Nani alishawahi kuusikia huu wimbo wa Mchaka Mchaka ?
" Kambona , ah, ah!
Kambona, ameolewa!
Wapi?
Uko Ulaya!
Wivu?
Wamkereketa!"
Ulikuwa maarufu sana mashuleni siku za nyuma, sina uhakika kama bado unatumika mpaka leo. Ulikuwa ni wimbo wa kumdhalilisha Kambona baada ya kukimbilia uhamisoni ulaya, U.K kama sijakosea.
MY TAKE:
Wimbo huu ni ishara tosha sana kwamba matatizo makubwa ya nchi hii yamesababisha na Rais wa Kwanza J.K Nyerere. Wimbo huu unadhihirisha wazi jinsi Nyerere alivyokuwa akitumia siasa za maji taka katika nchi changa kama Tanganyika. Kambona alikuwa mtu wa muhimu sana kwenye nchi hii, alijenga chama cha TANU vizuri sana kama katibu, baada ya kuacha kazi ya uwalimu Alliance school, Mazengo baadaye, na hakuwa na kosa lolote kimsingi la kumfanya atukanwe hivyo, zaidi ya kutofautiana kiitikadi, kumwambia mwanaume mwenzio AMEOLEWA, si kitu cha kiungwana, tena kiongozi wa ngazi ya juu aliyekuwa na nia thabiti na nzuri kwa nchi yake. Hata kama J.K Nyere hakutunga yeye, lakini kitendo cha ku uhalalisha wimbo huo hakikuwa cha kiungwana hata kidogo. As a Great Thinker lazima upate mashaka makubwa na busara za mtu huyo. Mbona nyimbo nyingi tu zimepigwa marufuku hapa nchini kwa madai ya kutoendana na maadili yetu, lakini huu uliachwa miaka yote. pamoja na kwamba waliomrithi wamekuwa very INFERIOR na kuendelea kumtukuza, na kuharibu kabisa historia na ukweli wa matatizo ya nchi hii, mimi nasema huyu Kiongozi wetu wa zamani hakuwa mtu mzuri, na ukifatilia historia sahihi ya Uhuru wa nchi yetu, utaona kabisa hakupigania uhuru kivile. alikuja DSM mwaka 1951, uhuru ni 1961. Kwa matatizo haya aliyosababisha, nasema hafai kuitwa baba wa taifa. Sina nia mbaya na yeye lakini huo ni mtazamo wangu. Ifike muda turekebishe historia ya nci hii, kwa manufaa yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.
Naomba kuwakilisha mada.