SI KWELI Picha hii imepigwa kwenye Shule ya Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1724563830584.jpeg.jpg
Hii Picha imezua majadiliano makubwa huko Jukwaa la Siasa, je hapa ni Tanzania na ni lini?
 
Tunachokijua
Picha inayoonesha mazingira duni ya Wanafunzi waliopo darasani, wamekalia matofali (mawe) huku sakafu ikiwa imejaa maji ya mvua.

Picha hizi imetumiwa na katika taarifa mbalimbali kuelezea hali duni za Shule katika nchi nyingi za Kiafrika. JamiiCheck ufuatiliaji wa awali wa JamiiCheck imebaini kuwa zaidi ya kuhusishwa na Tanzania picha hii imewahi husishwa na nchi ya za Afrika. Mathalani, January 31, 2023 mtumiaji wa Mtandao wa X Leksoikris aliitumia picha hii na kuihusisha na Nigeria (link imehifadhiwa hapa).

UPI UHALISIA WA PICHA HII?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck.com kwa kutumia Google Reverse Search umetupa majibu yanayoonesha kuwa picha hii imepigwa kutoka katika shule ya Mangororo iliyopo Kaunti ya Kilifi nchini Kenya na ilipigwa tangu Mei 10, 2019.

Aidha, picha hiyo pia ilihusishwa na darasa nchini Nigeria Kusini, mwaka huo 2019 na madai hayo yalifanyiwa uhakiki na AfricaCheck na Piga Firimbi na kubainika kuwa haikuwa kweli.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa taarifa ya shule hiyo ya The Citizen TV ya Kenya Mei 10, 2019. Taarifa hiyo ilionesha video halisi ya darasa hilo (Video imewekwa hapa). Aidha, taarifa hiyo ilimnukuu Teddy Mwambire ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ganze mwaka 2019 aliyeelezea hali hiyo ambaye alisema:

"Ninajitahidi kwa kiwango changu cha juu kupunguza hali kama hizi katika Jimbo langu, hata kama rasilimali zilizopo haziwezi kutosheleza hatua ya haraka.
"Inapaswa kuwekwa kwenye kumbukumbu sahihi kuwa Jimbo la Ganze bado linahangaika kupata mgao wa miradi yake kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 kutoka NG (Serikali ya Kitaifa) – CDF (Mfuko wa Maendeleo ya Eneo Bunge) kufuatia utambuzi wa kuchanganya kutoka kwa serikali iliyopita. NG – CDF imekuwa ikitutaka tutumie baadhi ya fedha zilizokusudiwa kukamilisha miradi kutoka kumbukumbu zao ambazo hazipo kwenye eneo."
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom