Katika jamii ya Kitanzania, baadhi ya mifugo kama vile mbuzi na ng’ombe hufariki wanapokula maganda ya mihogo mibichi. Hali hii huwastaajabisha wafugaji wengi, kwa kuwa mihogo hiyo huwa salama na hata tamu kwa matumizi ya binadamu, lakini inapoliwa na baadhi ya mifugo husababisha madhara makubwa, ikiwemo kifo.
ufuatiliaji ambao umefanywa umebainisha kuwa Mihogo ina kemikali zinazoitwa cyanogenic glycosides (hasa linamarin na lotaustralin). Kemikali hizi zikivunjika ndani ya mwili au wakati mihogo inapokatwa/kupondwa, hutengeneza hydrogen cyanide (HCN) ambayo ni sumu kali ndani ya mwili wa mnyama
Utafiti ambao umefanywa Tweyongyere,R. & Katongole (2002)umeeleza kuwa sehemu ya nje ya muhogo mara nyingi ina kiwango kikubwa cha cyanide...