SI KWELI Tundu Lissu afungua akaunti rasmi yenye jina la 'Tundu Lissu 2025' kwa ajili ya Kampeni za Urais

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu, joto la Uchaguzi mkuu limeanza kupamba moto. Tundu Lissu amefungua akaunti rasmi yenye jina la 'Tundu Lissu 2025' kwa ajili ya Kampeni za Urais.

Naona yupo tayari kukabiliana na Samia kwenye uchaguzi mkuu.

SI KWELI (7).jpg
 
Tunachokijua
Agosti 16, 2024, Makamu Mwenyekiti CHADEMA-Bara, Tundu Lissu alitangaza nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2025 kwa tiketi ya CHADEMA ikiwa atapata idhini hiyo.

Kwa mujibu wake, tayari alikuwa ameandika barua rasmi kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ya kuonesha nia yake. Mahojiano hayo yamehifadhiwa hapa.

Awali, Julai 26, 2024 akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam alipowasili akitokea nchini Ubelgiji, Tundu Lissu alizungumza pia hadharani na waandishi wa habari akionesha azma yake hii kubwa na kubainisha kuwa yupo tayari kumkabili Rais Samia kama alivyofanya kwa mtangulizi wake, Hayati John Magufuli kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Tangu Agosti 20, 2024 akaunti ya X ya tangu May 2020 yenye jina la @Lissu2025 imekuwa ikichapisha maudhui ya Tundu Lissu kutaka maoni ya Wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao tazama hapa, hapa, hapa, na hapa.

1724316880659-png.3076181

Picha: Akaunti ya X inayochapisha maudhui kuhusu Lissu na harakati za kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025
Akaunti hiyo imezua hisia tofauti kwa watu mbalimbali huku wengine akiwamo mdau aliyeleta mada hii wakitaka kujiridhisha ikiwa akaunti hii ni Tundu Lissu rasmi au la.

Ukweli kuhusu akaunti hiyo
JamiiCheck.com imefanya pitio la kimtandao kutafuta akaunti rasmi ya Tundu Lissu tumebaini kuwa Akaunti hiyo inayotumia jina la @Lissu2025 yanye wafuasi wasiozidi 300 mpaka kufikia leo Agosti 22, 2023 si akaunti rasmi ya Tundu Lissu (Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA). Akaunti rasmi ya Tundu Lissu katika mtandao wa X inatumia jina la @TunduALissu na ina wafuasi zaidi ya laki 7 mpaka kufikia leo Agosti 22, 2023. Tazama hapa chini:

1724317853457-png.3076201

Picha: Akaunti rasmi ya Tundu Antipas Lissu

Zaidi ya hayo, katika kupata uhakika zaidi JamiiCheck imefanya mawasiliano moja kwa moja na Lissu ambaye amekanusha kuhusika na akaunti hiyo pamoja na jumbe zinazowekwa kwenye akaunti husika. Akiifafanulia JamiiCheck Lissu amesema:

Hii sio ya kwangu, hata kama ujumbe wake hauna tatizo. Mimi ni mtia nia tu; sijawa mgombea bado.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom