Kati ya vitu ambavyo CHADEMA wame-prove kuwa wapo makini ni namna ambavyo wameweza kum-handle Zitto, chama ndiyo kilimfikisha hapo alipo, umaarufu wake ulianza pale alipotolewa bungeni lakini CDM ikaamua kumbeba na kuunganisha watu ili ichukulie kitendo cha kufukuzwa bungeni na matokeoa ya ushujaa wake, na msimamo dhidi ya maslahi ya taifa, kweli watu wakjitokeza kwa wingi baada ili kuitikia wito wa chama.
Alipoona makutano ya watu kiasi kile akajua hii ni shauri ya yeye kama yeye kama Zitto na si chama, imani ikajengeka ndani yake kuwa yeye ni zaidi ya chama, akaanza kufuata utashi na hisia zake, kama treni iliyoacha reli...waandishi waliokuwa wanamsifia wakaona mwelekeo wake hatari, Kibanda akaandika kuonya, Ngurumo akaandika, Happiness Katabazi akaandika, wengi wakaandika, sikio la kufa halisikii dawa, magazeti makini yakaachana naye, akaenda kuibukia kwenye magazeti ya udaku, akayashambulia magazetu yetu kuwa, magazeti ya udaku ndiyo yenye nguvu na yasomwayo na watu wengi duniani, hakufafanua watu wa aina gani. Muda si mrefu urafiki na magazet hayo ukaisha baada ya kuandika skendo zake za ngono na wasichana kadhaa wanaodhani kuwa majina yao ni makubwa hapa nchini, kumbe yanafahamika tu na wala hayana ukubwa wowote.
Turudi kwenye mada...akazua hali ambayo ilitafsiriwa kama kizaazaa ndani ya CDM, nadhani alifanya makusudi ili afukuzwe aondoke "kishujaa"(kama alivyopokewa jangwani) kwasababu kuna watu ndani ya CCM walimdanganya kuwa akifukuzwa na hata akiipoteza nafasi ya ubunge, atapewa wa kuteuliwa na rais, pia kupewa unaibu waziri, na ili kumhakikishia hilo akajengewa ukaribu na idara za usalama na watu mashuhuri walio pretend kwenda kwake kupata ushauri na msaada wa mambo kadhaa, akazidi kuwa jeuri, lakini maskini kijana huyu hakujua kuwa watanzania walishamuona kimeo muda mrefu uliopita kiasi cha viongozi wa CDM kuwekwa katika msukosuko na wananachama wao kuwa kwa nini wanamlea, lakini uongozi ulionyesha ukomavu kwa kuendelea kuwa naye na kumkumbusha maadili ya chama na siasa kwa ujumla.
Kabla ya kampeni mwaka za mwaka jana, alitishia kutogombea, lakinibaadaye akapima akapima akaona namna maisha yatakavyokuwa magumu nje ya siasa, kwani hakuna kazi itakayomlipa kama siasa, ukichukulia kwa muda huo alishaamua kushiriki siasa kwa maslahi binafsi, hivyo akabatilisha msimamo wake na kuamua kutetea kiti chake, kampeni zilipowadia, akijua kuwa chama chake kimesimamisha mgombea wa nafasi ya urais, lakini akaonyesha kuibeza hatua hiyo kwa kusema kuwa, tunakwenda kuchagua wabunge na madiwani kwani rais tayari tunae tumuache amalize muda wake, lakini uongozi wa CDM uliendelea kumvumilia, Kitendo hicho cha uongozi wa CDM kuendelea kumvumilia kimebomoa sana Image ya Zitto kwa jamii,na kuifanya CDM ionekana kama chama imara kinachoweza kuishi pamoja hata inapotokea wakatofautiana mawazo kati yao.....kwa hili CDM nawapa sifa sana. Zitto amechuja lakini hilo halitambui tena kwasababu sasa hivi anaishi kwa kutegemea taarifa za wapambe. Ameaminishwa kuwa kila ampingae ni walewale wanaotumiwa dhidi yake.
Sasa hivi ni naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni anaongoza watu wasio mkubali watu ambao walipiga kura ya kumkataa, maamuzi ambayo hayakuwahi batilishwa popote pale, lakini kwasababu ya upenzi wake kwa madaraka bila kujari anaongoza kwa mazingira gani as long as anapata chake, katika hili Zitto hataki kutumia akili yake kama mwanasiasa kijana na msomi kama anavyotaka kutambulika, ameamua kung'ang'ania madaraka hayo bila suluhu ya aina yoyote, hataki kupisha nafasi hiyo kwa mtu mwingine anekubalika.
Zitto ambaye nahisi kila aonapo wakina Mnyika, Lema Lissu na wengineo wakitoa hoja zinazotikisa bunge huwa hajisikii vizuri kwa kuumia moyo, akitamani hali hiyo ya bunge kutetemeshwa kwa hoja ingesababishwa na yeye. alijaribu kutengeneza 'msukule/Zombi' wake pale bunge (Kafulila), lakini sijui ulipoishia, japo kuna yule bint, simkumbuki jina lake ila nadhani ni wa viti maalum CDM, lakini wote wapo off-color.
Huyo ndiye Zitto kabwe, ambaye sasa anataka atambulike kama rais mtarajiwa, kwani ameshatangaza dhamira yake ya kugombea urais mwaka 20015, Zitto ambaye watu wakimkubusha wajibu yeye anadhani ni watu wanaomuonea husda kwa 'mafanikio' yake kisiasa, Zitto anayeamini moyoni na kichwani mwake kuwa yeye ni zaidi ya chama, lakini mdomoni anahubiri kuwa hakuna aliye zaidi ya chama.
Nimeandika si kwa mtiririko rasmi wa uandishi na utoaji habari, bali kwa mtindo wa kugusia gusia tu ili kukumbusha, kwa lengo la kuendelea kufikiri na kutafakari kwa pamoja.