Muungano umeathiri zanzibar kukuwa kimaendeleo-Mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano umeathiri zanzibar kukuwa kimaendeleo-Mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 26, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Written by makame silima // 26/06/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]Muungano upo lakini Tanganyika imeshakufa kwa jina la Tanzania.

  [caption id="attachment_31252" align="aligncenter" width="405" caption="Mbunge wa Chwaka Yahya Issa"][​IMG]


  Mbunge wa Chwaka (CCM), Yahya Kassim Issa, amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umechangia kuwarudisha nyuma kimaendeleo Wazanzibari.Yahya alisema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ujao wa fedha wa mwaka 2011/2012.
  “Kisiwe kile mimi nasema Wallaahi, Wallaahi kama si Muungano kisiwa kile siye nasema tungekuwa mbali, miye nakwambieni. Msitudanganye,” alisema Yahya.
  Aliongeza: “Hata nchi hii misaada iliyopata kama tungekuwa tunajitegemea unafikiri tungekuwa wapi? Na nchi zote zinakwenda wapi? Sisi tulikuwa na bendera yetu kimataifa, tuache mambo haya. Hatuwezi kuitupa nchi leo sisi tukasema tumeipoteza. Hatukubali suala hili. Na sisi ndio wa kusema wenye umri huu kwa sababu hamna humu wa kusema.”
  Alisema kitu, ambacho amekibaini ni kwamba, kuna watu hawapendezwi kwa Zanzibar kuitwa nchi kwani vitabu vingi vya serikali, kwenye machapisho yake, sehemu ya mikoa vimeichapisha Zanzibar katika orodha ya mikoa.
  “Mtoto leo kizazi kinachokuja atakujafahamu nini? Lipi analokuja lielewa? Hili ni kosa tunalofanya. Wakubwa kaeni mfahamiane na kwamba Zanzibar kuihesabu kama mkoa sisi hatutaki. Sisi hatutaki,” alisema Yahya.
  Alisema kati ya hoja tisa kuhusu kero za Muungano zilizojadiliwa chini ya uenyekiti wa Ofisi ya Makamu wa Rais, hoja mbili tu ndizo zilizopata maamuzi na kuonya kuwa jambo hilo linaweza kusababisha mgogoro kati ya pande mbili za Muungano.
  Yahya alisema iwapo serikali inataka usalama nchini na Muungano uweze kudumu na kuimarika, basi inapasa iwaelimishe vijana juu ya Muungano.
  Alisema serikali imetoa takwimu za vikao vilivyofanyika kwa lengo la kufahamiana, undugu na urafiki kati ya pande mbili za Muungano kwamba vimefikia 75, lakini imeshindwa kueleza ni vikao vingapi vya kujadili kero za Muungano, ambazo ndizo zinazotesa wananchi, vimekwishafanyika.
  Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, alisema serikali inaogopa kutoa maamuzi ili kuliletea taifa maendeleo, ambayo yanawezekana kupatikana.
  Katika mchango wake, Lowassa alisifia amani iliyopo nchini na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wa nchi, ikiwamo ujenzi wa reli ya Tazara na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) na kusema mambo hayo Watanzania wanajua na dunia pia inajua.
  Alisema mafanikio hayo yanatokana na kazi nzuri iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM na serikali yake kwa kuthubutu, hivyo akashauri juhudi hizo ziendelezwe, kwani iwapo serikali itanuia inaweza.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Tatizo la muungano wetu ni viongozi kuufanya "sacred" na kutojumuisha wananchi katika mustakabali wake. Tatizo lingine ni Wanzibari wengi wameathiriwa na utamaduni wa kiarabu wa kutojibidiisha na kutegemea kufanyiwa kazi. Kwasababu hiyo na ukijumlisha na hadaa za maisha Kama ya Oman kwa Sultani wanatamani kurudi huko walikokua. Swali ni wamatumbi wenzangu watafaidika na uarabu wanoulilia....jinsi Hali ilivyo ufa unazidi kukua na sioni uongozi wa kuuziba.sitasikitika ukivunjika Watanganyika waishi nao kamaWanavyoishi na Wakenya,waburundi,wakomoro n.k
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..kwanini umeme wanaopewa bure na Tanesco hawautumii kufanya shughuli za maendeleo?
   
 4. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbunge kama huyu mwenye mawazo mgando, mawazo ya sisi wazanzibar wao watanganyika, sisi waunguja wao wapemba hatufai, ni mzigo kwa taifa. Badala ya kuzungumzia kipi tufanye kuijenga tz yetu yeye anazungumzia mambo ambayo hata utafiti hajayafanyia,namuomba kipindi hiki kikiisha apumzike asirudi bungeni kwa kuwa mawazo yake ni mgando mno.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu Mbunge anaweza kukumesha huu unyonyaji tena kwa haraka sana. Badala ya kulalamika awazoe wabunge wote wa Zanzibar wapande boti na warudi zao Zanzibar and never to return this way. Na akifika kule aseme Zanzibar is officially an independent nation. Hapo atakuwa ameachana na hii adha ya unyonyaji toka Tanganyaika. Lakini akumbuke akipanda boti 'posho' hakuna!
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wametuchosha. Wangefanya haraka wajiondoe tupumzike kusikia vilio vya kipuuzi.
   
Loading...