KakaJambazi
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 18,830
- 12,291
Mh Zito ikiwekwa clip ya jana ya TBC utaumbuka. Mimi mwenyewe nilidhani "photoshop"
Jamani umeme umekatika hapa kijijini kwetu, hapa natumia kibatali huku betri ya laptop yangu ikisaidia.
Kuweni na subira.
Maneno mazuri. Kama Zitto anajitambua kuwa ni target ya watu wanaosubiri mkono udondoke iwe kwa mazuri au mabaya inabidi awe mwangalifu anapotamka ajaribu kuchuja maneno. Wengi wanamwangalia kosa kidogo tu litakuzwa. Ni sawa na kudondoka kwa rais jangwani, wangapi siku hiyo walidondoka pale jangwani lakini aliyeonekana ni mmoja tu. Wakati anajiuliza hayo vile vile ajaribu kujiuliza kwa nini TBC ika select tukio hilo likawa News na si mengine.Zitto akitajwa tu hapa JF kila mmoja anachomoka kutoka kwenye pango lake, angalau apate moja, wawili kutoka kwake ama asikie wengine wanasema je kumhusu. Hii ni kuonyesha kuwa kijana Zitto ni figure ya kitaifa.
Na amekuwa akitumiwa kama nanga kwa wale walio marafiki zake, na kama upanga kwa wale walio adui zake.
Lakini Zitto namwaminia kwa kusoma katikati ya mistari kwa kila issue inayoinuliwa ama kwa nia ya kumjenga au kumbomoa.
Amefanikiwa kuwa kijana mwanadiplomasia wa kitanzania mwenye uwezo sii tu wakuyakwepa majungu nchini kwake bali mwenye uwezo wa kujenga mahusiano ya kitaifa na kimataifa. Ref. Mazungumzo yake na raisi wa Ujerumani. Mtakumbuka kuwa rais mtarajiwa Dr W. Slaa aliombwa na chama kuwania urais wakati tayari alishachukua form ya kuwania ubunge. Hii inaonyesha kwamba Slaa hakimbilii ikulu bali anatumwa na watu. Ni dhahiri kwamba Zitto angeweza kuombwa ili atumwe yeye ikulu na anao uwezo huo kwani raia tumeuona uwezo wake wa kusimamia masuala ya kitaifa bungeni. Kizuizi pekee kwa zitto katika urais kwa sasa ni umri. Hivyo Zitto ana kila sababu ya kuwa rais wa Tanzania baada ya Slaa. Na hilo kijana atazidi kulingarisha katika bunge lijalo kwa hoja zake makini za uzalendo na utetezi wa rasilimali za nje. Kwa sasa nguvu zote zimeelekezwa kwa Slaa katika nafasi ya urais ila imebidi tuwe na mjadala huu kwa sababu ya dhamira ya upotoshaji habari uliyofanywa na TBC1 kumhusu Zitto.
Dr SLAA KUTINGA MAGOGONI.
INAWEZEKANA!!
Jaribu kuelewa katika context.Na mimi ngoja nikusaidie. Chance ya Zitto kugombea 2015 si kuwa ni ndogo tu ila haipo kabisa kwa vile katiba haimruhusu he will be 39 by that time. Kwa hiyo bado narudia tena conclusion yako ni butu kwa vile ime base kwenye wrong hypotheses.
Nipo naangalia Taarifa ya habari, nimemuona zito kabwe akihutubia kwenye kampeni za kuomba ubunge huko jimboni kwake kigoma. Katika mkutano huo Kabwe anawaeleza wananchi kuwa mwaka 2015 hataenda tena jimboni hapo, lakini si kugombea ubunge tena bali ni URAISI. Hivi ni nini mantiki ya hii kauli kwa kiongozi mwandamizi wa chama. Je ni kauli ambayo inaleta taswira gani, Je inajenga au inabomoa?
Jaribu kuelewa katika context.
Mimi ninachoongelea hapa ni Zitto kusema ana mpango wa kugombea 2015 wakati chama cha chake kiko kwenye kampeni za kumuuza mgombea urais wao kwa wananchi.Swala la kwamba 2015 hatakuwa na sifa za kugombea,huko ni kujaribu kutoka nje ya hoja yangu.
.Nipo naangalia Taarifa ya habari, nimemuona zito kabwe akihutubia kwenye kampeni za kuomba ubunge huko jimboni kwake kigoma. Katika mkutano huo Kabwe anawaeleza wananchi kuwa mwaka 2015 hataenda tena jimboni hapo, lakini si kugombea ubunge tena bali ni URAISI. Hivi ni nini mantiki ya hii kauli kwa kiongozi mwandamizi wa chama. Je ni kauli ambayo inaleta taswira gani, Je inajenga au inabomoa?
Hii style ya kupiga kampeni double double sijawahi kuiona.
Sasa basically anawaambia watu wa jimbo lake kwamba "nyinyi ni stepping stones tu, macho yangu yanakodolea Ikulu"
Hypothetically speaking, Slaa akishinda urais 2010, 2015 atamwachia Zitto agombee? Au itabidi Zitto afulie ?
Au ndiyo Zitto anasema kijanja kwamba hana imani kwamba Slaa atashinda urais ?
Bad timing, not a mature look at all.
Wow Kibs, I am impressed!!!
But you forgot to put the 's' in front of 'term'. It should've been 'terms'...but hugely impressed, nonetheless.
Back to your question, yes, I don't like him all around (qualification-wise, his attitude, his personality, you name it)
Zitto kishaona kwamba Slaa hawezi kuukwaa Rais mwaka huu wala hiyo 2015 kwa namna zozote zile. Ametathmini kwa makini sana. Always mtu makini sana huwa hapendwi popote Duniani.
wacha vituko vyako...!Lakini baada ya kusoma hiyo ya Kibs na tahariri yako juu yake imebidi nicheke tu... :becky: So funny!!
...Mimi siwezi kuzuia TBC kutoa habari wanayotaka kutoa na wala siwalaumu TBC kwa kutoa habari hiyo kwani ni jambo lililotokea na umma una haki ya kuhabarishwa..
...Basi fanyeni ceasefire ili tupite katika mchakato huu wa kusaidia mabadiliko katika nchi yetu. Mie nipo Kigoma nasaka kura za chama changu. Nanyi kokote mlipo chakarikeni. Kuna muda wa kutosha mwingi wa kutoa maoni kuhusu Urais wa Zitto mpaka ifike 2015. Wenye ya kusema watasema mengi na nitawasikiliza. This is Slaa time, not my time........... lets focus!
wacha vituko vyako...!
.
kuna mgogoro chadema, haiwezekani katikati ya kampeni za kumnadi Dr Slaa naye Zitto anajipigia kampeni ya Urais mwaka 2015 badala ya kumpigia kampeni Slaa. Kwa mfano, Slaa anashinda( utani tu) na kisha akawa na vipindi viwili 2010- 2020 kwa mujibu wa katiba.Haijawahi kutokea hapa nchini chama kinamnadi mgombea wake wa urais na mwingine ndani ya chama hicho hicho hatokei katika uzinduzi wa kampeni za chama chake (chadema) pale Jangwani na kuibukia kwao kigoma kutangaza Urais. Wenye akili watajiuliza kulikoni chadema? Je, wanastahili kuingia IKulu na mwendo huo.
Am sorry zitto, Ngoja niwe mkweli
Jana niliangalia hiyo taarifa ya TBC, wewe ndo ulianza ukisema " mwaka 2015 nataka nije kugomea urais nitaomba kura zenu" hapa wewe ndo ulianzisha, kama vile wananchi hawajasikia ukawauliza tena "mwaka 2015 nataka nigombee (mike ikaelekezwa kwa wananchi).... wananchi wakajibu Uraisssssss........."
Pili, katika hotuba ya jana sikusikia unanadi sera za chama
sera ulizokuwa nazo ni za kibinafsi,,,, ulisema utajenga barabara mbili.....cjui hii kama hipo kichama.....
Zitto naanza kuwa na wasiwasi nawewe......maana nguvu zako sasa hivi zimerudi nyuma
swali:
Kwanini uliomba michango ya kibinafsi na sio cham?
Ngabu, Nilichukizwa sana na distractions zako kwa hoja iliyopo mbeleni, kwa kusahihisha makosa ya kiuandishi ya Mh. Zitto badala ya kumlima maswali yahusianayo na mjadala kwa ku-capitalize kwenye fursa hii aliyopata kuweza kuingia JF...
Lakini baada ya kusoma hiyo ya Kibs na tahariri yako juu yake imebidi nicheke tu... :becky: So funny!!
Ndugu zangu wana JF,
Toka asubuhi nimekuwa nikisoma maoni yenu kuhusiana na habari iliyorushwa na TBC1 kuhusiana na mimi kugombea Urais mwaka 2015. Kwanza, sio jambo zuri sana kudakia mambo bila kuwa na hbri za kutosha na kuhukumu watu. Watu makini husikia au kusoma mambo, kuyatafakari na kisha kuyatolea maoni. Pili, ni vema ifahamike kuwa mazingira niliyokuwa ninahutubia ni mazingira ya namna gani na kwamba kauli ya Urais ni kauli kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kidahwe na wala sio kauli yangu. Ni kauli na maono ya watu wa Kigoma na nadhani sio dhambi hata kidogo. Mimi ni mwanasiasa na ninafahamu kanuni za mchezo huu. Kamwe siwezi katika kipindi hiki kuanza kutoa kauli za kuondoa attention kutoka kwa mgombea Urais wa chama changu. Mimi siwezi kuzuia TBC kutoa habari wanayotaka kutoa na wala siwalaumu TBC kwa kutoa habari hiyo kwani ni jambo lililotokea na umma una haki ya kuhabarishwa. Mimi nipo jimboni kwangu ninafanya kampeni za kuomba kura za HESHIMA. Pia ninamwombea kura Katibu Mkuu wangu Dr. Slaa ili awe Rais. Kila tukio la kampeni zangu ninaweka katika blogu yangu na pia katika facebook Zitto na Demokrasia. Ninaomba wenye kuhitaji kufuatilia matukio ya Kigoma wafuatilie huko.
Ndugu zangu, busara ya kawaida inasema hiki ni kipindi cha kufanyakazi za kutafuta mabadiliko katika nchi yetu. Sio kipindi cha kushutumiana na kuzushiana mambo. Tuwe na staha. Hatutaleta change katika nchi yetu kwa kusemana na kusengenyana. Hatutaleta mabadiliko kwa kutegeana makosa. Angalau kwa kipindi hiki basi tuelekeze nguvu zetu katika kusaka kura za kuleta mabadiliko. Tunahitaji Madiwani, Wabunge na Rais.
Ninasononeshwa sana na muda unaopotea kusema Zitto hivi ama vile. Najua kuna Zitto haters humu. Basi fanyeni ceasefire ili tupite katika mchakato huu wa kusaidia mabadiliko katika nchi yetu. Mie nipo Kigoma nasaka kura za chama changu. Nanyi kokote mlipo chakarikeni. Kuna muda wa kutosha mwingi wa kutoa maoni kuhusu Urais wa Zitto mpaka ifike 2015. Wenye ya kusema watasema mengi na nitawasikiliza. This is Slaa time, not my time........... lets focus!
Hao wananchi wa kijiji cha Kidahwe walisema nini na wewe ukasema nini? Tuhabarishe tafadhali...
Zitto,
Hujajibu swali, ulisema chochote kuhusu urais 2015? Walichosema wananchi ni nini na ulichosema wewe ni nini?
Sasa kwa nini hukuingia na kuanza kumlima hayo maswali kama uliona mimi sikufanya hivyo?