CHADEMA, kama Pinda analipwa per diem ni wizi mkubwa zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, kama Pinda analipwa per diem ni wizi mkubwa zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Jun 21, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwa kuwa pm anatetea posho, nawaomba wabunge wa chadema muwashe moto zaidi. pm ana nyumba dodoma amepewa na serikali na akiwa hapo yupo nyumbani. je analipwa per diem ya nini wakati hiyo ni posho ya kuwa nje ya nyumbani? hii pia itumike kwa mawaziri na wabunge ambao nyumbani kwao ni dodoma.
   
 2. m

  mob JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  nadhani dodoma kuna residence homes kwa ajili ya makati wakuu na mawaziri.je zile nyumba za kisasa ni za akina nani
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya wanaharakati wote kulivalia njuga hili suala la posho; kwani ni mojawapo ya njia ambayo inatumiwa kujineemesha. Ni kweli mawaziri wengi wanapokuwa bungeni wanafikia kwenye nyumba za serikali huku wakilipwa siyo posho ya vikao, bali pia posho ya kujikimu. Siyo hiyo tu bali pia mawaziri nao wanalipwa shs. 2.5 milioni kila mwezi kwaajili ya lita za mafuta 1000 anazopewa mbunge kwaajili ya kutembelea jimbo lake, wakati mawaziri hao hutembelea majimbo yao kwa kutumia magari ya serikali.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Posho zitaibua mengi sana. Hivi mbunge wa Dodoma Mjini analipwa per diem?
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Naona taraaatiiibu mnakuja kwenye msimamo wangu. Msimamo wangu ni kwamba tuziangalie posho na marupurupu mengine yalipwayo kwa watumishi wa serikali kwa ujumla wake. Sasa yanaibuka haya ya mafuta, mawaziri kuwa na nyumba/rest houses dodoma na kulipwa per diem, mawaziri kulipwa mafuta huku serikali inawajazia mafuta kwenye magari yao, wabunge kusafiri kwa first class kwenye ndege, maafisa kutembelea mashangingi, nk . Kwa hiyo haya mambo yanatakiwa tupate stahili allowance zoote na marupurupu mengine yalipwayo serikalini ili tuwe na mjadala muafaka tusijikite kwenye posho za vikao peke yake. Tukijikita kwenye posho za vikao peke yake tutalimaliza hilo kesho tunashtuka aaah kumbe waziri analipwa per diem akiwa dodoma wakati anaishi kwenye nyumba ya serikali. Tunajadili linasha , tutaishia kujadili na kujadili. Hili inabidi tulimalize kisha tugeukie mambo mengine. Katiba inatusubiri.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Waziri kama hana nyumba Dodoma basi ana rest house inayohudumiwa na Serikali. Posho zitaibua mengi, nilisema.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wote wanazililia ni walafi tu.
   
 8. i

  iMind JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Ni kweli hata waziri na katibu mkuu wetu wana nyumba dodoma na ni juzi tu tumenunua generators mpya kwa ajili ya nyumba hizo. Lakini hupewa posho za kujikimu wawapo dodoma
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mbona hata shamba analo Dodoma,si tulionyeshwa kwenye gazeti akikagua shamba lake,wizi mtupu,hapaswi kupata posho akiwa nyumbani kwake ,kwani ofisi yake si iko Dodoma au huwa analipwa siku zote akiwa Dr es Salaam kwa vile ofisi yake iko Dodoma,kweli Tanzania shamba la bibi
   
 10. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  pinda ni mwizi tofauti yake na lowasa ni kuwa pinda anaiba kidogo lowasa alikuwa anakomba.
   
 11. m

  mukama talemwa Senior Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna kitu kingine huwa kinanikelra saana Waziri anasfari ya kwenda kwenye jimbo lake anamwambia Dreva atangulie na gari la serikali yeye kesho yake au baada ya siku tatu anapanda ndege yule dreva anaenda kumpokea airport,anakaasiku tatu anapelekwa airport na dreva kesho yake anawasha gari kurudu Dar.Hivi hilo gari analokopeshwa kwa ajili ya jimbo ake linakazi gani?na mafuta anayopewa ni kwa ajili ya nini?HUU NI WIZI ULIOKITHILI
   
 12. p

  pat john JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndivyo serikali inavyowamaliza waTz. Kweli Tanzania shamba la bibi.
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Posho zitaibua mengi!!
   
 14. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani takukuru waliishia wapi na uchunguzi wao wa wabunge kulipwa posho mara mbili? au ilikuwa ni gia ya kuwatishia wabunge ili waache kumtaka mkurugenzi huyo ajiuzulu? Tanzania inabomolewa na watanzania wenyewe, hasa wanasiasa na watumishi wa umma.
   
 15. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Posho ya kujikimu ninavyoifahamu inatolewa kwa mtu anapokuwa nje ya eneo la kazi na inajumuisha chakula na malazi. Ukweli ni kuwa sijawahi kukutana na kiongozi wa nchi kama rais akijinunulia chakula wala akitafuta malazi hotelini. Kama rais naye analipwa posho ya kujikimu anaposafiri kwenda mikoani na hasa Dodoma, hiyo posho ya kujikimu anaitumia kwa kufanya nini?

  Tutakufanya na umaskini wetu na ujinga wetu. nadhani ndiyo kunaanza kukucha, giza linaanza kuisha.
   
 16. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  aisee umeuliza swali matata sana!! sijui kama wataweza kulijibu.. kulingana na utaratibu wa per diem kwa serikalini. mtu aliyepo katika kituo chake cha kazi hatakiwi kulipwa per diem...
   
 17. H

  Heri JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ningeomba na ningefurahi sana kama kuna mtu/watu wenye information ifatayo.
  1. Ni wangapi kati ya hawa wenye nyumba Dar es Salaam na/au Dodoma ambazo zinagharamiwa na serikali ie Waziri , naibu waziri, Katibu wakuu, Naibu Katibu wakuu na wakurugenzi.
  2. Gharama hizo ni zipi? km maji , umeme, ulinzi, wapishi, DSTV, kuweka tv nk.
  3.Gharama za serikali katika session ni ngapi kwenye posho za madereva, posho za wasaidizi na maofisa kutoka wizara mbalimbali, mafuta kwa ajili ya magari yaliyokwenda Dodoma kutaka Dar na sehemu nyigine za Tanzania.
  4. Kuna nyumba za NSSF zilizojengwa hapo Dodoma, je Wabunge hawawezi kuzitumia kwa ajili ya malazi? Pangeweza pakawa estate inayojitegemea kwa kila kitu km Cafeteria, bar , library etc.
   
 18. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ana nyumba ya serikali Dodoma, askari, wafanyakazi wawili wa ndani, dereva na VX la serikali na GX la ubunge, na hapa napo tuulize.

  Zito ameleta matatizo makubwa sana, naona sasa watu mnatoka usingizini.
   
 19. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hivi tuna mawaziri wangapi wenjeji wa Dodoma mjini na je wabunge wangapi ni wabunge wa dodoma mjini ukiacha wale wa Kondoa, Kongwa, Mpwapwa, Bahi na Dodoma vijijini? Umekula lunch mkuu pengine hizo posho unazipigia mahesabu ya wali na maharage ikiwa ndio hivyo basi unakosea Dodoma majimbo yake sio kama majimbo ya Dar es Salaam ambayo unaweza kuzungukia majimbo yote ndani ya masaa kumi na mbili hii ni tofauti na majimbo ya Dodoma.

  My take.

  Kama kitu hukijui bora unyamaze kuliko kuonekana mpumbapumba.
   
 20. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ndio maana mkahimizwa msome ili na nyie muwe na maisha mazuri, anyway hivi unataka waziri mfano sitta asafiri kwenda jimboni kwake kwa gari halafu kazi nyingine kwa mujibu wa diary yake zisimame mpaka arudi kutoka jimboni? anafanya hivyo kwa kuokoa muda anapoenda jimboni anafanya mambo yake anamaliza anarudi ofisini kuwajibika. Jaribu kufikiria kabla ya kupost mkuu.
   
Loading...