Mkuu ikiwa tutajadili suala la taasisi ya urais kuona kama kuna umuhimu wa kupunguza umri au la outside Zitto na wengine wengi mimi ni miongoni mwa watu wanaounga mkono suala la kupunguza umri kabisa tena ikiwezekana mtu mwenye umri wa miaka 30 kama anafikia sifa zingine za Kikatiba basi aruhusiwe kugombea urais. Ikiwa tunasema life spam yetu sasa ni 47 why kugombea urais wa nchi iwe 40?? A young person can be a great president of the country. Point yangu hapa hatuwezi kujadili taasisi ya urais kwa kuwa tu Zitto au January wanataka kugombea bali tujadili kwa kuwa tu vijana wana uwezo wa uongozi.
@Hassan J. Mosoka, sina tatizo na umri wa rais, anaweza kuwa miaka 18, 20, 35, 50 na hata 80 na kuendelea PROVIDED tuna mfumo mzuri wa kiuongozi. Kwa miaka 50 tangu Tanzania ipate uhuru, tumekuwa chini ya urais (presidency) wa kifalme. Rais amekuwa na mamlaka makubwa sana na yuko almost every where kwenye chain ya utawala. Na rais anaonekana kuwa juu ya sheria. Rais anateuwa mpaka mkurenzi mkuu wa gazeti na hakuna wa kumhoji! Awe ni mtu mwenye uwezo au la hakuna wa kumzuia. Huu ndio utaratibu tuliokuwa nao kwa miaka yote 50.
Yote hiyo inaweza isiwe tatizo lakini shida inakuja pale inapotokea mtu anayekalia hicho kiti cha urais (urais wa kifalme) akawa ni dhaifu. Hapa ndipo nchi inaweza kwenda mrama. Wananchi wanabaki kuwa kama mateka, wanajikuta hawana nguvu hata kidogo ya kurekebisha mambo kwa sababu mfumo hautoi nafasi.
Sasa hivi tuko kwenye mchakato wa kupata katiba mpya, hatuna uhakika itakuwaje maana politics inaweza kuingiza vitu tusivyotaka (tuombe mungu isiwe hivyo). Na kwa hakika rais ajae atakuwa na challenge kubwa sana maana ataanza uongozi chini ya katiba mpya, lakini kama taifa bado tutakuwa kwenye 'transition period' kutoka kwenye urais wa kifalme kwenda kwenye urais ulio na ukomo kimamlaka (tafsiri yangu).
Je, ni mtu wa aina gani anayeweza kubeba mzigo huu mzito wa kuongoza nchi toka kwenye urais wa kifalme kwenye kwenye urais wa ukomo kimamlaka? Jibu la haraka haraka ni mtu mwenye uelewa, nia dhamira uzoefu/tested (nasisitiza) na anayeweza kufanya maamuzi magumu, kwa kifupi aliyekomaa. Na je, mtu aliyekomaa anakuwa na umri gani? 18? 20? 35? 60? 80? 120? Hapa ndipo kuna kasheshe.
Jambo jingine muhimu sana watanzania wote tunatakiwa tukumbuke ni kwamba tuko kwenye wakati wa majiribio makubwa, nchi hii ina madini mengi sana, diamond, gold, tanzanite, URANIUM. Na sasa tuna gas. Ukishakuwa na hivi vitu viwili URANIUM na GAS inabidi uwe tayari kwa michezo ya kuigiza toka kwa big boys wa nchi za magharibi. Sasa hivi tunaona jinsi gani Marekani iko kila mahali, kuanzia malaria no more hadi Symbion. Wakati huo huo Urusi kila kukicha kuna 'special messanger' toka kwa rais wao anakuja kuleta ujumbe. Haujakaa vizuri China wanatuandalia Chinese New Year. Ukigeuka kule France inakuambia 'nakufutia madeni! (unafuta madeni wakati credit rating yako imekuwa down-graded?). Unafuta madeni halafu inakuwaje? Kila mtu anaenda nyumbani and live happily ever after?
Ninasema yote haya ili kama taifa tujue challenge tuliyonayo katika kusuka mfumo wa uongozi kuanzia rais hadi serikali za mitaa. Kama ni kushudha umri wa urais basi tuwe na hakika tuna vijana wa Tanzania wanaoweza kumkatalia special envoy wa rais wa nchi yeyote kuhusu rasimali za nchi hii. Tuwe na hakika kwamba tuna vijana 'tested' wanaoweza kuhimili mikikiki ya kununiliana suti. Lakini kubwa tushushe umri wa urais tukiwa na hakika tuna 'system' ambayo itainusuru nchi pale udhaifu wa kiongozi huyo utakapotekea. Tusijaribishe kwenye hili. 50 yrs is enough. tuwe na uhakika na tunalofanya.