezekana katika vikao vyao wana ajenda moja tu ya kuattack hoja nzito za Upinzani (CHADEMA). Lakini naona wamekosea kwani watanzania tayari tunawaona makasuku, bora wachache wanaopenda kuonekana tena mjengoni wazikane ajenda hizi potofu.
 
Back
Top Bottom