- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Katika pita pita yangu ndani ya maktaba moja kubwa hapa nchini nimekutana na jina la huyu mtoto, Momčilo Gavrić na taarifa kuwa ndiye mtoto au mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuingia vitani mpaka sasa, huku vita ya kwanza ya dunia WWI iliyoanza Julai 28, 1914 na kutamatika mwezi Novemba 11, 1918.
Momčilo Gavrić inasemekana aliingia vitani akiwa na umri wa miaka nane tu na kuanza majukumu ya kupambania taifa la Serbia. Nimekuja huku ili nipate kufahamu je ni kweli kuwa Momčilo Gavrić alipata kujiunga na jeshi akiwa na umri huu wa miaka nane?
- Tunachokijua
- Momčilo Gavrić ni raia wa Serbia, alikuwa mtoto wa nane kati ya watoto kumi na moja, kwa wazazi wake Alimpije Gavrić (baba) na Jelena (mama) mwezi Mei 1906 katika milima ya Gučevo, Serbia. Vita vya Kwanza vya Dunia vilipoanza mwaka 1914, wanajeshi wa Austro-Hungary wa Royal Croatian Home Guard ambao walijulikana kama Devil’s Division walianza kuua maelfu ya raia, wakiwemo familia ya Momčilo Gavrić: baba yake, mama yake, dada zake watatu, kaka zake wanne, na bibi yake waliuawa. Momčilo Gavrić alifariki dunia mwaka 1993
Kuna hoja zinadai kuwa Momčilo Gavrić ameweka rekodi ya kuwa mtoto au mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuingia vitani mpaka sasa huku akihusishwa na Vita ya Kwanza ya Dunia.
UFUATILIAJI WA JAMIICHECK
JamiiCheck.com imefuatilia historia hii kwa kupitia vyanzo mbalimbali ikiwamo kurasa Rasmi za Jeshi la Serbia (link imehifadhiwa hapa). Vyanzo vingine vinavyosimulia historia ya Momčilo Gavrić tulivyovipitia vimehifadhiwa hapa hapa, hapa na hapa) ambavyo vyote vinakiri kuwa historia hiyo ni ya ukweli.
Ukurasa huo wa Jeshi la Serbia na vyanzo vyote vilivyotajwa hapo juu vinaeleza kwa kina historia ya Momčilo Gavrić huku vikimthibitisha Momčilo kuwa askari mdogo zaidi kuwahi kushiriki Vita vya Kwanza vya Dunia wakati akiwa na umri wa Miaka nane tu. Sehemu ya ukurasa wa Jeshi unaeleza:
Momčilo Gavrić alikuwa mtoto mdogo zaidi aliyejiunga na jeshi la Serbia wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia. Alizaliwa mwaka 1906 na alibaki yatima mwaka 1914 baada ya familia yake kuuawa na wanajeshi wa Austria-Hungaria. Akiwa na umri wa miaka nane, alijiunga na jeshi la Serbia kulipiza kisasi, akapewa sare na nafasi ya kupiga mizinga.Alishiriki katika mapigano makubwa kama vile vita vya Kajmakčalan na alivuka Albania na wapiganaji wa Divisheni ya Drina. Baada ya vita, alipelekwa Uingereza kwa masomo. Momčilo ni mpiganaji wa umri mdogo zaidi kuwahi kupewa Nishani ya Ukumbusho wa Albania.