Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Basi akagombee chama kingine lakini sio chadema. Lazima chama kiwe na malengo. dr.Slaa alishapiga jaramba 2010 kilichobaki ni kuingia uwanjani(ikulu). Zitto bado anao mda wa kujipanga na umri unaruhusu. hatutaki kupoteza nguvu kazi kama Slaa ipotee hivihivi. Inabidi dr.Slaa atoe mchango wake kwa taifa lake nasi tumfaidi.

si muwapambanishe kwenye kura za Maoni? Au mnaogopa matokeo ya kura za maoni au mdahalo kati ya Slaa na Zitto? Kama nyie ni wanademokrasi mngeruhusu watu wajitokeze then ipigwe kura ya maoni tujiridhishe kuwa kweli mgombea wenu ni chaguo la wanachama sio kujifungia chumban mnaibuka na jina la mgombea,kura ya maoni ndo inatumika Dunia nzima nyie mnaogopa nini kama mgombea wenu ni chaguo lenu?
 
Zitto sawa na mtanzania mwingine yeyote anayo haki ya kugombea urais. Lakini watanzania nao kwa upande mwingine wanayo haki ya kumfahamu mtu yeyote anayekusudia kuwaongoza. Tunataka kujua kwa mfano yale mawasiliano ya Zitto na adui namba moja wa watanzania Rostam Aziz usiku wa manane yalilenga nini. Tumekwisha umwa na nyoka hivyo tukiguswa hata na unyasi tunakuwa na wasiwasi.
 
mkosoe kwa hoja,hakujiunga Chadema baada ya kuchakachuliwa kura na CCM kama wengine,hakuna mwanasiasa asiejisifia,nitajie hata mmoja ili nikiri kuwa sifahamu siasa,hata Mwl Nyrere ambae ndo kioo cha wanasiasa alikuwa akijisifia kwa mazuri alokuwa anafanya, pitia andiko la zitto then edit kila kwenye jina la zitto andika la yule jamaa yako ili uridhike,sera za CDM unazotamba nazo mitaani ni jasho la mboe na zitto upende usipende,usifie usisifie!

Very true broda wanaomsakama Zitto kwa waliokuja baada ya Zitto na Mbowe kujenga chama ni watu wanaofuata mkumbo na hao msiwahesabu kama ni wanachama wenu kwani wanaemshabikia akiondoka ataondoka nao na nina wasiwasi hao ni wale waliokuwa wanamshabikia mhe lyatonga (nadhani mwenye akili atajua nasema nini)
 
Zitto sawa na mtanzania mwingine yeyote anayo haki ya kugombea urais. Lakini watanzania nao kwa upande mwingine wanayo haki ya kumfahamu mtu yeyote anayekusudia kuwaongoza. Tunataka kujua kwa mfano yale mawasiliano ya Zitto na adui namba moja wa watanzania Rostam Aziz usiku wa manane yalilenga nini. Tumekwisha umwa na nyoka hivyo tukiguswa hata na unyasi tunakuwa na wasiwasi.

Gagnia je akitokea mtu mwingine akasema mathalani mhe slaa yeye ni mpe madaraka baada ya kubwangwa kwenye kura za ubunge alipokuwa ccm akakataa kubaki kwenye chama akakimbilia kwa kina zitto na je kuna uhakika gani ikitokea asiteuliwe kwenye urais au ubunge hataondoka chamani utamjibu nini? Siasa ni tofauti na unavyofikiria wewe mkuu kuna wakati inakubidi uwe na wale wanaooneka hawafai ili uweze kuwin kwenye baadhi ya mambo.

Nimeshazungumza mara kadhaa sisi waafrika tuna matatizo nadhani vijinasaba vyetu vina chembechembe nyingi ya wivu, choyo na majungu na ndio maana hatuendelei.!!
 
Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.

Kiongozi, huo ujumbe wako ni murua na rahisi sana kuutoa lakini utamsaidia kidogo sana (if any) Zitto kufanya vizuri zaidi. Kama unamtakia mtu mwema basi ni vizuri ukamstua pale unapoona anaelekea kujikwaa. Na Kama atasema amefanya mengi lakini watu bado wanauliza then it is obvious that 'he's been shooting in the dark'. So, he needs to change his tactics.
 
Naomba ninukuu maneni ya Ernesto Sheka kwenye maandiko yake ya The Moment Of Truth:

Can CDM give that a chance to someone from nowhere?

Who is Ernesto Sheka?? He can't be trusted, he will never be a reliable source of information pertaining to Chadema's welfare!!

Tatizo lako kubwa ni moja tu, una chuki zisizo na msingi wowote dhidi ya chadema as an institution huku ukiwa na mahaba dhidi ya watu fulani fulani walioko ndani ya chadema, hususan wale wa dini yako. Kwa lugha nyepesi kabisa unaendekeza udini, na huo ndio unakitafuna chama chenu pendwa na ambao unawish kila siku kuusambaza kwa vyama vya wengine wenye akili zao.

Zitto Kabwe ni kiongozi wetu na sisi wenyewe wanachadema ndio tunafahamu thamani yake, na yeye anafahamu jinsi anavyothaminiwa ndani ya chama chake. Sasa hivi viherehere vyenu vya kujifanya kupika majungu mkidhani mtafanikiwa kuwagombanisha wanachadema na viongozi wao ni jitihada za vipofu gizani.

Ni jambo la kheri sana kwa Zitto kuonyesha matamanio yake ya kutaka kuwa raisi wa nchi hii kwakuwa ametoa mwanya kwa wanachama na wananchi kwa ujumla kumpima na kumtafakari uwezo wake, nia yake na uzalendo wake kwa watanzania, kuliko ninyi wanafiki na mafisadi mnaojificha ficha hadi dakika za mwisho mnaibuka kutafuta uraisi kwa kuwanunua wananchi na wanachama wenu.

Zitto Kabwe endelea kujiimarisha kamanda, wakati muafaka ukifika utapata nafasi ya kuwaongoza watanzania, kwakuwa uwezo huo unao, nia hiyo unayo na sababu za kuwaongoza watanzania katika nafasi hiyo ya uraisi unayo. Hawa wafitini na wapika majungu wasikupotoshe ama kukukatisha tamaa, kwakuwa wanafanya hivyo kwa ajili ya kukidhi matarajio yao.
 
What do you say?
Mh.Zitto....i don't think its bad for you to openly express your personal views as to whether you like vying for presidency or not...i think this is a basic right for any Tanzanian and i really wonder why people are wasting so much of their time on this.....On the positive note though....now that you are here in this thread......please..please please....what are you guys (CHADEMA MPS) doing concerning the implementation of the new mining law??????come on!!!don't you see that the country is being robbed of her natural resources (gold)day and night????

I recall you being among the Bomani mining committee....come on! What are you doing on the implementation of the committee's recommendations???.....you guys...don't you read about the way the mining companies are making huge profits from gold exports?????while our people are dying of dire poverty???..even around those gold mines??...these gold companies are making extremely huge profits from their international stock markets and you MPs are here discussing about becomng future presidents???really???are you really serious???

...please..please...go get that new mining law into action....by the way,why is that.. things are being passed by the parliament and thereafter not implemented????and you MPs tend to back to the parliament and continue with sessions as though things are ok????....i really don't understand you people.....
 
Zitto anaonekana Mtu mwema kwa macho.

Nakumbuka uchaguzi wa mwenyekiti wa chadema alivyokuwa anatoa povu yeye na kafulila, nakumbuka jinsi alivyo muunga mkono kafulila badala ya mgombea wa chadema 2010, nakumbuka alivyokuwa anamuunga mkono kafulila kutoka kwake chadema hadi akasema nipo nyuma yako nakufuata huko nccr, nakumbuka alivyosaliti wabunge wenzake waliposusia hotuba ya kikwete. Haya yananifanya nisimwamin anatembea na wenzake, wenyewe wanaangalia mbele yeye anaenda kinyumenyume.

Haaminiki.
 
Hii ndiyo itakuwa suluhu ya yale makundi mawili yanayopingana...Mbowe vs DR.SLAA.
 
Kiongozi, huo ujumbe wako ni murua na rahisi sana kuutoa lakini utamsaidia kidogo sana (if any) Zitto kufanya vizuri zaidi. Kama unamtakia mtu mwema basi ni vizuri ukamstua pale unapoona anaelekea kujikwaa. Na Kama atasema amefanya mengi lakini watu bado wanauliza then it is obvious that 'he's been shooting in the dark'. So, he needs to change his tactics.

Mkuu inategemea huyo anaesema/kumsuta ni nani? kama atasutwa na Mbowe au Bob Makani itabidi tutafakari na pengine tukubali usutwaji huo.

Hapa nimekumbuka usemi wa hekima uliomo katika Biblia unaosema, "Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana aendavyo." (Methali 14:15). Kwa hivyo, ili tusiwe wajinga,kabla ya kuzikubali au kuzikataa sababu hizo,zinazotolewa dhidi ya Zitto, inatubidi kwanza tuzichunguze; tena,kwa makini. Isije kuwa sababu waziotoazo watu zina malengo binafsi.
 
Je katiba ya chama chake inamkataza kuwa na ukaribu na Makamba? kama jibu ni ndio kwanini msimvue uanachama? acheni siasa za kijinga wakuu hivi wewe kama ni cdm huna ndugu ambae ni tlp? hamsocialize? kwa kuwa tu huyo ndugu yako hayupo chama kimoja na wewe? au ndugu zako wote ni wa chama unachikisapoort?

Msimsakame Zitto yeye ni mtu jasiri amethubutu kusema tofauti kama wengine wanavyoeleza chini chini au hujasoma hii kitu iliyoandikwa na wabara?

Hatujamsikia Mheshimiwa Mbowe akisema kama anautaka urais ila ukisoma hiyo habari utaona kuwa kuna kundi lake ndio linataka Mhe asimame 2015! Kundi lake linaenda chaka sababu wanayoitoa ni kuwa Mbowe ametumia pesa zake sasa wanamaana inabidi Mbowe awe Rais arudishe pesa zake? mfike mahali muwe mnaleta hoja zisionekana zina maslahi binafsi. Hakuna mtu asietaka kiongozi mwenye uchu wa maendeleo na hakuna atakae kiongozi mwenye uchu wa mali unless/only and if uchu huo huyo mtu atanufaika nao.

Vyama vyote vya siasa vitakuwa na mitikisiko kuelekea uchaguzi wa 2015 cdm hasa wanajf wengi humu mmekuwa mkimshutumu Pro Lipumba kugombea kila mara kama hakuna mtu mwenye uwezo mwingine zaidi yake, kwa kumpinga Zitto na Mbowe na kutaka Slaa aendelee mtajitofautisha vipi na CUF? Mbowe alishajaribu kadhalika na Dr Slaa pia hamuoni sasa apishwe mtu mwingine mwenye ambition atakaeweza kuwawakilisha 2015? nadhani kama mnaamini chama chenu kina sera thabiti swala la nani asimame halitakuwa gumu kwenu.

Tafakari.

Prof. Lipumba amegombea uraisi wa JMT mara nne bila kuonyesha dalili zozote za mafanikio; 1995, 2000, 2005 na 2010,na bado anakusudia kugombea, akijilinganisha na raisi wa senegal abdulaye wade, aliyechokwa sasa na wasenegal.

Maalim Seif amegombea urais wa SMZ, sasa SUKZ mara nne bila mafanikio japo alitoa ushindani mkubwa sana; 1995, 2000, 2005 na 2010.

Sasa unapojaribu kuwalinganisha hao wagombea wa kudumu na Mbowe aliyegombea mara moja-2005 na Dr. Slaa aliyegombea mara moja-2010 na kutoa upinzani mkubwa kwa ccm na hata kuonyesha dalili za kuing'oa ccm madarakani, unakuwa unatumia utaalamu gani ama vigezo gani kusema Dr. Slaa na Mbowe wawaachie wengine wakati umeshindwa kunyanyua kinywa chako kuwaasa viongozi wa chama pendwa chako kuacha kuwa wagombea wa kudumu na kuwapisha wengine.

Huu ugombea wao wa kudumu katika nafasi za uenyekiti wa chama na uraisi wa JMT kwa Lipumba na ugombea wa kudumu wa ukatibu mkuu na uraisi wa znz kwa maalim seif ndio chanzo cha timua timua iliyomkumba hamad rashid kwa kuhofia kumalizwa kwa usultani wao ndani ya chama. Na hapo ndipo mahali muafaka pa wewe kujikita kutoa ushauri mwanana wa kukiboresha chama chako. Kujaribu kujivika ushauri kwa chadema ni unafiki, narudia tena huo ni unafiki kwakuwa unafahamu kwamba hufanyi hivyo kwa moyo msafi bali husda tu ndio inakusukuma.
 
Naona kuna utata kwa jinsi watu wanavyochangia mada hizi, kama reference ni zitto mbona yeye ameweka wazi kuheshimu na kutii utaratibu wa chama, sasa tatizo lipo wapi? kama hoja haaminini(Ingawa sikubaliani na hoja hii) basi kamkataeni kwenye chama kwa hoja sio kutuletea majungu kwenye jamvi hili.
 
Prof. Lipumba amegombea uraisi wa JMT mara nne bila kuonyesha dalili zozote za mafanikio; 1995, 2000, 2005 na 2010,na bado anakusudia kugombea, akijilinganisha na raisi wa senegal abdulaye wade, aliyechokwa sasa na wasenegal.

Maalim Seif amegombea urais wa SMZ, sasa SUKZ mara nne bila mafanikio japo alitoa ushindani mkubwa sana; 1995, 2000, 2005 na 2010.

Sasa unapojaribu kuwalinganisha hao wagombea wa kudumu na Mbowe aliyegombea mara moja-2005 na Dr. Slaa aliyegombea mara moja-2010 na kutoa upinzani mkubwa kwa ccm na hata kuonyesha dalili za kuing'oa ccm madarakani, unakuwa unatumia utaalamu gani ama vigezo gani kusema Dr. Slaa na Mbowe wawaachie wengine wakati umeshindwa kunyanyua kinywa chako kuwaasa viongozi wa chama pendwa chako kuacha kuwa wagombea wa kudumu na kuwapisha wengine.

Huu ugombea wao wa kudumu katika nafasi za uenyekiti wa chama na uraisi wa JMT kwa Lipumba na ugombea wa kudumu wa ukatibu mkuu na uraisi wa znz kwa maalim seif ndio chanzo cha timua timua iliyomkumba hamad rashid kwa kuhofia kumalizwa kwa usultani wao ndani ya chama. Na hapo ndipo mahali muafaka pa wewe kujikita kutoa ushauri mwanana wa kukiboresha chama chako. Kujaribu kujivika ushauri kwa chadema ni unafiki, narudia tena huo ni unafiki kwakuwa unafahamu kwamba hufanyi hivyo kwa moyo msafi bali husda tu ndio inakusukuma.

Kabla ya kupost fuatilia matokea ya urais ya maalim seif na shein au karume, nani aliyeonyesha upinzani mkubwa sefi aliyepata zaidi ya 45% au slaa.
Mapenzi yako kwa slaa yasikufanye kuwa kipofu
 
Huyu kaka anamapungufu. Nasikia eti hajaoa!!!!. Hii post ni ya wababa, kijana kama huyu hajatulia, wachumba watamsumbua, Ikulu itajaa vichupi so badala ya ku deal na issue atadeal na vichupi
 
Kabla ya kupost fuatilia matokea ya urais ya maalim seif na shein au karume, nani aliyeonyesha upinzani mkubwa sefi aliyepata zaidi ya 45% au slaa.
Mapenzi yako kwa slaa yasikufanye kuwa kipofu

Sasa hapa umeandika nini kama hata maandishi yangu huwezi kuyasoma na kuyaelewa?
Nimeandika hivi kuhusu maalim seif "Maalim Seif amegombea urais wa SMZ, sasa SUKZ mara nne bila mafanikio japo alitoa ushindani mkubwa sana; 1995, 2000, 2005 na 2010".

Au hata hapo nilipopigia mstari hupaelewi? usikurupuke kijana tuliza akili unaposoma comments za watu hapa JF.
 
Zitto = Rostam Aziz

Nadhani chadema inabidi iwafunze adabu juu ya viongozi wenu halafu ndio muingie kwenye mchakato wa kuchukua Serikali. Kwa mtazamo wangu nyie (washabiki) maana sidhani kama kwa maneno yako una chembe ya kuwa mwanachama!

Nimekuwa nikisema wenye mapenzi na Zitto watamwtukana Slaa kwa majina mabaya tumeona maneno kama "hawara yako" na mengine mengi yakitumika dhidi ya Dr pale watu walipokuwa wakihoji milioni kumi zisemwazo zililipwa kwa Josephine Mushumbuzi. Ukisoma thread ile kuna watu walienda mbali sana kumtukana Mhe Slaa!

Sasa leo tena wapo wenye uthubutu wa kumvurumishia maneno ya kashfa Zitto sasa ili mzizi wa fitina muukate mjifunze nidhamu kwanza au mumwachie Shibuda agombee uraisi au mnasemaje?
 
Huyu kaka anamapungufu. Nasikia eti hajaoa!!!!. Hii post ni ya wababa, kijana kama huyu hajatulia, wachumba watamsumbua, Ikulu itajaa vichupi so badala ya ku deal na issue atadeal na vichupi

Basi kwa wanaotajwatajwa cdm ni mbowe peke yake mwenye ndoa huoni ni busara yeye akigombea?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom