Zitto kugombea urais 2015?

Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.
Hv Zito Kabwe kushauriwa asigombee uenyekiti wa CDM ili kuepusha siasa za makundi na mgawanyiko ndani ya chama kutokana na wagombea wote F.Mbowe na Zito Kabwe kuwa na influence kubwa ndani ya chama. je maamuz haya yalikuwa ya busara au siasa ilibakwa?!!
Nyerere alitengua ushindi wa JAKAYA KIKWETE kugombea nafasi ya urais kupitia CCM na kupewa Ben Mkapa, je nyerere alibaka siasa au alifanya maamuz ya busara?!!
 
tutayasikia mengi na ndio kwanza 2011, ikifika 2014 nadhani mambo yotea yatakuwa hadharani wananchi waamue wenyewe! ila ukweli upo palepale hakuna asiyetamani kesho awe juu zaidi ya jana na leo!
 
Mijadala kama hii naiunga mkono. Ninaona katika hili mimi ninaunga mkono upande unaomshambulia Zitto. Zitto ameonyesha mifano mibaya kama kiongozi katika utendaji wake. Nitataja mifano michache:
1. Kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, 2010, alisema waziwazi kuwa atamwunga mkono ndugu Kafulila katika kugombea ubunge. Kama Zitto angelikuwa mwanachama wa kawaida katika CDM ningelaumu kiasi kidogo, lakini kama naibu katibu Mkuu wa CDM nilijiuliza inamaana CDM haitakuwa na mpango wa kusimamisha wagombea katika majimbo kama hilo atakalogombea Kafulila. Baadaye nilichoshuhudia ni kuwa Kafulila alipata ubunge kupitia NCCR - mageuzi pamoja na wengine kutoka NCCR. Je, jitiahada za Zitto zilikuwa wapi katika kuinadi CDM?

2. Wakati rais Kikwete anahutubia bunge la kumi mwaka jana wabunge wa CDM walitoka nje. Zitto ambaye hakuwepo siku ile bungeni alisema kuwa yeye anamheshimu sana rais kwa hivyo hakuona sababu ya kufanya kitendo kama kile. Swali ambalo sisi tusikuwa viongozi wa CDM wala wanachama wa CDM tulijiuliza kuwa msimamo wa Zitto ulikuwa na mantiki gani mbele wabunge wenzake? Na taarifa tulizopata baadaye ni kuwa uamuzi ule ni uamuzi ambao wabunge wa CDM waliujadili na kuupigia kura, kwanini Zitto aliupinga uamuzi ulioamuliwa Kidemokrasia?

3. Zitto alikuwa mstatari wa mbele kupiga kelele Dowans inunuliwe kitu ambacho hata baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wakilipinga. Leo tumeona Dowans ni nani. Hata katika hili bado kuna watu watamtetea Zitto?

Kwa mantiki ya kawaida hata kama mtu si mwanachama wa CDM atagundua kuwa Zitto anacheza ngoma tofauti na ile Wanachadema wanaicheza. Anafanya nini huko? Wengine wamechangia kuwa eti uhusiano wake na viongozi wa CCM na baadhi ya watu wa usalama wa Taifa hauna tatizo, ni aina gani ya uhusiano na unahusu nini? Je, uhusiano huo hauna athari ya yeye kutumiwa vibaya.

Zitto hata ukitetewa eti kwamba watu wanakuonea wivu bado ukweli unabaki pale pale kwamba mashaka yangu ni makubwa kuhusu Zitto wala simwamini kama mtu anayefaa kuwa kiongozi.
 
Put na good side of Zitto hapo itakuwa imebalance. how do u see?
 
Zitto is a quality young leader ila nadhani he is rushing na hiyo ndoto yake ya urais ya 2015

he is not rushing man, that is his destiny may be so he has to start early to march
 
Nimefuatilia maoni ya watu mbali mbali ktk mada hii lkn nimegundua kwamba kuna watu wanafikiri Zitto anaonewa, binafsi nasema sikweli.

Zitto amekuwa overconfidence mno, nilimpenda mwanasiasa huyu lkn inavyooneka hawezi kuwa kiongozi kwani anajiangalia yeye kama yeye. Yeye anatakiwa kuwa mtendaji, aagizwe fanya hili fanya lile basi. Kuongoza wengine kunahitaji hekima na busara vitu ambavyo kwa maoni yangu hana.

Ni vema atambue pamoja na viongozi wengine ndani ya CDM kwamba uimara wa chama chochote unatokana na collective responsibility na siyo Mwenyekiti anasema hivi, katibu jingine na mwingine anasema lake. Hii haina maana kwamba watakubaliana ktk kila jambo ila tu kwa ajili ya kulinda umoja thabiti katika masuala ya msingi.
 
kati ya vitu ambavyo chadema wame-prove kuwa wapo makini ni namna ambavyo wameweza kum-handle zitto, chama ndiyo kilimfikisha hapo alipo, umaarufu wake ulianza pale alipotolewa bungeni lakini cdm ikaamua kumbeba na kuunganisha watu ili ichukulie kitendo cha kufukuzwa bungeni na matokeoa ya ushujaa wake, na msimamo dhidi ya maslahi ya taifa, kweli watu wakjitokeza kwa wingi baada ili kuitikia wito wa chama.

Alipoona makutano ya watu kiasi kile akajua hii ni shauri ya yeye kama yeye kama zitto na si chama, imani ikajengeka ndani yake kuwa yeye ni zaidi ya chama, akaanza kufuata utashi na hisia zake, kama treni iliyoacha reli...waandishi waliokuwa wanamsifia wakaona mwelekeo wake hatari, kibanda akaandika kuonya, ngurumo akaandika, happiness katabazi akaandika, wengi wakaandika, sikio la kufa halisikii dawa, magazeti makini yakaachana naye, akaenda kuibukia kwenye magazeti ya udaku, akayashambulia magazetu yetu kuwa, magazeti ya udaku ndiyo yenye nguvu na yasomwayo na watu wengi duniani, hakufafanua watu wa aina gani. Muda si mrefu urafiki na magazet hayo ukaisha baada ya kuandika skendo zake za ngono na wasichana kadhaa wanaodhani kuwa majina yao ni makubwa hapa nchini, kumbe yanafahamika tu na wala hayana ukubwa wowote.

Turudi kwenye mada...akazua hali ambayo ilitafsiriwa kama kizaazaa ndani ya cdm, nadhani alifanya makusudi ili afukuzwe aondoke "kishujaa"(kama alivyopokewa jangwani) kwasababu kuna watu ndani ya ccm walimdanganya kuwa akifukuzwa na hata akiipoteza nafasi ya ubunge, atapewa wa kuteuliwa na rais, pia kupewa unaibu waziri, na ili kumhakikishia hilo akajengewa ukaribu na idara za usalama na watu mashuhuri walio pretend kwenda kwake kupata ushauri na msaada wa mambo kadhaa, akazidi kuwa jeuri, lakini maskini kijana huyu hakujua kuwa watanzania walishamuona kimeo muda mrefu uliopita kiasi cha viongozi wa cdm kuwekwa katika msukosuko na wananachama wao kuwa kwa nini wanamlea, lakini uongozi ulionyesha ukomavu kwa kuendelea kuwa naye na kumkumbusha maadili ya chama na siasa kwa ujumla.

Kabla ya kampeni mwaka za mwaka jana, alitishia kutogombea, lakinibaadaye akapima akapima akaona namna maisha yatakavyokuwa magumu nje ya siasa, kwani hakuna kazi itakayomlipa kama siasa, ukichukulia kwa muda huo alishaamua kushiriki siasa kwa maslahi binafsi, hivyo akabatilisha msimamo wake na kuamua kutetea kiti chake, kampeni zilipowadia, akijua kuwa chama chake kimesimamisha mgombea wa nafasi ya urais, lakini akaonyesha kuibeza hatua hiyo kwa kusema kuwa, tunakwenda kuchagua wabunge na madiwani kwani rais tayari tunae tumuache amalize muda wake, lakini uongozi wa cdm uliendelea kumvumilia, kitendo hicho cha uongozi wa cdm kuendelea kumvumilia kimebomoa sana image ya zitto kwa jamii,na kuifanya cdm ionekana kama chama imara kinachoweza kuishi pamoja hata inapotokea wakatofautiana mawazo kati yao.....kwa hili cdm nawapa sifa sana. Zitto amechuja lakini hilo halitambui tena kwasababu sasa hivi anaishi kwa kutegemea taarifa za wapambe. Ameaminishwa kuwa kila ampingae ni walewale wanaotumiwa dhidi yake.

Sasa hivi ni naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni anaongoza watu wasio mkubali watu ambao walipiga kura ya kumkataa, maamuzi ambayo hayakuwahi batilishwa popote pale, lakini kwasababu ya upenzi wake kwa madaraka bila kujari anaongoza kwa mazingira gani as long as anapata chake, katika hili zitto hataki kutumia akili yake kama mwanasiasa kijana na msomi kama anavyotaka kutambulika, ameamua kung'ang'ania madaraka hayo bila suluhu ya aina yoyote, hataki kupisha nafasi hiyo kwa mtu mwingine anekubalika.

Zitto ambaye nahisi kila aonapo wakina mnyika, lema lissu na wengineo wakitoa hoja zinazotikisa bunge huwa hajisikii vizuri kwa kuumia moyo, akitamani hali hiyo ya bunge kutetemeshwa kwa hoja ingesababishwa na yeye. Alijaribu kutengeneza 'msukule/zombi' wake pale bunge (kafulila), lakini sijui ulipoishia, japo kuna yule bint, simkumbuki jina lake ila nadhani ni wa viti maalum cdm, lakini wote wapo off-color.

Huyo ndiye zitto kabwe, ambaye sasa anataka atambulike kama rais mtarajiwa, kwani ameshatangaza dhamira yake ya kugombea urais mwaka 20015, zitto ambaye watu wakimkubusha wajibu yeye anadhani ni watu wanaomuonea husda kwa 'mafanikio' yake kisiasa, zitto anayeamini moyoni na kichwani mwake kuwa yeye ni zaidi ya chama, lakini mdomoni anahubiri kuwa hakuna aliye zaidi ya chama.

Nimeandika si kwa mtiririko rasmi wa uandishi na utoaji habari, bali kwa mtindo wa kugusia gusia tu ili kukumbusha, kwa lengo la kuendelea kufikiri na kutafakari kwa pamoja.

umetumia nguvu nyingi ya kuongea kwa kupindisha ukweli,kati ya wanasiasa ambao wapo tayari kukosana ata na familia yake kwenye maswala ya msingi ni zitto kabwe.viongozo wa chadema hawampendi kwasababu anazuia ufisadi na ni mtetezi wa watu wa naokandamizwa na chadema,hivi iyo hoja ya kununua magari ya mitumba kwani ni zitto pekeyake aliye ikataaa,mbona profesa beregu,,mnyika wamepinga kwanini zito, huoni kuna mkakati mzito hapa wa kumtafutia mingo ya kumtoa chadema ?hivi unafikiri chadema mkimfukuza zitto taswira yenu ya udini na ukaskaskazini mtaificha wapi? Zitto amefanya makubwa mangapi ambayo watanzania leo hii wanajivunia. Na uyo dr slaa kukaa kimya wakati watu wanakemea ufisadi na yeye kwanini asikemee na kuungana na zitto
 
kwaiyo nyerere akikosea na wewe unakosea,nyerere alikua anatembea na kifimbi mwambie nae freeman mbowe nae atembee na kifimbo wafuasi wa chadema hamna akili ya kuchambua mabo vizuri,
 
kwa kweli huyu kijana nimemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua ni miongoni mwa viongozi wa chache ambao wana nia ya dhati ya kuwakombania wananchi wa nchi hii ya Tanzania

pia ni kijana mwenye maono na uwezo wa kujenga hoja, ni mtu mwenye kujiamini na kuwa tayari kuusimamia na kuutetea msimamo wake

ni mtu asiendeshwa na emotion kama viongozi wengine, ni kiongozi pekee karibu vyama vyote vya siasa na wasiokuwa na vyama wanamuheshimu na kumpenda

kwa kweli zitto anafaa kuwa mgombea wa chadema 2015
 
Sikutaka kuongea lolote tena kuhusu Zitto ila nimeshindwa kuvumilia. Zitto amebaki ni shati tu na siasa kugombea uraisi ni ndoto zenu msiejua siasa na mkifikiri cdm ni kama ujinga wa ccm. Atakae mpigia kura za kumpitisha kwenye hii nafasi ya cdm ni nani? cdm hatutaki watu wanafki na kuwepo kwa Zitto ndani ya cdm mpaka leo ni bado tunamchuza tabia zake na siku yeyote Zitto atakuwa TLP au NCCR.

Zitto kwa maneno ya huku na kule ni sawa na Nape CCJ. Kilichomweka Zitto cdm mpaka sasa ni njaa ya uongozi na dream yake ya kutaka kupanda kiharaka haraka. Ofisi ya raisi Tanzania haitaji mtu anayetumiwa na chama kingine kuwaua wananchi hata mara moja. Haya mambo yamefanyika sana ccm na angalia Taifa lilipo. Tumeendelea kupata viongozi wenye njaa na wezi kupindukia, hivyo Zitto ana-fit hii category kabisa. Wananchi tunajua tutamkamata Zitto tu katika hizi harakati za njaa zake na tutamshuhurikia. Kwa kifupi Zitto alishapoteza influence yake ktka siasa cdm na kitaifa
 
kwa kweli huyu kijana nimemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua ni miongoni mwa viongozi wa chache ambao wana nia ya dhati ya kuwakombania wananchi wa nchi hii ya Tanzania

pia ni kijana mwenye maono na uwezo wa kujenga hoja, ni mtu mwenye kujiamini na kuwa tayari kuusimamia na kuutetea msimamo wake

ni mtu asiendeshwa na emotion kama viongozi wengine, ni kiongozi pekee karibu vyama vyote vya siasa na wasiokuwa na vyama wanamuheshimu na kumpenda

kwa kweli zitto anafaa kuwa mgombea wa chadema 2015

Peleka huko tambala lako bovu la deki hivi mnafikiri CDM ni sawa na CCM.
 
Hivi Watz tumerogwa? Badala ya kudeal na matatizo yetu ya sasa tumeanza kuwaza urais 2015 hebu tuache uwendawazimu. Tusicheze ngoma ya viongozi wenye uchu wa madaraka hii ni hatari sana, hebu tusolve matatizo yetu kwa sasa urais tuanza kuwaza huko 2013, no wonder huu mtanange wa urais 2015 ndo unaoipasua CCM
 
kwa kweli huyu kijana nimemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua ni miongoni mwa viongozi wa chache ambao wana nia ya dhati ya kuwakombania wananchi wa nchi hii ya Tanzania

pia ni kijana mwenye maono na uwezo wa kujenga hoja, ni mtu mwenye kujiamini na kuwa tayari kuusimamia na kuutetea msimamo wake

ni mtu asiendeshwa na emotion kama viongozi wengine, ni kiongozi pekee karibu vyama vyote vya siasa na wasiokuwa na vyama wanamuheshimu na kumpenda

kwa kweli zitto anafaa kuwa mgombea wa chadema 2015

Unaongea vitu gani wewe?Zito huyuhuyu alietutosa bungeni juzi na kuanza kuwasiliana na Rostam,hata km alifanya vile kwa utashi na busara hakuwa na sababu ya kuwa karibu na mtuhumiwa namba moja wa ufisadi!Zito bado haaminiki na anahitaji kuthibitisha msimamo na uzalendo wake kwa vitendo!kwa 2015 bado kipimo hakimtoshi!Bado tunaamini Slaa anaweza kuongoza nchi hii!Ushauri wa bure ni kuwa thread km hii inaleta chokochoko mwishowe tuanze mvurugano mapema,hebu kwanza tumwache zito afanye kazi zake halafu ikifika 2014 tuanze kujadili Urais wa 2015!
 
kwa kweli zitto ndani ya chadema ni kiongozi pekee ambaye hajachafuka. zitto ni kiongozi ambae haendeshi siasa za maji taka, au kutaka popularity, maana yeye tayari popular.

hata juzi nilisikiliza kwa umakini akizungumzia kuhusu bajeti mbadala nimemkubali

zitto hawezi kufanana na slaa ambaye, yeye hulishwa data na kuropokwa bila kufanya upembuzi yakinifu

sisahau slaa alivyomwita kiongozi mwenziwe kuwa ati sisimizi. zitto hana tabia ya kuwadharau viongozi wenziwe hata wanapotafautiana kimsimamo

zitto alijiunga na chama sio kwa njaa bali kwa imani na msimamo wake juu ya taifa lake.
 
kwa kweli huyu kijana nimemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua ni miongoni mwa viongozi wa chache ambao wana nia ya dhati ya kuwakombania wananchi wa nchi hii ya Tanzania

pia ni kijana mwenye maono na uwezo wa kujenga hoja, ni mtu mwenye kujiamini na kuwa tayari kuusimamia na kuutetea msimamo wake

ni mtu asiendeshwa na emotion kama viongozi wengine, ni kiongozi pekee karibu vyama vyote vya siasa na wasiokuwa na vyama wanamuheshimu na kumpenda

kwa kweli zitto anafaa kuwa mgombea wa chadema 2015

CHADEMA has many CREDIBLE people to run for presidency, ZITO is the list if not completely out!!! kwa kigezo kimoja tu cha CREDIBILTY.
 
kwa kweli zitto ndani ya chadema ni kiongozi pekee ambaye hajachafuka. zitto ni kiongozi ambae haendeshi siasa za maji taka, au kutaka popularity, maana yeye tayari popular.

hata juzi nilisikiliza kwa umakini akizungumzia kuhusu bajeti mbadala nimemkubali

zitto hawezi kufanana na slaa ambaye, yeye hulishwa data na kuropokwa bila kufanya upembuzi yakinifu

sisahau slaa alivyomwita kiongozi mwenziwe kuwa ati sisimizi. zitto hana tabia ya kuwadharau viongozi wenziwe hata wanapotafautiana kimsimamo

zitto alijiunga na chama sio kwa njaa bali kwa imani na msimamo wake juu ya taifa lake.
KAFU wameshindwa ndoa, hawapati tendo la ndoa ndani sasa wanatafuta mabwana wa nje!!

Kweli upumbavu hauna ujazo!!
 
Hivi Watz tumerogwa? Badala ya kudeal na matatizo yetu ya sasa tumeanza kuwaza urais 2015 hebu tuache uwendawazimu. Tusicheze ngoma ya viongozi wenye uchu wa madaraka hii ni hatari sana, hebu tusolve matatizo yetu kwa sasa urais tuanza kuwaza huko 2013, no wonder huu mtanange wa urais 2015 ndo unaoipasua CCM
Yamewashinda kwao sasa wanahangaika na vya watu............ HAWA NDIO WALE TUNAOOMBA MATUSI YARUHUSIWE TUWAFANANISHE NA NANIHII
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom