JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kuna Taarifa zilizosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii, zinazodai Tarehe 31 Januari 2023 wakati Tundu Lissu akifanya Mahojiano ya channel ya YouTube ya Jambo TV, kwamba alimpongeza Rais Samia kwa kuunda Tume mpya ya Kuchunguza Haki Jinai. Taarifa hizo ni Uzushi. Uzushi huo ulidai kuwa Tundu Antipas Lissu alisifia kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai, hata hivyo, kwa mujibu wa video iliyorekodiwa wakati wa mahojiano hayo Lissu hakupongeza kuundwa kwa tume ya haki jinai wala hakuzungumzia kundwa kwa tume ya haki jinai bali alizungumzia mfumo wa haki jinai kwa kukosoa mfumo huo. Tarehe 31 Januari 2023 Rais Samia alizindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai. Rais Samia alisema Tume hiyo imeundwa kutokana na kuvurugika...
Kipindi cha afya hai ya uzazi wa mwanamke hutawaliwa na mizunguko ya hedhi ya kila mwezi ambayo hukoma baada ya kupata ujauzito, muda mchache baada ya kujifungua na pia baaada ya kufikia umri wa ukomo wa hedhi. Kwa maana rahisi, mwanamke hawezi kupata ujauzito ikiwa hapati hedhi. Hata hivyo, tumesikia mara kadhaa baadhi ya wanawake wakitoa madai kuwa wamepata ujauzito muda mfupi tu baada ya kujifungua, kabla hata hedhi yao ya kwanza haijarudi. Madai haya yana ukweli kiasi gani?
Kumekuwepo na madai kuwa Serikali imesitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo baada ya Kushindwana na mwekezaji. Hapo awali Serikali ilifufua mazungumzo na mwekezaji kuhusu ujenzi wa Bandari hiyo ila mazungumzo hayakwenda sawa. Hayo yamesemwa na Waziri Prof. Makame Mbarawa NB. Kwenye suala na negotiation timu ya mama Samia ipo vizuri sana na ipo kwa maslahi ya watanzania wote.
Asali ni chakula kinachotumika kama dawa ya magonjwa mengi. Hutibu vidonda, kikohozi, huondoa sumu mwilini, ni chanzo bora cha nishati pia hutumika kwa kazi nyingi za urembo. Ukipita mtandaoni utaona baadhi ya makala zikiweka marufuku ya kuwapatia watoto wachanga asali. Jambo hili linaleta ukakasi mkubwa wa jamii kwa kuwa asai imekuwepo kwa miaka mingi, na karibia kila jamii huitumia. Katazo hili lina ukweli gani kisayansi?
Inadaiwa kuwa mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi). Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada. Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya...
Kwa mujibu wa mdau mmoja, Disemba 12, 2019 aliona kwenye taarifa ya habari ya chombo kimoja wakitangaza kuwa familia moja imepoteza watoto wao wanne kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula mihogo yenye sumu. Aidha, mada hii imekuwa inazungumzwa sana mitaani, huku ikiacha mashaka makubwa kwa kuwa mihogo ni chakula kinachotumika kwa kiasi kikubwa, kama kingekuwa na sumu basi watu wengi wangekuwa wamepoteza maisha. Tuelewe nini kuhusu madai haya? Ni kweli kuwa mihogo huwa na sumu, au ni uzushi tu unaopaswa kupuuzwa?
UVUMI Hivi karibuni baada ya Elon Musk kuununua mtandao wa Twitter kuliibuka uvumi kwamba bilionea huyo amepanga kurejesha akaunti zote za Twitter zilizofungiwa, kasoro ile ya aliyekuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021, Donald Trump. Kichwa cha habari cha taarifa hiyo kinasomeka kwa Kiingereza: “Elon Musk States Intention to Restore Every Banned Twitter Account, ‘Except For Donald Trump’, huku ikifuatiwa na maandishi yasomekayo kwa Kiingereza: "It may seem petty but I just don’t like him"- ikimaanisha kuwa ni jambo linaweza kuoneka dogo, ila yeye (Elon Musk) hampendi tu Donald Trump. Picha (screenshot) hiyo inayodaiwa kutoka ukurasa wa gazeti maarufu la Marekani, New York Times, imekuwa ikizunguka kwenye mitandao ya...
Siku chache baada ya kufariki nywele za mtu pamoja na kucha zake huonekana zikiwa zimeongezeka urefu. Jambo hili huonekana mara nyingi sana, linaweza pia kuthibitika kwa kutazama masalia ya binadamu yanayoibuliwa kila kukicha. Baada ya kufariki, sayansi inasema kuwa ukuaji wa kiumbehai kupitia seli hai zake hufikia mwisho, mifumo yote tendaji hukoma na hakuna jambo lolote ambalo huendelea. Kwanini ukuaji wa sehemu hizi unapingana na sayansi?
Back
Top Bottom