Kampuni ya BAE mnayoiandikia, wala haina moral authority ya kuwa muamuzi wa kwamba fedha ziende wapi, zitumike vipi. Wao ndio walihusika na wizi huo in the first place. Hata kisa cha Out of Court Settlement, ni sehemu ya kukubali kwao, kushirikiana na baadhi ya watu wetu wasio waaminifu kuwaibia mamilioni ya wananchi wetu walio masikini mijini na vijijini. BAE hawakutuibia watanzania peke yetu, waliwaibia wamarekani pia ndio maana wamewarejeshea pesa zao pia (kwenye serikali ya Marekani, na sio NGO).Kama unafuatilia vizuri suala la BAE utabaini kwamba wenzetu waingereza wameweka UZALENDO MBELE. Kumalizwa kwa shauri lile nje ya mahakama, limezingatia maslahi ya wananchi wa Uingereza, ambao wanapata ajira pale BAE, na ambao wananufaika na huduma za serikali zinazotolewa kutokana na kodi inayolipwa na BAE..... Kwa hiyo, wamekuwa tayari kufunika kombe, MWANAHARAMU apite katika issue hiiii....Wametambua MAKOSA YA WATU WAO WACHACHE (maofisa wasio waaminifu) hayafuti MASLAHI YA WENGi.