- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Nimeona hii taarifa huko X kuwa polisi wazuia mikutano ya hadhara ya CHADEMA imezuiliwa, je ni kweli?
Nimeona hii taarifa huko X kuwa polisi wazuia mikutano ya hadhara ya CHADEMA imezuiliwa, je ni kweli?
- Tunachokijua
- Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kisiasa nchini Tanzania ambacho kuanzia mwaka 2010 kilikuwa chama kikuu cha upinzani.
Kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa waziri wa fedha katika miaka 1977 hadi 1979.
Kumekuwepo na taarifa za kuzuiwa kwa mkutano wa hadhara ambao ulipangwa kufanywa na CHADEMA Ngorongoro, taarifa hizo zinadai kuwepo kwa barua ambayo polisi wamewajibu CHADEMA baada ya CHADEMA kuindikia polisi kutoa taarifa ya mkutano wao kwa mujibu wa taratibu.
Je, ni kweli Polisi wamezuia Mkutano wa CHADEMA?
Mara baada ya taarifa hizo kusambaa mtandaoni na mdau wa JamiiCheck kutaka kufahamu ukweli wa barua hiyo, JamiiCheck iliwasiliana na CHADEMA kupitia kwa Godbless Lema ambaye alikiri ni kweli CHADEMA wamepokea barua hiyo kutoka polisi inayoeleza kuzuiliwa kwa mkutano waliopanga kufanya kwa madai ya kuimarisha shughuli za kiusalama kwenye maeneo waliyoomba.
Pia, JamiiCheck iliwatafuta Jeshi la Polisi ambao walikiri kuzuia mkutano huo kama ambavyo barua mbayo wamekiri ni yao ya Tarehe 26, 08, 2024 ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngorongoro L. N. Ncheyeki inavyoeleza.