Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Zitto, mimi huko pia Urais nautaka na kama ni UWEZO TUNAO haya twende basi tukaupate huo urais ukiwa wa moto moto bada.

Pengine Urais wa Tanzania upo on Sale lakini wengine hamna taarifa. Mzee Mtikila kwani wewe urais hautaki, je mzee mapesa, na wewe hapoPasco vipi twendeni tukajipakulia urais wa JMT.

Masou wa Kipanya, urais ndio huu hapa twenzetuni basi maadam kuna vijisenti mfukoni mengi MAFISADI watatuongezea huko mbele ya safari ili tukawalinde kwa kusema mwacheni akina Ndugu X na Y wakapumzike basi kwisha mchezo.
 
Mkuu,

Umeamua kuingia kwenye personal vendatta baada ya kubanwa kwenye hoja.Ndiyo sikatai kwamba kufungua matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi niligomea na nililisema wazi mbele ya Balozi.tukiwa nje ya Tanzania sisi huwa tunajulikana kama watanzania na si wanachadema wala wana-CCM.Tunatakiwa tuungane tuwe kitu kimoja kwani tulikuwa wachache.Wenzetu wanigeria walikuwa wengi na hawakuwahi kufanya jambo la kijinga kama lile.

Balozi mzima aliyosomea protocal anasimamia zoezi la kuwagawa watanzania?ulitaka nimchekee?

Tangu lini hapa Tanzania tukaona wamarekani wamenzisha matawi ya Republican na democrats hapa Tanzania kwa kuzingatia utashi wa vyama vyao?huku si ndiko tulikoiga demokrasia ya mfumo wa vyama vingi?ni kwa nini sasa tuingie kwenye siasa kizuzu hadi tutie fedheha ugenini? Kwangu mimi ni Tanzania kwanza mengine baadae na siwezi kumuogopa Balozi,waziri au mwanasiasa yoyote
Mkuu Ben,
Kungekuwa na Thanks ningekugongea kabisa katika hilo,
Watanzania wa ughaibuni wanaotarajiwa kuleta chachu ya maendeleo nyumbani wakishagawanywa kwa maana ya vyama vya siasa wamekwisha, hayo ndo yanayotumaliza sana! Badala ya watu kuunganishwa na utanzania wao wanagawanywa kwa vyama vya siasa.
 
I mean tufike mahali tutenganishe National interest na personal interest, Zitto ni symbol tu ya Vijana wengi wenye uwezo ambao wanaona wakati ni huu, sasa it should be a National debate kwa kuangalia the history je toka vijana waanze kushika power kwenye vyama mpaka taifa, kuna anything good kwa taifa as opposed na kabla hawajashika?
Ha ha ha!"The Vijana Revolution"?
 
Hakika haijapata kutokea kwenye harambee ya CDM jana kule Naura Spring Arusha.Na umri wangu nilio nao sijawahi shuhudia kilichofanywa na CDM jana.Halafu wanatokea Manyang'au wanawabeza majabali Mbowe na Slaa.Narudia kusema kwamba namuomba Mungu wangu anipe maisha marefu nimshuhudie Dr Slaa akiapishwa kuwa Rais mwaka 2015.Baada ya hapo Roho yangu inaweza kwenda kwa amani.
Zilipatikana shilingi ngapi mkuu??...
 
Nimepitia hii mada ya Zitto na hakika inahitaji mjadala mpana sana.

Binafsi sidhani kama kuna haja yoyote kwa sasa kufanya wagombea urais kuanzia miaka 35. Hii ni hoja changa sana tena ya kitoto. Ni hoja iliyopikwa kwa sababu maalum na kwa malengo maalum. Tunajua mwasisi wa hoja hii ni Rais Kikwete pale alipowaeleza siri hiyo kina Zitto na Kafulila kule Kigoma. Na baada ya pale ndipo Zitto akalibebea bango.

Niwe mkweli kwamba CDM wafanye kazi ya kuimarisha chama chao waachane na porojo za urais. Ni upuuzi badala ya kuimarisha chama watu wanaanza kujipigia kampeni za kugombea urais. CDM nadhani wana mgombea bora kabisa wa Urais ambaye bado ni kipenzi cha watu Dr Slaa. CDM wanapaswa kumsaidia Dr Slaa ili aje awe Rais bora.

Kinachomnyima Zitto credit kugombea kupitia CDM ni sababu moja tu kwamba anapigiwa debe la nguvu na wale maadui wote wa CDM. Wajanja wanajiuliza Kulikoni? Adui yako akikusifia ujue there is something wrong!
Mkuu ikiwa tutajadili suala la taasisi ya urais kuona kama kuna umuhimu wa kupunguza umri au la outside Zitto na wengine wengi mimi ni miongoni mwa watu wanaounga mkono suala la kupunguza umri kabisa tena ikiwezekana mtu mwenye umri wa miaka 30 kama anafikia sifa zingine za Kikatiba basi aruhusiwe kugombea urais.

Ikiwa tunasema life spam yetu sasa ni 47 why kugombea urais wa nchi iwe 40?? A young person can be a great president of the country.

Point yangu hapa hatuwezi kujadili taasisi ya urais kwa kuwa tu Zitto au January wanataka kugombea bali tujadili kwa kuwa tu vijana wana uwezo wa uongozi.
 
Rufji said:
Kuchangia kuhusu Zitto na mwenzake January kugombea urais 2015 ni kupoteza muda kwani katiba haitawaruhusu kufanya hivyo kutokana na umri wao. Kinachotakiwa kufanyika ni kubadili katiba kwanza, kitu ambacho itakuwa ni vigumu kufanyika. Hawa vijana inawezekana wana dhamira lakini bado hawajajua jinsi ya kufanikisha malengo yao ya kisiasa. Ili waweze kubadili umri wa kugombea ni lazima wapitie bungeni, ambapo majority ya wabunge wana umri zaidi ya miaka 40.
January atakuwa na miaka 41, hata hivyo amesema hautaki uraisi. Hivi mkuu, kwani si ni hivi punde tutaanza kuandika katiba mpya? Katiba hawaandiki wabunge.
 
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com

Binafsi sihitaji ujibu chochote juu ya makala ya mwanazuoni.unadhani kwa umjibu utawabadili imani wale wengi waliamini hivyo?sasa hivi mimi sioni hata tofauti ya CCM na CDM zaidi ya majina.
mimi ninakushauri ukaendelee na kazi ya kutekeleza ahadi ulizotoa kwa wananchi wa jimboni kwako unless useme umeshatimiza zote halafu muda ukifika wa kugombea ndipo uchukue fomu ili tukupime kwa ulichofanya kwani kwa sasa wananchi tunakabiliwa na matatizo mengi na hili la urais halina tija kwa sasa.
 
WANAOPINGA KUONDOLEWA KWA KIKWAZO CHA UMRI WA URAIS WATOE HOJA



Sabatho Nyamsenda

Labda nitaje mapema kabisa kuwa mimi naupinga mjadala huu kwa lengo na namna unavyoendeshwa, aina ya watu wanaoushadadia, na baadhi ya hoja zinazotolewa. Lakini sipingi kuondolewa kwa vikwazo vya watu kugombea nafasi za kisiasa vikiwemo vigezo vya vyama na umri.

Mimi si shabiki wa nadharia za kibwanyenye. Lakini wananadharia wa kiliberali wanasema kuwa binadamu kwa asili yake amezaliwa na uhuru kamili ambao haupaswi kuingiliwa na mtu ama taasisi yoyote. Binadamu anapaswa kuwa mwamuzi wa maisha yake mwenyewe na kuzitumia fursa alizo nazo pasi na kuingiliwa. Mtu anayenyimwa uhuru ama fursa, haijalishi kama anaitumia ama la, anashurutishwa na kuonewa [‘she or he is being coerced']. Hivyo, yule anayemnyang'anya mtu uhuru na fursa alizonazo anapaswa kujitetea na kuthibitisha uhalali wa kufanya hivyo.

Katika nchi yetu, tulikuwa na kiongozi mahiri na shupavu, lakini ambaye mara nyingi aliziminya fursa na uhuru wa watu kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kujenga umoja wa kitaifa na hata kujiimarishia mamlaka ya kuwa Rais mfalme. Mtu huyo ni Mwalimu Nyerere. Na kila mara alipowanyang'anya watu uhuru wao alijenga hoja juu ya kwa nini amefanya hivyo. Alifuta vyama huru vya wafanyakazi, akafuta vyama vya upinzani, akafuta ushirika, akawanyima watu fursa za kutajirika na kuwanyonya wenzao, akaminya uhuru na fursa za kuiba fedha za umma na kula rushwa, n.k. Lakini alijenga hoja ambazo waliozipinga waliishia tu kusema, "Ah! Hana lolote huyo, anataka tu kujiongezea madaraka." Na baadae alikiri kuwa baadhi ya vitu alivyofanya vilikuwa na makosa ikiwemo kufuta ushirika.

Historia ya dunia inatufundisha kuwa binadamu amenyimwa uhuru kwa namna mbalimbali. Kuna wakati wanawake hawakutambulika kama binadamu. Hata walipotambulika hawakupewa fursa za kupiga kura, achilia mbali kugombea na kumiliki mali. Lakini baada ya ‘mapambano' sasa dunia inakiri kuwa wanawake ni binadamu na wanapaswa kuamua hatma zao kwa namna mbalimbali ikiwemo kupiga kura na kugombea. Watu weusi vivyo hivyo. Lakini sasa dunia inatambua [hata kama ni kwa unafiki] kuwa nao ni binadamu. Masikini vivyo hivyo, lakini sasa japo wanaruhusiwa kupiga kura na kugombea, haijalishi kama wana uwezo wa kushinda.

Hoja niijengayo hapa ni kwamba waliowanyang'anya – na wanaotetea – Watanzania wenye chini ya miaka 40 fursa ya kugombea urais sharti wajenge hoja zenye mantiki na zenye kushawishi. Kwa nini ni 40 na si 39 ama 25? Ni katiba gani inayotaja umri wa kuanzia lakini haiweki kikomo? Kuna vigezo gani vya kisayansi, kihistoria ama kimantiki vinavyoweza kuthibitisha kuwa mtu mwenye miaka 40 atafaa zaidi kuwa Rais kuliko mwenye 37 au 29?

Ukizipitia kwa umakini hoja za wapingao umri kupunguzwa utagundua namna zilivyojaa chembechembe za uhafidhina. Kwanza wapo wasemao chini ya miaka 40, mtu anakuwa bado ni mchanga, kijana, n.k. Lakini hawatuambii kama mtu akifikisha 40 ndio anakuwa amekua na kukomaa. Wala hawaikemei Katiba kutoweka kikomo, kiasi kwamba hata ‘kikongwe' mwenye miaka 120 ana haki ya kugombea urais, lakini si ‘kichanga' mwenye miaka 39.

Wapo wanaotumia jina la Mwalimu kuthibitisha ‘uharamu' wa hoja zao. Kuna mtu alitolea mfano wa mwaka 1995, Mwalimu alipomwambia mmoja wa wagombea wa urais kupitia CCM, kuwa, ‘Wewe bado ni mdogo. Subiri kwanza ukue'. Lakini mtu huyo [tumwite ‘Bwana Mdogo'] alikuwa na miaka 45 wakati huo. Mwalimu mwenyewe hakuzuiliwa kugombea urais wa TAA na baadae TANU na kuongoza harakati za ukombozi licha ya udogo wake kiumri. Nijuavyo mimi, sina hakika kama Mwalimu angebadili mawazo yake, iwapo angekuwa hai, mwaka 2005 pale ‘Bwana Mdogo' alipojitokeza tena, akiwa na uzoefu mkubwa zaidi na umri wa miaka 55. Angalau karibu nizungumzaye nae ananiambia udogo na uchanga wa ‘Bwana Mdogo' huyo si wa umri, ni wa uwezo.

 
nimekuwa nikifuatilia kwa kina kunani kati ya zitto zuberi Kabwe na Dr. Slaa hapa pamenistua, nimepitia tamko la zitto juu ya urais kwa vijana, amerudia historia yoote ya chadema lakini anamtaja Freeman Mbowe kama mtu aliye shiriki nae kujenga chama na si Slaa, katika macho ya zitto k. slaa hana lolote ndani ya chadema, lakini kuna watu tunaujua weledi wa slaa, anasema walikubaliana na mbowe 2005 agombee urais lengo likiwa kujenga chama. na 2010 haiongelei kabisa ambayo slaa alivuta kura nyingi, je zitto amekuwa na mtazamo gani kwa slaa? kwani mara chache anamrecognise, naye slaa anafanya nini ndani ya chadema, coz ni kama antumiwa tu?

pia zitto ana mwongelea mdee tuuu, na mnyika tuuuu. what about vijana watz wasio kati ya hao? je ni kweli alishiriki kuvuruga uchaguzi 2010 kwa mawasiliano yake na wakubwa wa TISS? je chadema ya wapenda pesa kama mbowe, zitto na wengine wataweza kweli kusimamia maslahi ya nchi yetu mbele ya wageni? alijichanganya alipoingia tume ya madini, je amejichomoa huko? usafi aliopoteza mbele yetu vijana tulio makini ana hakika gani kama tumemuelewa tofauti? ajitoze katika midhara ya wazi ya vijana walio makini na ayajibu haya basi?
mustakabali wa chadema uko mashakani
 
  • Thanks
Reactions: DSN
It is too early CHADEMA,we're going to hurt our party. let us continue concentrating on building the bases ( Voters awareness and civil education) . Let us not be diverted by CCM's tactics on lobbying few CHADEMA's promonent members, this guy being the ones.
Let us leave this awkward business to CCM and we'll ultize their party division ( groups ) to win the expected general election 2015 believe in me or not.
 
Ndio tatizo lenu watu wa kaskazini mnalazimisha Slaa 2015 agombee urais ili hali atakuwa mzee na hatufai tena. Na isitoshe mzee hana jipya kwa sasa, awaachie vijana wakina Zitto. Kuhusu umri katiba ijayo tunalirekebisha hilo na Zitto ambae ni chaguo la CDM wengi ata qualify.

Mambo haya kawambie magamba wenzio. Ni ushauri unaowafaa maana nasikia hata January naye alishatangaza nia.
 
Na wewe bana..acha uoga wa kijinga na kutishwa na so called usalama..wazungu wanakupenda wewe? mbona hujiulizi hilo swali kabla ya kumtwisha Ben mzigo huo?

Wewe inakuhusu nini au wewe ni hawara ya ben.ninyi wadada mnapenda vibaya mno.

bahati nzuri Jf kuna rekodi bwana.chuki zake dhidi ya wazungu zinadhihirika angalia alivyokuwa anajibizana na waberoya hapa

quote_icon.png
By Waberoya
Mkuu nimekupatanimekuelewa

1. Nataka Slaa awe kama Morgan anayeonekanamachoni pa watu! na siyo Morgan aliyejificha, definitely I would not haveadvised Slaa to be like the Morgan Traitor.....

2. Umenichekesha kuona kuwa unawachukia wazungu kiasi hicho.....ila kwademokrasia wako mbali sanaingawa walitutawala na wanaendelea kututawala. Ila in real sense SITAKUJAKUWALAUMU wazungu kuja kututawala!!! maana hata sisi tungekuwa wazungutungewatawala wao, IT IS NATURAL. Ni kama swala anagoma asiliwe na simba wakati yumo mbugani This wasunavoidable....zile effects za UKOLONI WA KUZIONDOA NI SISI WENYEWE....kamaenzi hizo machifu waliuza ardhi...na miaka 60 baadae bado tunauza ardhi kwa haohao wazungu, what does that mean??

3. We are the one who make ourselves inferior, nchi za ASIAhazikutawaliwa?? what made them to compete with Europein almost everything? tell me...Tangu tumepata uhuru hatujajua athari za ukoloni?

1. Nani anapaswa abadilishe mitaala ya shule?
2. Go to judiciary system is totally british
3. Go to our bunge session and style..is totally British
4. Who encourages modernisation of western?? we are

British or Americans have nothing to do with our stupidity.....they did that because of survival of fittest…..todate we can not compete with them in almosteverything, why are we blaming them??

Does whites force you to spend time in Facebook, to watch CSI and 24 series??does whites forcing you to live and die with Premier league??

Tell me, what is that we are doing that whites are forcing us to do?? Wait a minute..does whites force us to beg them, to ask for aids..because we can not feed ourselves!!!! Just imagine the way we are multiplying and we can not even get our needs…yet this is muzungu's faults??

You know what Mr. Ben I can feel your anger and hatred towards these people but wont help!

WE MISSED LEADERS who knows our background, who can actually preserve our culture and history, we missed people who can actually let AFRICAN be african, like chinese, japanese etc.

We are the ones to be blamed we did not counter attacked the situation...we failed, we are failing and we may never recover ...AFRICANS IS NO MORE... with globalisation and science and technology AFRICA has collapsed

we were not ready for free market or globalisation, we are not READY even now!!!

WHAT SHOULD BE DONE IS TO CLOSE BOUNDARIES.......NEVER CONTACT WITH OTHER COUNTRIES..let dig, produce and eat what we have THAT IS THE ONLY SOLUTION APART FROM THAT WE WILL CONTINUE HATING WHITES FOR NO CAUSE...huwezi ukaona unakufa,chakula kiko africa ukae tu..kwa kuwa ukienda utaonekana m'baya




South africans are stronger today because once their boundaries was closed due to apartheid , they survived inspite of all difficulties of being excommunicated from other worlds

Ben......Slaa and you has to rise up...NO EXCUSE if we need to survive we need to learn from who survived....the problem is that we have not reached the industrial revolution...we have not even reached the 19th century...we are somewhere that our history will mock at us...WE ARE IN THE AGES WHERE OUR COUNTRY IS ACTUALLY A DUSTBIN...OF EVERY TECHNOLOGY AND LIFE STYLE FROM EUROPE ..oh! my God we can not blame white..Can we??


Ben alijibu hivi hapa chini

Sure,We can't blame whites!

Mkuu Wabe,tupo on the same page kwa yote uliyosema but my point ilikuwa juu ya kuvunja minyororo ya utumwa.Hayo uliyoandika ndiyo ambayo tunataka sasa tuyatekeleze kwa hiyo kama Slaa atafanana na Morgan Tsavangiraia tutaendekeza ukoloni,tutakuwa tunabadilisha regime tu na kuwasaidia zaidi mabeberu.Tutakuwa tunatekelezana kuisadia foreign policy of the United States(Regime change policy)

Siwachukii wazungu,hata shetani mwenyewe na ufedhuli wake simchukii bali matendo yao.Sasa kama nachukia matendo ya kibeberu na ofcourse wanasaidiwa na incompetent leaders kutoka nchi zetu,je sina haki ya kuwachukia vibaraka wanaotaka kutufanya tuzidi kutawaliwa kifikra?

Vijana sasa hivi hawafanyi kazi zaidi ya ku-bow down mbele ya cultural imperialism.Ligi kuu za Ulaya ndiyo siasa kwao,ndiyo kazi ndiyo entertainment n.k. Ofcourse hili taifa linahitaji uponyaji na uponyaji huu unahitaji inspiration kutoka kwa leaders wanaojua tunahitaji nini,historia yetu ikoje na tunataka kwenda wapi.mfumo wa uongozi tangu tupate uhuru umekuwa wa kuendekeza ukoloni mambo leo kifikra,hapa ndipo ninapotaka sasa tufanye radical change(hapa nafurahi kuona hii spirit sasa imeanza kuingia damuni mwa baadhi ya viongozi ndani ya chama,signature yangu ya JF ilikuwa inasema Movement For Radical change na jana kwenye fundraising ya Arusha theme ilikuwa Movement for Change,M4C).

Sure,we need to rise up,we need to inspire a radical departure from mental slavery.Taifa linahitaji healing lakini si kuendekeza ukibaraka.Thanks kwa ku-admit kwamba Moragan the Traitor hawezi kuwa role model au figure ya kufanyia reference kwenye transformation tunayoitamani

Come on Wabe! Facebook is a social network.Tunakataa ubeberu lakini technology inayoletwa na mabeberu hatuwezi kuikataa pengine tukiweza kubadili fikra za watu wetu tutaweza kuitumia vizuri na kuigeuza against their ambitions.Facebook ndiyo ilitumika kuleta radical change kule Egypt na kumuondoa kibaraka wa Mabeberu dikteta Hosni Mubaraka.Facebook ilikuwa tool muhimu iliyotumika na vijana wa Tunisia na Misri kuwatia matumbo joto mabeberu kwa kujua hii revolution inaweka Camp David Accord at stake

Kutokana na fedheha iliyowakumba wakaamua kuleta balance katika ile region kwa kutumia force Libya na sasa Syria.The U.S./NATO bombing of Libya has clarified where imperialism stands regarding that country. The transnational exploiters are determined to totally seize hold of the richest oil reserves in Africa and cut off the billions of dollars that Libya was contributing toward the development of much poorer African countries.

Syria is also targeted by imperialism -- because of its heroic defense of Palestinian resistance over decades and its refusal to recognize the Zionist occupation. Syria's assistance to Hezbollah in their struggle to end the Israeli occupation of Lebanon and their strategic alliance with Iran cannot be forgotten

Comrade Waberoya,sasa hivi mabeberu wanatumia nguvu na technolojia yao + unpatriotic spirit ya viongozi wetu both kwenye ruling side na opposition(prospective government/regime) kuhakikisha maslahi yao hayathiriki.Ningekuwa na uwezo wa kuja hidden agenda za viongozi hawa na tulio nao hapa Tanzania nisingeona aibu ku-champion assasination kwa Traitor hawa kama ningeshindwa kuwabadili kifikra ili waweze ku-fit katika vision kwa maslahi mapana ya watanzania na Afrika kwa ujumla.

Wabe, mababu zetu waliokuwa wanamapinduzi wa kweli walijitoa sadaka kwa kushirikiana na intellectuals na kweli waliwashikisha adabu wakoloni wale. Comrade Osagyefo(Kwame Nkrumah) spent time in England and discovered its weak economy following World War II, then planned a political strategy with an economic offensive of boycotts, strikes, and demonstrations, "positive action," to cripple England and win independence for Ghana on 6th March 1957. Today America's economy is weak and in the spirit of Osagyefo Kwame Nkrumah, we are calling on Africans youths and true leadrs to demonstrate, strike, and boycott, and other oggresive measure according to the current situation in solidarity with resistance, to win total independence for Africa. Ni lazima tuanze na viongozi wetu both in the ruling party na hata upinzani incase kuwae na dalili za ukibaraka

Kama tunashindwa hivi kwa kisingizio cha demokrasia ya magharibi basi tuifanyie modification otherwise Africa itashuhudia rebellion against our puppet leaders.Viongozi walioko madarakani Tanzania na Afrika na hata vyama vya upinzani washuhudie maasi,wale comrades wanaoelewa hili tutaungana mkono.Waberoya najua wewe ni mmojawapo

Asia haikufikia hapa ilipo kwa sababu viongozi wao wao wa kwanza waliweka misingi ya kukataa ubeberu.Mahatma Gandhi na Shri.Jawahlal Nehru heroically waliongoza India kukataa ubeberu na ndiyo maana ukisoma foreign policy ya India (Diplomatic relation kati ya India vs United states ilikuwa zig zag untill 2000's). India leo huwezi kufanya investment ukamiliki stake kwenye company more than 49% kama foreigner.India wana policy,wanajitahidi ku-preseve culture yao ambayo inawa-define na inafiti katika ambition na interest zao kama Taifa.Halikadhalika China

China,Comrade Mao Tse Tung aliindoa China kwenye janga la kuwa victim wa ubeberu.Wale traitors aliowapindua walikimbilia Taiwan (alifanya kosa kuwaacha hai Hadi leo US anaitumia Taiwan kuelekeza detterence millitary kwa china).Chairman Mao Tse tung alipoanza na the great Leap,alinyonga watu wengi (Ofcourse Traitors deserves nothing but DEATH) lakini China Imesimama na inaweza kuvunja rekodi ya Soviet kuwa super power ndani ya kipindi cha miaka 70.Ooops,nisije nikatoka nje ya mada sana sasa....!

Kazi iliyoko mbele yetu ni tete kama tunataka kuliponyesha Taifa hili.

Kwa kuanzia tu kama wanasiasa,kama intellectuals tunaweza kuanza na utekelezaji wa maudhui ya hapa kwenye signature yangu

Personal vendetta??????????................
 
Mda huu watu na chama tupo tukihakikisha ukombozi arumeru then we zitto unaendesha siasa zako humu, nakuheshimu sana zitto but kwa maujinga ambayo huwa unayafanya na unayoyafanya yanazidi kupunguza iman yako kwa chama na watu, badala ya kuendeleza harakati kwanza jinsi ya kukomboa arumeru ambapo masikio na macho ya watu yapo huko, we unaanza ujinga wako humu mitandaoni, najua hii ni haki yako kidemokrasia but unaimisuse vibaya sana.

Jiulize hivi ni kwanini pro-ccm wanakusuport sana kwa hoja zako za urais na kumpinga slaa? Je ni kwanini slaa hawampendi wale wote mafisadi na pro ccm?

Ni ukweli dhahiri kwamba dr. Slaa bado anafaa na hakuna haja ya mtu kuendesha propaganda za urais kwa huu mda kwani ujue unavyofanya hivyo unachochoea mgawanyiko chamani.

David kafulia aliwahi kusema hivi " uongozi bila demokrasia ni udikteta lakini demokrasia bila nidhamu ni fujo"

TAKE CARE ZITTO.
 
sioni ubaya wowote wa Zitto, ni mtendaji mzuri haswa, mwenye nia ya dhati ya mabadiliko, siyo mchumia tumbo, kama kigenzo cha umri hakitamkwamisha na akapita kwenye chama chake, na kama mataifa ya magharibi hayataingilia uchaguzi wetu, sioni pingamizi lolote la Zitto kutokuwa rais wetu,kizuri kinajiuza kwa kweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom