Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,199
Tukutakie kheri katika ndoto hizi tamu kwa ndumirakuwili kama wewe!!
kwani kasema atagombea 2015?
kasema tu atagombea, kama ni kweli kasema
hajataja mwaka
Huyu Malaba ndie kaongeza huo uzushi wa 2015
Chadema hatuwez kuruhusu mtu anayejulikana kigoma peke yake kugombea urais
akagombee huko kwa rafiki yake Kafulia
Zitto anajua kwa nini NCCR wameshinda Kigoma, kauli yake hapa chini ni tata:
"Kati ya wabunge wanne wa NCCR, watatu walikuwa viongozi wetu wa chama hadi mwaka 2009 na kama tungekaa nao vizuri, pengine leo hii wangekuwa wabunge wetu na kuongeza idadi yetu Kigoma."
Kwa mtindo huu huyu jamaa hatafika popote.......................... CDM wamwache tu alopoke mpaka achoke mwenyewe. Kwenye politics inabidi uwe mkimya na watu ndiyo watambue uwezo wako siyo wewe kuwaeleza uwezo wako. Hakuna mtu aliyetegemea watu kama akina Yestin, Obama, Goabachev n.k ukwa watakuja kuwa marais................ila hiyo haimaanishi kuwa hawakuwa na hiyo nia. Kimya chao ndiyo kiliwasaidia na wakasubiri muda mwafaka. Unless yeye Zitto anataka kuwa kwenye historia kuwa aliwahi kugombea urais wa TZ kama walivyofanya akina Chemponda na the likes.
Asavali amegundua kwamba umaarufu wake pia unaambatana na chama chake..sasa kwanini alipinga msimamo wa chama chake bungeni ? mnafiki huyu.
Chadema hatuwez kuruhusu mtu anayejulikana kigoma peke yake kugombea urais
akagombee huko kwa rafiki yake Kafulia
Muwe na kumbukumbu.Hata kabla ya uchaguzi wakati akiwa kwenye kampeni zake alisema wamchague kwani 2015 anataka kugombea urais.hajasingiziwa.Lakini wakati fulani akiwa Shinyanga aliwahikusema asingegombea ubunge 2010 badala yake anataka kuendeleza taaluma yake hasa kuwa lecturer.Tusisahau mapema watanzania.Ndio maana tunashindwa kufuatilia ahadi za wanasiasa kwa ugonjwa wa kusahau sahau.
Zitto aseme yote lakini la kudai kuwa ndani ya chama kuna watu wanampiga vita hilo siliafiki. Yeye ndiye anatuchanganya. Makosa afanye yeye halafu arudi kusema kuwa kuna watu wanampiga vita? Ni yeye mwenyewe kwa utashi wake aliamua kukiuka makubalino ya wenzake ya kususia hotuba ya JK, na kama hiyo haitoshi akaenda kwenye vyombo vya habari kueleza namna alivyokiuka kanuni ya kuwajibika pamoja. Watu wakisema alikosea, tayari anaibuka na hija kuwa kuna watu wanataka atoke CDM. Actually wanachama na wapenzi wa CDM ndio wanamtaka aondoke na sio viongozi.
Sisi wana CDM tumekwisha mstukia na hata kama hataondoka kamwe CDM ajue tu kuwa yeye sio yule Zitto wa zamani, huyu ni Zitto mwingine ambaye haaminiki tena, na kama asipojirekebisha, anaelekea kwenye kaburi la siasa.
hilo analijua sana, ndio maana kasema kuwa hawezi kukihama CDM hata kwa mawe,anjua kabisa kuwa kafika hapo si bure bali Chadema
wanajamii acheni kupoteza muda wenu zitto kabwe aliokotwa na usalama wa taifa tokea alipokua kigoma sekondari alikua mpambe mzuri wa kaburu, then akaten.enezwa na kuwa anapewa information za kutosha na usalama wa taifa ili apate umaarufu then wamtumie kuiuwa chadema. They invested in him a lot, na pia that guy is very good in playing mind games. Chadema wawe makini sana na huyu bwana mdogo ni extremely smart, nadhani ni bora wawe makini sana na zito hata zaidi ya ccm, kwa sababu zitto kabwe ni KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.