Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kuna taarifa (toka TBC1) kuwa leo Zitto katoa tamko rasmi kuwa ana mpango wa kugombea urais wa Tanzania mwaka 2015 na akawaomba wananchi wampe kura nyingi ili apate hadhi ya kuweza kugombea urais wa nchi hii.

Kila la heri mkuu Zitto, walau una nia! Je, katiba itabadilishwa?

LAKINI

Zitto hawezi kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kwenye uchaguzi wa 2015 kwa sababu hizi zifuatazo:

1. Zitto amezaliwa September 24, 1976. Hivyo, mwaka 2015 atakuwa ametimiza miaka 39 Inshallah. Katiba inasema mgombea Urais Tanzania awe na si chini ya miaka 40.

2. Zitto amechafuka ndani ya CHADEMA kama Lowassa alivyochafuka ndani ya CCM. Wakati CCM wanaweza kumchagua Lowassa kuwa mgombea wao wa Urais 2015 kutokana na upumbavu wao, CHADEMA si wapumbavu.

3. Bado Watanzania wanamhitaji na kumwamini DK. WILLIBROD SLAA. Pamoja na kuwa DK. SLAA mwenyewe hana mpango wa kugombea 2015, wito wa Watanzania utakuwa ni mkubwa sana na nadhani ataitikia wito huo.

4. Hata yeye Zitto anajua kuwa hana nafasi ya kuwa mgombea Urais wa CHADEMA, hata kama DK. SLAA akiamua hagombei. Amejiharibia mwenyewe kwa uhusiano wake wa kifisadi na Rostam Aziz na watawala wa serikalini.

5. Zitto akiwa mgombea Urais wa CHADEMA, Watanzania wengi wataamua kutopiga kura au kumpigia kura mgombea Urais wa CCM.
 
Nipo naangalia Taarifa ya habari, nimemuona Zitto Kabwe akihutubia kwenye kampeni za kuomba ubunge huko jimboni kwake kigoma. Katika mkutano huo Kabwe anawaeleza wananchi kuwa mwaka 2015 hataenda tena jimboni hapo, lakini si kugombea ubunge tena bali ni URAISI. Hivi ni nini mantiki ya hii kauli kwa kiongozi mwandamizi wa chama.

Je ni kauli ambayo inaleta taswira gani, Je inajenga au inabomoa?
 
Uzuri ni kwamba hata akigombea atashindwa vibaya sana. Na ukitokea muujiza akashinda, basi Watanzania tumekwisha. Kama mlidhani Mkapa alikuwa na jeuri na nyodo, you ain't seen nothing yet!! Zitto is Mkapa on steroids na mimi nitafanya juu chini ashindwe na kulegea ktk jitihada zake hizo.
 
Akihutubia katika mkutano wa kampeni wa kuomba kura kwa wananchi, Zitto aliwaomba wananchi hao wampe kura nyingi zitakazompa heshima ili mwaka 2015 aweze kugombea Urais. Zitto alisema 2015 atakaporudi jimboni hapo atakuwa akisaka kura za Urais.

Kwa taarifa zaidi: Sikiliza Video Clip hii toka TBC:
 
Mheshimiwa Zitto ana kila haki ya kufanya hivyo Kikatiba lakini nina mashaka sana na Busara aliyotumia kutangaza adhma hiyo kipindi hichi.
 
Zitto hajui kuwa ktk siasa usiangalie mbele na kuruka kihunzi kilichopo mbele yako sasa. Badala ya kulenga ktk kushinda ubunge kwenye uchaguzi ujao yeye anaanza kutangaza nia za mwaka 2015.....to me that demonstrates poor judgment. Hafai kuwa raisi huyu kwa sababu nyingi tu.....
 
Hizi habari za kweli jamani ?

Kama za kweli, inamaana Slaa akishinda 2010, 2015 hatagombea? Au Zitto haamini kwamba Slaa anaweza kushinda 2010 ?
 
uzuri ni kwamba hata akigombea atashindwa vibaya sana. Na ukitokea muujiza akashinda, basi watanzania tumekwisha. Kama mlidhani mkapa alikuwa na jeuri na nyodo, you ain't seen nothing yet!! Zitto is mkapa on steroids na mimi nitafanya juu chini ashindwe na kulegea ktk jitihada zake hizo.

nitakuunga mkono ktk hili
 
Jamani umeme umekatika hapa kijijini kwetu, hapa natumia kibatali huku betri ya laptop yangu ikisaidia.

Kuweni na subira.
 
Nipo naangalia Taarifa ya habari, nimemuona zito kabwe akihutubia kwenye kampeni za kuomba ubunge huko jimboni kwake kigoma. Katika mkutano huo Kabwe anawaeleza wananchi kuwa mwaka 2015 hataenda tena jimboni hapo, lakini si kugombea ubunge tena bali ni URAISI. Hivi ni nini mantiki ya hii kauli kwa kiongozi mwandamizi wa chama. Je ni kauli ambayo inaleta taswira gani, Je inajenga au inabomoa?

Anatimiza haki yak ya kikatiba
 
Zitto hajui kuwa ktk siasa usiangalie mbele na kuruka kihunzi kilichopo mbele yako sasa. Badala ya kulenga ktk kushinda ubunge kwenye uchaguzi ujao yeye anaanza kutangaza nia za mwaka 2015.....to me that demonstrates poor judgment. Hafai kuwa raisi huyu kwa sababu nyingi tu.....
Aliingilia maslahi yako? Au alibeba ile dogox2 yako Mr NN? be open! ili na mimi nikuunge vidole:glasses-nerdy:
 
Kama ametanganza ni vema ametangaza mapema ili tupate muda wa kutosha kumpima... si vema kuwashtukiza watu katika suala nyeti kama hili. Lakini nilivyomsikia si kama ametoa tamko rasmi, maana alikuwa anawauliza watu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara pale Kidahwe
 
Kama ametanganza ni vema ametangaza mapema ili tupate muda wa kutosha kumpima... si vema kuwashtukiza watu katika suala nyeti kama hili. Lakini nilivyomsikia si kama ametoa tamko rasmi, maana alikuwa anawauliza watu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara pale Kidahwe

Hii style ya kupiga kampeni double double sijawahi kuiona.

Sasa basically anawaambia watu wa jimbo lake kwamba "nyinyi ni stepping stones tu, macho yangu yanakodolea Ikulu"

Hypothetically speaking, Slaa akishinda urais 2010, 2015 atamwachia Zitto agombee? Au itabidi Zitto afulie ?

Au ndiyo Zitto anasema kijanja kwamba hana imani kwamba Slaa atashinda urais ?

Bad timing, not a mature look at all.
 
Mkuu heshima mbele. Habari hizo si za kweli kwa sababu Zitto alishaeleza hadharani kuwa hawezi kugombea urais 2015 kwa sababu atakuwa hajafikia kiwango cha chini cha umri wa kugombea urais ambayo ni miaka 40. Mwaka 2007 ilielezwa kuwa alikuwa na umri wa miaka 30. Mwaka huu atakuwa na miaka 33, na mwaka 2015 atakuwa na miaka 38. Kwa umri huu hawezi kugombea urais mwaka 2015. Mwaka 2020 anaweza kugombea urais kama akitaka kwa kuwa atakuwa amefikisha miaka 43. Umri wa Zitto unaweza kuthibitishwa kwenye tovuti ya bunge la Tanzania
 
Huyu zitto mie nashindwa kumuelewa, kila kwenye sakata ndani ya chama mpaka na yeye jina lake lihusike hata kwenye kesi ya rushwa ya mgombea mwengine!

Labda atagombea kwa chama chengine na si chadema ndo maana haijalishi matokeo ya uchaguzi huu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom