Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe.
Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?
Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?
- Tunachokijua
- HIV ama Human Immunodeficiency Virus ni kirusi kinachoshambulia mfumo wa kinga mwili, ambacho baada kuishi mwilini kwa kipindi fulani kinaweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI).
Virusi hawa wanaweza kumwingia mtu kupitia ushiriki wa tendo la ndoa ambapo majimaji ya uke, uume au shahawa ndiyo hubeba virusi hawa, kushirikiana vitu vyenye ncha kali, kubadilishana damu na mazao yake au maambukizi ya mama na mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua na kunyonyesha.
Virusi hawa wenye sifa ya RNA, hubeba aina 15 za protini pia huzungukwa na kuta mbili za mafuta. Hushambulia seli hai zenye vipokeo vya CD4 pekee, hubadilika mara kwa mara pamoja na kupoteza sifa ya kuishi kikiwa kwenye mazingira yasiyo rafiki.
Ili virusi viweze kuingia mwilini na kusababisha madhara huhitaji mambo matatu ya msingi-
- Damu au Majimaji ya mwili
- Kitendo hatarishi
- Upatikanaji wa moja kwa moja wa mishipa ya damu
Hii ndiyo sababu inayofanya watu wengi wasiambukizwe VVU kupitia salon na siyo kutokuishi kwa virusi kwenye mashine kama hoja ya mdau ilivyo.
Hata hivyo, JamiiForums inatambua kuwa hali hii haitoi maana kuwa salon haziwezi kabisa kuambukiza VVU hasa katika hali ambazo mazingira yote matatu yatakuwepo.
Ni muhimu kwa wamiliki wa salon kutakasa mashine zao kila mara pamoja na kuchukua tahadhari zote za kulinda wateja ikiwemo kutowakwangua sana ili kuepusha uwezekano wa kuichubua mishipa ya damu, kitendo kinachoweza kutoa nafasi ya kuingia kwa virusi mwilini.