- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
SINEMA INAENDELEA : Mwanaharakati Maria Sarungi, Hilda Newtown na Twaha, walivyokutwa kwenye kikao cha siri huko Nairobi cha kutengeneza sinema ya kupotea kwa kijana msaidizi wa Tundu Lissu ambaye hafahamiki hata na familia ya Tundu Lissu.
CHADEMA wala waje na kitu kingine ila hili la kujiteka, ni sinema kama sinema nyingine na Watanzania washazishtukia.
CHADEMA wala waje na kitu kingine ila hili la kujiteka, ni sinema kama sinema nyingine na Watanzania washazishtukia.
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwapo na picha inayosambaa ikidaiwa kuwa ni ya wanaharakati pamoja na wanachama wa CHADEMA, Maria Sarungi, Hilda Newton na Twaha Mwaipaya.
Taarifa hiyo ilidai pia kuwa msaidizi wa Tundu Lissu aliyetekwa David Djumbe ni miongoni mwa wanaoonekana katika picha hiyo, na kwamba taarifa zake za kutekwa zinapotosha.
Uhalisia wa picha hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa picha hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde. Picha inayoonekana ina mapungufu badhi ikiwemo sura zinazoonekana hazirandani na sura za waliotajwa yaani Djumbe, Sarungi, Twaha na Hilda.
Hata hivyo uchunguzi kwa njia za kidigitali umebaini kuwa picha hiyo ina viasharia vya kuundwa kwa AI kwa takribani 99%.
Uhalisia wa kutekwa kwa msaidizi wa Lissu, David Djumbe
David Djumbe kwa mujibu wa Taarifa ya polisi na yeye mwenyewe (Djumbe) alichukuliwa na watu wenye silaha alipokuwa akirejea kwake maeneo ya Mbweni kabla ya kufanikiwa kuwatoroka na kurejea nyumbani kwake akiwa na pingu.
Hitimisho
Picha hiyo si halisi lakini pia David Djumbe alitekwa kweli na hakuwepo Nairobi kama inavyoelezwa.