JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Wakuu, Habari hii imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba huyu Daktari baada ya kumkosoa Rais wa Burkina Faso Kpt. Ibrahim Traore kuhusu kushindwa kupambana na magaidi, alikamatwa, akavishwa magwanda kwenda kupambana na magaidi hao kwakuwa yeye analiweza suala hilo kuliko jeshi. Hii taarifa ni ya kweli au tunapigwa kamba tu?
Ingawa ni kama utani na inachekesha ila huwezi amini kuwa ng'ombe akijamba/kutoa ushuzi basi kile kitokacho huambatana na gesi ya methane ambayo huzalisha joto na moto/mwanga. Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakidiscourage ufugaji/uzalishaji wa ng'ombe kwa wingi na kusema wazi kuwa ushuzi wa ng'ombe huleta mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu ng'ombe hutoa methane, gesi chafu inayohusishwa na ongezeko la joto duniani. Ng'ombe akiwa anajamba, ukiwasha njiti ya kiberiti moto unawaka kutokana na gesi ya methane. Ningependa kujua ukweli wa hili jambo.
Video ya Kushtua ya Wanajeshi imetolewa ikimuonesha Jonas, wa Kamandi Kuu ya Ideal Zimbabwe, anapinga moja kwa moja serikali ya Zimbabwe na Kuomba msaada wa silaha zaidi katika video yake. Jonas Alitangaza Mrengo wake mpya wa Kijeshi mwezi uliopita na watu wengi hawakumchukulia kwa uzito wakati huo, ikijumuisha Gambakwe Media. Mahema na waasi wanaonekana kwa nyuma huku Jonas anazungumza katika kile kinachoonekana kama jumba la kijeshi linalofadhiliwa vyema. Video ya Tinashe Jonas akizungumza mpango wa kumwondoa madarakani Rais Emmerson Mnangagwa
VVU/UKIMWI vinasalia kuwa janga kuu la afya ya Umma duniani, janga lililogunduliwa zaidi ya miaka 40 iliyopita likiwa limechukua uhai wa watu zaidi ya milioni 40.4 huku maambukizi yakiendelea katika nchi zote duniani. Hadi kufukia mwishoni mwa mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa watu milioni 39.0 wanaoishi na VVU, theluthi mbili kati yao (milioni 25.6) wakipatikana barani Afrika. Pia, mwaka 2022 pekee, watu 630 000 walipoteza maisha kutokana na sababu zinazohusiana na VVU na watu milioni 1.3 walipata VVU.
Nadhani wengi tumetizama movie ya Titanic, ikielezea penzi la vijana wawili na pia kuzama kwa meli hiyo. Inasemekana ina uhalisia kiasi fulani na tukio la kweli la kuzama kwa meli hiyo mwaka 1912. Jambo la kutafakarisha, imekuwa ikidaiwa kuwa aliyekuwa kapteni mkuu wa Meli hiyo Edward John Smith kabla ya kung'oa nanga alisikika akisema kuwa ''Hata Mungu Mwenyewe asingeweza kuzamisha hii meli'' - ( "Even God himself couldn't sink this ship") Kauli hiyo inayodaiwa kutamkwa na Kapteni wa TITANIC, imetafsiriwa na wengi kama chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu hivyo kupelekea kuwaadhibu maelfu ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo. Edward John Smith Meli ya Titanic
Hii dunia ina vitu vya ajabu sana na vya kushangaza. Kuna historia baadhi unaweza unaweza kushangazwa nazo mojawapo ikiwa hii niliyopata kusimuliwa. Msitu wa Nyumbanitu una historia nyingi za kushangaza. Msitu huu upo katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe. Msitu huu nimepata kusimuliwa kuwa endapo mwanamke atakuwa kwenye siku zake basi hatoruhusiwa kuingia katika msitu huo, Ikiwa atakaidi basi akiingia kwenye huo msitu ndio utakuwa mwisho wake wa kuonekana maana atapotea mazima. Nadhani hili jambo mnaona linavyostaajibisha. Najiuliza huu msitu una nguvu na miujiza gani mpaka uweze kuwatendea hivyo dada zetu.
Kevin Carter alikuwa ni mpiga picha, sasa katika kazi zake alifanikiwa kufika Sudan na alikuta eneo fulani nchini Sudan likikabiliwa na njaa kali sana. Wakati anaendelea kuchukua matukio katika picha, alikutana na mtoto dhoofu mwenye utapiamlo aliyekuwa akikabiliwa na njaa kali pamoja na kiu, cha kusikitisha zaidi nyuma ya mtoto huyo dhoofu kulikuwa na ndege hatari aina ya TAI akimuwinda huyo mtoto ili kujipatia kitoweo. Inadaiwa Kevin Carter alipiga picha na kusepa. Inasemekana huko nyuma mtoto yule kutokana na kuwa dhoofu aliweza kuuawa kirahisi na TAI yule. Inasemekana picha ile ya Kevin Carter ilipata umaarufu sana mpaka kupata tuzo ya Pulitzer iliyoanzishwa na Joseph Pulitzer. Inadaiwa Kevin Carter umaarufu aliopata...
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kusikia mwanamke mmoja nchini Uganda kajifungua watoto wawili (mapacha) wenye baba tofauti, hali hii ilinishangaza sana. Hali kama hii iliripotiwa pia Septemba 9, 2022 kwenye jarida la CNBC ambapo mwanamama mmoja kutoka Minerois, Brazil alithibitika kuwa na ujauzito wa mapacha ambao baada ya kupimwa DNA zao ilibainika kuwa walikuwa wa baba tofauti. Kisayansi, ni kweli kuwa jambo hili linaweza kutokea? Kama jibu ni ndio, linatokeaje?
Kijana wa miaka 29 aliushangaza ulimwengu kwa kitendo cha kikatili kisichokuwa na chembe ya utu. Inadaiwa baada ya kumpindua na kumuua Rais aliyekuwa madarakani William Tolbert, Samuel Doe alihakikisha anamaliza mizizi ya mtangulizi wake kwa kuua viongozi wote waandamizi. Inadaiwa Aprili 22, 1980 viongozi 13 walifikishwa ufukweni mwa bahari ya Atlantic nchini humo, wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ambapo walifyatuliwa risasi na vikosi vya Rais Samuel Doe. Kati ya waliouawa ni pamoja na Frank E. Tolbert ambaye alikuwa Kaka yake na rais Tolbert, na Rais wa Bunge la seneti. Picha: hali ilivyokuwa siku ya mauaji Muosha huoshwa, Rais Samuel Doe naye alikuja kupinduliwa na kuuawa kikatili sana na waasi.
Salaam ndugu zangu, Nimepata taarifa kwamba Shirikisho la soka nchini Zanzibari limeweka ugumu kwa wachezaji wa Tanzania Bara na itawasajili kama Wageni. Taarifa hii imeandikwa: Bodi inayosimamia Ligi kuu ya Zanzibar (PBZ) imepitisha kanuni mpya za Usajili kuwa Klabu yoyote itakayomsaini mchezaji kutoka Tanzania bara ataingizwa kwenye system kama Mchezaji wa kigeni kwa maana lazima akatiwe Kibali cha kuishi Zanzibar ambacho kina gharimu pesa za kitanzania laki 5. Pia kwenye klabu Moja hawatakiwi kuzidi wachezaji 9 Kwa ligi ngazi ya Mkoa Mchezaji kutoka Tanzania bara atakatiwa kibali cha kuishi na kufanya kazi kwa msimu. Mmoja ambacho kita gharimu Pesa za kitanzania Laki 3. Kwa upande wa Tanzania Bara, mchezaji akisajiliwa kutoka...
Back
Top Bottom