JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kwenye hii video Manara anadai kuna Fact ambayo haisemwi kuwa Simba ilianza kuuza jezi na tiketi wiki 5 nyuma. Yanga wametumia wiki 1 tu kuuza tiketi na jezi na zimeisha, huku akisema kuna propaganda ambazo yeye alikuwa anatumia huenda ndio Simba wametumia kuonesha wamemaliza tiketi zao( Sold out) Anesena wana Yanga wajipongeze kwa kumaliza tiketi hizo kihalali. Je, Ni kweli Simba walianza kuuza Tiketi wiki 5 nyuma? Jamiicheck naomba msaada hapa tupate ukweli.
Picha hii inadaiwa kuchukuliwa maeneo ya Ubungo, Dar es Salaam. Inadaiwa kuwa twiga hawa wanasafirishwa kinyume cha utaratibu hivyo mamlaka za Serikali ikiwemo Polisi zifuatilie kwa undani suala hili. Kadhalika picha hiyo imetumika Oktoba 10, 2025 katika mtandao wa Instagram na kuelezwa kuwa "Muongoza watalii huko Zambia amekimbia na Twiga wawili na nyoka mmoja baada ya kuchelewesha kulipwa pesa zake"
Mei 29, 2023 kwenye Mtandao wa Twitter, Mtumiaji mmoja alichapisha andiko linalosomeka kuwa Mwaka 2016 Serikali Ilikataa kumpokea Balozi Mpya wa Zambia Nchini Tanzania Bwana Musenge Mukuma kwa kuwa Jina lake linatoa tafsiri Mbaya Katika Lugha ya Kiswahili. Andiko la aina hii liliwahi pia kuchapishwa Januari 1, 2023 kwenye Mtandao huohuo. Ukweli upoje?
Hello JamiiCheck, Nimeona mtandaoni ukurasa wa Mtandao wa X wa Watetezi TV ukikanusha madai ya kuwahi huchapisha taarifa ya Rais Samia akisema kuna madini kwenye baadhi ya hifadhi zetu na yanapaswa kuanza kuchimbwa kwakuwa Simba na Tembo hawali Madini. Wao wanasema akaunti iliyoposti ni bandia, siyo yao lakini nakumbuka kama niliwahi kuiona mtandaoni siku za nyuma. JamiiCheck fanyieni uhakiki hili suala.
Back
Top Bottom