- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Je kuna ukweli wowote juu ya hii picha
- Tunachokijua
- Katika kuendelea kuboresha usafiri wa anga ununuzi wa ndege ni moja ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya Tanzania, Machi 13, 2023 Serikali ilitoa tamko la kuendelea kununua ndege nyingine kwa mwaka 2023/2024.
Katika mpango huo siku kadhaa nyuma zilisambaa taarifa za kuwasili kwa ndege mpya ya shirika la ndege ATCLBoeing B787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo mamlaka zilidai itapokelewa Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na Dkt Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Baada ya kutolewa kwa taarifa ya ujio wa ndege, ilijitokea picha mitandaoni ikidaiwa ndiyo ndege ambayo itapokelewa huko Zanzibar Ikiwa imeandikwa Zanzibar Airlines, Tazama hapa na hapa
Je, ukweli ni upi?
JamiiCheck imefuatilia picha hiyo kupitia ufuatiliaji wa kimtandao na kukuta hakuna chanzo cha picha kilicho rasmi na cha kuaminikakilichochapisha pisha hiyo. Pia, ufuatilia wa kimtandao unaonesha picha hiyo imehaririwa na kupachikwa jina hilo la Zanzibar Airlines.
Katika kuendelea kutafuta ukweli, Jamiicheck imewasiliana na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Charles Hilary, ambaye amekanusha kuwepo kwa ndege hiyo.
"Hakuna ukweli wowote. Hiyo ndege ni ya ATCL imewasili juzi na wao wakabandika tu hayo maneno yao kwa lengo la kufuja tu. Hakuna ukweli wowote"
Hata Hivyo ilipofika 20/08/2024, ATCL Walipokea Ndege visiwani Zanzibar ambayo ni ATCLBoeing B787-8 Dreamliner ambayo ilikuwa imeandikwa AIR TANZANIA na siyo Zanzibar Airlines kama ilivyodaiwa.