Zitto kugombea urais 2015?

Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.
karibu jf mkuu
jamani naona vijana mnaendekeza ile issue ambayo wanaharakati wa cdm hatuitaki,hatutaki kuwa na watu maarufu zaid ya chama,hivyo msitake kuleta habari za kutafuta kuchonganisha viongozi wetu wa chama,kwani tunajua hata mbowe au slaa akitangulia mbele ya haki cdm itabaki hai tu,sio kama mnavyotaka wtu 3/2 wawe wao ndio kila kitu,je wasipohudhuria na vijana wa cdm wakapewa hoja hizo wazilete mikutanoni,hamtawapokea?....hata hivyo zitto nakuomba ukiwa na usikivu jitokeze sasa,kwanza ujue mitaani wamepoteza imani na wewe kwa kosa lako la kuropoka sana kwenye vyombo vya habari na hao wanafiki wanatumia nafasi hii kuchocgea chuki sana,
 
Nimekuwa nikimfuatilia huyu mpiganaji kwa karibu na nilishangazwa alivyoshindwa kuhudhuria walau ufunguzi wa maandamano ya kanda ya ziwa na kisha akarudi kumuuguza mama yake, Sasa kwa haya maandamano ya nyanda za juu kusini yatakayoanza mei 4 hatutaki akose. Mm nipo kati ya hiyo mikoa ya nyanda za juu kusini na nawasubiri viongozi wote wa kitaifa akiwemo na yeye.

kwa hiyo maandamano ni ya kulazimishana siyo? nilifikiri mtu anashiriki kutokana na kuvutiwa na agenda.
hahahahaa kuuza sura? au
 
mbona unatukana mjomba au kama huwezi jibu ni bora ukae kimya..heshimu mawazo ya watu..

Mwache atukane mmezidi udini,k2 kidogo uislamu mara mufti,mara askofu,mnaipeleka wapi nchi kwa udini?
 
lets wait Zitto atakuja na sababu zipi, mtu maana huyu naibu katibu mkuu wetu alway yupo mguu ndani mguu nje
keep in wait we shall see!
 
mufti asijisahau siasa unamhusu nini? hawa ndio wanaomponza JK, waonekane wanamtetea, watulie, arudishe kauli yake na akikataa poa, kusini hamna waislamu, amsaidie kwanza bosi wake gaddafi anaefanywa vibaya na DAVID na NICOLA, si aliaahidiwa msikiti wa gorofa shirin? ndio mana meitisha mandamano ya kumuunga mkono.
kazi rahisi kweli ukitaka kuonyesha ujinga wako
Ka
 
Kati ya vitu ambavyo CHADEMA wame-prove kuwa wapo makini ni namna ambavyo wameweza kum-handle Zitto, chama ndiyo kilimfikisha hapo alipo, umaarufu wake ulianza pale alipotolewa bungeni lakini CDM ikaamua kumbeba na kuunganisha watu ili ichukulie kitendo cha kufukuzwa bungeni na matokeoa ya ushujaa wake, na msimamo dhidi ya maslahi ya taifa, kweli watu wakjitokeza kwa wingi baada ili kuitikia wito wa chama.

Alipoona makutano ya watu kiasi kile akajua hii ni shauri ya yeye kama yeye kama Zitto na si chama, imani ikajengeka ndani yake kuwa yeye ni zaidi ya chama, akaanza kufuata utashi na hisia zake, kama treni iliyoacha reli...waandishi waliokuwa wanamsifia wakaona mwelekeo wake hatari, Kibanda akaandika kuonya, Ngurumo akaandika, Happiness Katabazi akaandika, wengi wakaandika, sikio la kufa halisikii dawa, magazeti makini yakaachana naye, akaenda kuibukia kwenye magazeti ya udaku, akayashambulia magazetu yetu kuwa, magazeti ya udaku ndiyo yenye nguvu na yasomwayo na watu wengi duniani, hakufafanua watu wa aina gani. Muda si mrefu urafiki na magazet hayo ukaisha baada ya kuandika skendo zake za ngono na wasichana kadhaa wanaodhani kuwa majina yao ni makubwa hapa nchini, kumbe yanafahamika tu na wala hayana ukubwa wowote.

Turudi kwenye mada...akazua hali ambayo ilitafsiriwa kama kizaazaa ndani ya CDM, nadhani alifanya makusudi ili afukuzwe aondoke "kishujaa"(kama alivyopokewa jangwani) kwasababu kuna watu ndani ya CCM walimdanganya kuwa akifukuzwa na hata akiipoteza nafasi ya ubunge, atapewa wa kuteuliwa na rais, pia kupewa unaibu waziri, na ili kumhakikishia hilo akajengewa ukaribu na idara za usalama na watu mashuhuri walio pretend kwenda kwake kupata ushauri na msaada wa mambo kadhaa, akazidi kuwa jeuri, lakini maskini kijana huyu hakujua kuwa watanzania walishamuona kimeo muda mrefu uliopita kiasi cha viongozi wa CDM kuwekwa katika msukosuko na wananachama wao kuwa kwa nini wanamlea, lakini uongozi ulionyesha ukomavu kwa kuendelea kuwa naye na kumkumbusha maadili ya chama na siasa kwa ujumla.

Kabla ya kampeni mwaka za mwaka jana, alitishia kutogombea, lakinibaadaye akapima akapima akaona namna maisha yatakavyokuwa magumu nje ya siasa, kwani hakuna kazi itakayomlipa kama siasa, ukichukulia kwa muda huo alishaamua kushiriki siasa kwa maslahi binafsi, hivyo akabatilisha msimamo wake na kuamua kutetea kiti chake, kampeni zilipowadia, akijua kuwa chama chake kimesimamisha mgombea wa nafasi ya urais, lakini akaonyesha kuibeza hatua hiyo kwa kusema kuwa, tunakwenda kuchagua wabunge na madiwani kwani rais tayari tunae tumuache amalize muda wake, lakini uongozi wa CDM uliendelea kumvumilia, Kitendo hicho cha uongozi wa CDM kuendelea kumvumilia kimebomoa sana Image ya Zitto kwa jamii,na kuifanya CDM ionekana kama chama imara kinachoweza kuishi pamoja hata inapotokea wakatofautiana mawazo kati yao.....kwa hili CDM nawapa sifa sana. Zitto amechuja lakini hilo halitambui tena kwasababu sasa hivi anaishi kwa kutegemea taarifa za wapambe. Ameaminishwa kuwa kila ampingae ni walewale wanaotumiwa dhidi yake.

Sasa hivi ni naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni anaongoza watu wasio mkubali watu ambao walipiga kura ya kumkataa, maamuzi ambayo hayakuwahi batilishwa popote pale, lakini kwasababu ya upenzi wake kwa madaraka bila kujari anaongoza kwa mazingira gani as long as anapata chake, katika hili Zitto hataki kutumia akili yake kama mwanasiasa kijana na msomi kama anavyotaka kutambulika, ameamua kung'ang'ania madaraka hayo bila suluhu ya aina yoyote, hataki kupisha nafasi hiyo kwa mtu mwingine anekubalika.

Zitto ambaye nahisi kila aonapo wakina Mnyika, Lema Lissu na wengineo wakitoa hoja zinazotikisa bunge huwa hajisikii vizuri kwa kuumia moyo, akitamani hali hiyo ya bunge kutetemeshwa kwa hoja ingesababishwa na yeye. alijaribu kutengeneza 'msukule/Zombi' wake pale bunge (Kafulila), lakini sijui ulipoishia, japo kuna yule bint, simkumbuki jina lake ila nadhani ni wa viti maalum CDM, lakini wote wapo off-color.

Huyo ndiye Zitto kabwe, ambaye sasa anataka atambulike kama rais mtarajiwa, kwani ameshatangaza dhamira yake ya kugombea urais mwaka 20015, Zitto ambaye watu wakimkubusha wajibu yeye anadhani ni watu wanaomuonea husda kwa 'mafanikio' yake kisiasa, Zitto anayeamini moyoni na kichwani mwake kuwa yeye ni zaidi ya chama, lakini mdomoni anahubiri kuwa hakuna aliye zaidi ya chama.

Nimeandika si kwa mtiririko rasmi wa uandishi na utoaji habari, bali kwa mtindo wa kugusia gusia tu ili kukumbusha, kwa lengo la kuendelea kufikiri na kutafakari kwa pamoja.
 
Kama Zitto ni mwelewa atarudi kwenye mstari. Ana nafasi kubwa ya kuwa PM hata rais lakini hatafikia lengo kwa njia anayofuata. Inabidi ajenge mazingira ya kukubalika ndani ya chama kwanza na aache mambo yanayotia shaka
 
kama zitto ni mwelewa atarudi kwenye mstari. ana nafasi kubwa ya kuwa pm hata rais lakini hatafikia lengo kwa njia anayofuata. inabidi ajenge mazingira ya kukubalika ndani ya chama kwanza na aache mambo yanayotia shaka
 
Hizo ni hisia zako lkn kamwe sitoziamini, ninavyoona mimi Zitto Kabwe ni mpigani shupavu. Na kuwa mbunge wa chama cha upinzani hakumaanishi usiwe na uhusiano wa karibu na wabunge au viongozi wa chama tawala.

Jamani vyama vingi visiwe sababu ya kuwaacha marafiki zetu au kutokukaribisha marafiki wapya. Imekuwa muda mrefu akishutumiwa mhe Zitto kuwa ni kibaraka wa chama tawala especially alipotaka kugombania nafasi ya uwenyekiti wa CHADEMA na hii ilikuwa ni haki yake kikatiba. Kwa hiyo kwangu mimi hizi zote ni njama za kumuondoa Zitto katika duru ya kisiasa. Na ndugu zangu siasa sio ugomvi siasa ni hoja.

Kwa hiyo Zitto kuwa na ukaribu na viongozi wa chama tawala sio kosa sisi hatupigani vita na CCM tunapambana nao kisiasa so hakuna sababu ya mwanachadema au kiongozi wa chadema kutokuwa na mawasiliano na viongozi wa CCM.

Jamani hapa kuna kitu nyuma yake na ikiwa huu ndio itakuwa mwenendo wetu hatutofika popote na tutake tusitake Zitto kama mzito ametoa msaada mkubwa sio tu ktk chama bali kwa taifa kwa ujumla na asiyejua ni mchango Zitto kautoa ktk chama na taifa kwa ujumla basi ni mbumbumbu.
 
ZItto ana matatizo lakini inaelekea ipo siku atatulia tu!!!
 
Zitto is a quality young leader ila nadhani he is rushing na hiyo ndoto yake ya urais ya 2015
 
Naona mmejipanga kumshambulia, kila siku ni hoja za kumvunja moyo.
Bila shaka kuna kundi limetumwa kumpika vita zitto. Nahisi ni janja yenye siri nzito nyuma yake.
Hakika kikulacho ki nguoni mwako.
Zitto usikate tamaa, pambana na adui zako ndani na nje ya chama.
Fitina kila sehemu- mnadhani zitawasaidia?
 
naona mmejipanga kumshambulia, kila siku ni hoja za kumvunja moyo.
Bila shaka kuna kundi limetumwa kumpika vita zitto. Nahisi ni janja yenye siri nzito nyuma yake.
Hakika kikulacho ki nguoni mwako.
Zitto usikate tamaa, pambana na adui zako ndani na nje ya chama.
Fitina kila sehemu- mnadhani zitawasaidia?

umeongea kweli ndugu huu ni mkakati ambao una mgongo wa vizito wa chadema nia yao kumuundosha zitto katika duru ya siasa lkn kamwe wakimuuondosha kwa hila yyte ile na wao wajichimbie kaburi lao
 
Kama kweli ana Ndoto ya urais 2015 basi hasahau,...dr. Slaa kama kawaida lazima asimame tena.
 
Zitto practices modern politics,siasa zinazo endana na dunia ya leo.tatizo wana CDM wengi wapo biased na wmekaa ki chama chama zaidi kuliko ku focus issues...hii kasumba ipo ccm pia,so its the same trend,mzimu huu unawakumba wana CDM bila ya wao kujua..

Mfano: Zitto alipogombea uenyekiti wa CHADEMA ...hapa ndo matatizo yalipo anza na Zitto kuonekana mtovu wa nidhamu,mroho wa madaraka,puppet,ametumwa na mafisadi.kila neno baya alipewa.

Ukweli ni kwamba alikua anatimiza wajibu wake kama mwana chama na kwa kua muda ulikua umefika wa uchaguzi, katiba na kanuni zina mruhusu kugombea alifanya hivyo...

Mbowe na wapambe wake wakati wa uchaguzi wakaleta hoja ya uchanga wa chama,mara chama kitagawanyika na kumshauri zitto ajitoe, yes alikubali. Kama matatizo ya kugawanyika chama na chama kua bado kichanga kuhimili vishido vya uchaguzi, kwanini MBOWE aliye liona tatizo hili mapema asinge jitoa yeye kumpisha Zitto?

Jamani kila siku Zitto, Zitto, Zitto mbona majungu mengi kwa huyu mtoto kuna nini? Hao malaika wenu mbona hamjawahi kuwaandika vibaya au hawana mapungufu kabisa?
 
Musembi,

Naona upo kazini, endelea kuwajibika uilishe familia yako!!

Lakini Zitto bado yupo vizuri sana, ata michango yake Bungeni sio ile ya almuradi naye kaongea kama wafanyavyo Wabunge walio wengi bali imejaa upeo na fikra pevu zinazoweka mbele maslahi ya Taifa kuliko vijikundi vidogovidogo vilivyoko Bungeni, dhahabu ni dhahabu tu!!
 
Zitto anayeamini moyoni na kichwani mwake kuwa yeye ni zaidi ya chama, lakini mdomoni anahubiri kuwa hakuna aliye zaidi ya chama.
Anayoyaamini moyoni na kichwani mwake umeyajuaje wewe?
 
Kama Zitto ni mwelewa atarudi kwenye mstari. Ana nafasi kubwa ya kuwa pm hata rais lakini hatafikia lengo kwa njia anayofuata. Inabidi ajenge mazingira ya kukubalika ndani ya chama kwanza na aache mambo yanayotia shaka
Alishajichanganya na huyu amesababisha watu wakamshtukia mapema wala asijaribu kugombea urais yeye abaki huko huko kwenye ubunge. Rais ndumila kuwili atairudisha nchi kwenye ukoloni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom