Zitto kugombea urais 2015?

Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.
Tuzungumzie mustakabali wa 2010. Mambo ya 2015 yawe pending.
 
Ahahahahahaaaaaa, jamani msameheni huyu anataka kutuzingua tusahau wajibu wetu wa kuchambua mambo muhimu. Hatujamaliza suala la sasa la kuona kama Waadilifu wanaingia Ikulu wewe unafikiriamgombea mwingine? Tuhakikishie kwanza kuwa tayari Slaa ni presindent alafu changes ni za kawaida. Alafu angalia popularity ya zitto kwa sasa uilinganishe na ya Slaa, sasa mie nakupa taarifa iliyoko ndani kuwa hata Slaa asipoenda ikulu akaenda Jk japo si kwa kishindo kama zamani, itaanza kampeni ya nyumba kwa nyumba kwa ajili ya 2015. Pia Kumbuka hadi Slaa anakuwa mgombea uraisi hakuchukua fomu ya Kugombea Urais bali alichukua ya Ubunge lakini akaombwa a chama chake agombee Urais. Kwa hiyo zitto kutoa kauli hiyo ni sawa tuu.
 
hata kama katiba itabadilishwa ili kumruhusu zitto kugombea akiwa na umri huo,baraza la wazee wa kichaga (samahani,ni la CHADEMA-CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO) litamwambia zitto hatuwezi kumweka mgombea urais tusiemjua,kama alivyoambiwa kwenye sakata la uenyekiti,labda silimu na awe mchaga!!
 
CHADEMA haiendi kwa mazoea ya CCM...Miaka 10 kama unaperform term moja tu kama poor performance au hutaki tu kuendelea kama Mandela. Kama Zitto anataka should prepare!
 
hata kama katiba itabadilishwa ili kumruhusu zitto kugombea akiwa na umri huo,baraza la wazee wa kichaga (samahani,ni la CHADEMA-CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO) litamwambia zitto hatuwezi kumweka mgombea urais tusiemjua,kama alivyoambiwa kwenye sakata la uenyekiti,labda silimu na awe mchaga!!

Hata Iweje,kanisa Katoliki Haliwezi Kuniambia Nimchague Slaa!! 2010 Hatugawanyiki!!

Mchague Bi Mkubwa Salma
 
Wadau vipi? Mbona tunahama mada. Swala lililopo mbele yetu ni kupata Rais mwadilifu ni mabadiliko. Naona huyu Bwn anania ya kutuyumbisha tubadili mwelekeo wetu. Sema usemalo fanya ufanyalo lengo letu ni kupata Presida Mpya si huyu anayelinda mafisadi. Tuwe na msimamo swala la Zito na kugombea Uraisi bado liko mbali. Na hapa hatuangalii ukabila ndugu, Tanzania ni yetu wote bila kujali dini kabila na rangi.

'' The write to be heard does not automatically include the right to be taken seriously''. Hubert H. Humphrey.
 
hata kama katiba itabadilishwa ili kumruhusu zitto kugombea akiwa na umri huo,baraza la wazee wa kichaga (samahani,ni la CHADEMA-CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO) litamwambia zitto hatuwezi kumweka mgombea urais tusiemjua,kama alivyoambiwa kwenye sakata la uenyekiti,labda silimu na awe mchaga!!

Very shallow mind like the rest of your kind
 
Wadau vipi? Mbona tunahama mada. Swala lililopo mbele yetu ni kupata Rais mwadilifu ni mabadiliko. Naona huyu Bwn anania ya kutuyumbisha tubadili mwelekeo wetu. Sema usemalo fanya ufanyalo lengo letu ni kupata Presida Mpya si huyu anayelinda mafisadi. Tuwe na msimamo swala la Zito na kugombea Uraisi bado liko mbali. Na hapa hatuangalii ukabila ndugu, Tanzania ni yetu wote bila kujali dini kabila na rangi.

'' The right to be heard does not automatically include the right to be taken seriously''. Hubert H. Humphrey.

The spelling was wrong in the Quote -right to heard. The art of progress is to preserve order amid change- and to preserve change amid order. ''Alred North Whiteheard''.
 
Anthony Kayanda, Kigoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amezua jambo jingine kwenye chama chake cha Chadema baada ya kueleza kuwa kelele zote ndani ya chama hicho, zinatokana na fitina ambazo zimejengwa baada ya kutangaza kuwa mwaka 2015 atagombea nafasi kubwa kwenye uchaguzi mkuu.

Tamko lake kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha kwenye Uwanja wa Cine Atlas mjini Kigoma juzi unaonekana kukaribisha mgogoro mwingine baina yake na wanachama wenzake baada ya kutuhumu kuwepo na njama dhidi yake kutokana na nia ya kugombea urais mwaka 2015 baada ya Dk Slaa kuzoa kura nyingi katika uchaguzi wa mwaka huu alipogombea nafasi hiyo.
Zitto, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akitofautiana na wanachama wenzake kiasi cha kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika uongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alisema hayo juzi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika eneo la Cine-Atlas lililo Ujiji mjini Kigoma.

Zitto aliuambia mkutano wa hadhara kuwa kelele zote ndani ya Chadema zimetokana na fitina zinazotengenezwa dhidi yake kwa kuwa kuna uwezekano kwake wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"Baada ya uchaguzi kumalizika, watu sasa wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine. Kuna watu wanaotaka nihame Chadema kwa kuwa wananiona ni kikwazo kwao, lakini nasema siwezi kuhama kwa kuwa nina mtazamo wa mbele wa kugombea urais," alisema Zitto.

"Kigoma inaweza kumtoa rais ingawa watu wanasema haiwezekani kwa sababu ni mwisho wa reli (ya Kati). Nasema siwezi kufanya makosa ya kuhama kama walivyofanya walionitangulia na wakapoteza dira.
"Kingine najua mtakuwa mmesikia mengi kupitia vyombo vya habari, lakini nataka niwaeleze kwamba sikulishwa sumu na hakuna anayeweza kunipa sumu."
Mbunge huyo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chadema, aliongeza kusema: "Mimi sing’oki Chadema kamwe na wale wanaotaka nitoke basi waanze wao. Kwa sababu, chama hiki ni chetu. Watu waliteswa, walifungwa jela, hata kupigwa na polisi na kuumizwa kwa ajili ya Chadema. Nasema siwezi kukimbia hata mara moja."

Alisema baadhi ya watu wa Kigoma waliokuwa viongozi wa Chadema na kuamua kukimbilia CCM baada ya kutokea mifarakano ndani ya chama hicho, wamejikuta wakipata aibu kwa kupoteza heshima mkoani Kigoma.
Alisema viongozi hao licha ya kukimbilia CCM, bado mkoa huo haujapiga hatua yoyote kubwa ya kimaendeleo jambo linaloonyesha kwamba maendeleo hayaletwi na chama bali ni juhudi na mikakati ya viongozi kwa kushirikiana na wananchi katika kuibua miradi, kuisimamia na kuitunza kwa faida ya Jamii.

Zitto alibainisha kuwa migogoro yote inayoonekana Chadema ni mchakato wa kidemokrasia lakini kwa ujumla mambo ni shwari ndani ya chama hicho.
"Ndugu zangu nataka niwaambie kwamba, kwa kawaida, baada ya uchaguzi mmoja, watu hujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao. Sasa haya mnayoyasikia ni mchakato wa kidemokrasia tu ndani ya Chadema, lakini kwa ujumla mambo ni shwari," alisema.

Zitto ametoa kauli hiyo takriban majuma mawili tangu alieleza gazeti hili kuwa ameamua kutozungumzia masuala ya chama chake kwa kuwa ameona kufanya hivyo ni kuchochea migogoro.
Zitto alikuwa ametakiwa kutoa msimamo wake baada ya kamati kuu ya Chadema kukataa kuidhinisha uamuzi wa wabunge wa chama hicho kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye na kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kupima mwenyewe uzito wa kitendo hicho cha wabunge wenzake.

Katika hatua nyingine, Zitto aliwataka viongozi wa Chadema kujiuliza sababu zilizosababisha NCCR Mageuzi kushinda majimbo manne mkoani Kigoma huku walioshinda ubunge wakiwa wanachama walioihama Chadema.
"Viongozi (Chadema), tunapaswa kukaa chini na kutafakari kwa kina, tatizo lipo kwetu sisi viongozi au tulisimika wagombea wasiokubalika?
"Kati ya wabunge wanne wa NCCR, watatu walikuwa viongozi wetu wa chama hadi mwaka 2009 na kama tungekaa nao vizuri, pengine leo hii wangekuwa wabunge wetu na kuongeza idadi yetu Kigoma."

Aliwaeleza Wananchi hao kwamba Serikali ina tabia ya kusikiliza sauti ya Kigoma wakati mbunge anapokuwa chama cha upinzani na kwamba hali hiyo imechangia mkoa huo kuanza kupata miradi ya barabara kadhaa za lami, hivyo kurahisisha shughuli za uchukuzi na usafirishaji, jambo lililokuwa kikwazo kwa miaka mingi mkoani humo.

Kuhusu kesi inayomkabili mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Ally Mleh Zitto alieleza kwamba wabunge wa Chadema wanaotoka Kigoma watahakikishiwa wanaisimamia kesi hiyo, ili iweze kusikilizwa na maamuzi kutolewa kwa haki na kwamba chama hicho kinatarajia ushindi.

Zitto alisema kwa mujibu wa fomu za matokeo zilizokusanywa kutoka vituoni, mgombea wa Chadema alishinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.
Katika uchaguzi huo zilizuka vurugu kubwa baada ya polisi kuwapiga mabomu ya mochozi wananchi waliofurika kwa wingi katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini kufuatilia matokeo.

Hata hivyo, Serukamba aliwaeleza wananchi Desemba 17 kwamba kamwe hatarajii kupoteza nafasi hiyo kutokana na kesi dhidi yake kutokuwea na ushahidi wowote wa kumkwamisha.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza Januari 15, 2011 katika Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi ambapo inatarajiwa kutawala hisia za wengi ndani na nje ya Jimbo hilo.
 
Zitto anajua kwa nini NCCR wameshinda Kigoma, kauli yake hapa chini ni tata:

"Kati ya wabunge wanne wa NCCR, watatu walikuwa viongozi wetu wa chama hadi mwaka 2009 na kama tungekaa nao vizuri, pengine leo hii wangekuwa wabunge wetu na kuongeza idadi yetu Kigoma."

Malaba, hebu acheni habari za Zitto, kila siku Zittto Zitto, hakuna wanasiasa wengine wa kuwajadili? Mbona wengine hamwasemi? Zitto alikwisha kusema kuwa mwaka 2015 hataweza kugombea Urai kwani atakuwa na miaka 39 na katiba ya nchi inatamka kuwa mgombea urais ni lazima asiwe chini ya miaka 40. Mbona huo uzushi mnauendelezaaaa pamoja na magezeti ambalo hujaweka source yake?

ZITTO JENGA CHAMA CHAKO, ACHANA NA WAZUSHI KWANI WENGI HAWAPENDI CHADEMA KIKIKUA, ILA KUMBUKA KUWA WAO WANA FEDHA NA SISI TUNA MUNGU, KUPIA KWA NGUVU YA WANANCHI..........
 
ndugu Masaiti , hii habari imeandikwa na gazeti la Mwananchi.
Hat mimi najua lazima ufikishe 40y kugombea uraisi, lakini lazima tujifikirie kwanini asema hayo maneno kwa kauli yake mwenyewe? je anayemdanganya ni nani? sipendi kumsifia mtu bila sababu ila naamini kuwa yamtokayo mtu kinywani wake ndio yaujazao moyo wake.
si mnataka kubadilisha katiba, labda na hilo la age limit anajua litakuwa limeshabadilishwa ..who knows?
Malaba, hebu acheni habari za Zitto, kila siku Zittto Zitto, hakuna wanasiasa wengine wa kuwajadili? Mbona wengine hamwasemi? Zitto alikwisha kusema kuwa mwaka 2015 hataweza kugombea Urai kwani atakuwa na miaka 39 na katiba ya nchi inatamka kuwa mgombea urais ni lazima asiwe chini ya miaka 40. Mbona huo uzushi mnauendelezaaaa pamoja na magezeti ambalo hujaweka source yake?

ZITTO JENGA CHAMA CHAKO, ACHANA NA WAZUSHI KWANI WENGI HAWAPENDI CHADEMA KIKIKUA, ILA KUMBUKA KUWA WAO WANA FEDHA NA SISI TUNA MUNGU, KUPIA KWA NGUVU YA WANANCHI..........
 
Chadema hatuwez kuruhusu mtu anayejulikana kigoma peke yake kugombea urais

akagombee huko kwa rafiki yake Kafulia
 
huyo ametumwa sio bure.hivi anajiona kuwa yeye ndo maarufu sana au bora sana kuliko wanachama na viongozi wote CDM?hata mie ntagombea urais 2015 lakini sio kwa mbinu chafu kama zake.
Naanza kumuonea huruma Mbowe kwa kuhairisha safari yake ya wingereza kipindi kile ili kumuandalia mapokezi mazito zitto baada ya kusimamishwa mjengoni,maana hakujua kama shida ya huyu bwana mdogo ndio ingeanzia hapa.keshatanika kichwa kwa sifa anajiona kama Mungu.
anadhani akigombea anaweza kupata hata robo ya kura alizoleta SLaa?kikwete na yeye afadhali kikwete.
 
.. Zi kugombea Urai kwani atakuwa na miaka 39 na katiba ya nchi inatamka
kwani kasema atagombea 2015?

kasema tu atagombea, kama ni kweli kasema

hajataja mwaka

Huyu Malaba ndie kaongeza huo uzushi wa 2015
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom