Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Kiongozi mwenye dhamira njema, kabla ya sheria, anazingatia katiba. Mtu mwovu kama alivyokuwa marehemu, wakati wote anatafuta mwanya utakaomwezesha kutenda uovu.

Magufuli alimwondoa Asad baada ya report yake iliyoonesha utawala wa Magufuli ulikuwa amepora 2.4 trillion. Hiyo pesa mpaka leo haijawekwa wazi ilikopelekwa japo kuna tetesi zenye nguvu zinazoeleza kuwa alienda kuzificha Canada, akitumia mwanya wa kununua ndege.
Hivi kati ya sheria na dhamira kipi kifuate? na kwani Katiba sio sheria?

Huwa naona "emotions" zinatawala sana vichwa vyenu popote akihusishwa, au kutajwa jina la Magufuli.
 
Umeelewa lakini? Kilichopo ni mgongano kati ya Sheria na Katiba! Katiba inatamka kuwa mkaguzi mkuu atatumikia mpaka afikishe miaka 60 ndipo astaafu lakini sheria ya ukaguzi inatoa mwanya kuwa mkaguzi mkuu atakuwa na vipindi viwili vya utumishi katika kiti chake, yaani miaka 5 ya kwanza then ikimpendeza Rais atamteua tena, kwaiyo Magufuli aliutumia mwanya wa sheria ambayo inafafanunua Katiba, wakati uo Zitto alienda Mahamani kupinga kifungu hicho cha Sheria na kwa mujibu wa Sheria zetu, sheria yoyote inayokinzana na Katiba basi kifungu hicho ni batili.

Sheria za namna hii tunazonyingi sana katika Taifa letu! Ata lile la Ndugai kulazimishwa kujiuzulu ni sawa tu na ili la Assad sapo wanaoamua wanaangalia upepo kuwa sasahivi Magufuli hayupo basi hakuna cha kuhofia, ila now Samia yupo ndiye alitefanya Ndugai atoke basi ili haliwezi kukubaliwa kule!
Unaweza sema bora Magufuli alitumia mwanya wa kisheria kukinzana na Katiba ila Samia hakutumia lolote kwa Ndugai zaidi ya power aliyonayo.
Kwa mujibu wa barua ya kujiuzulu Ndugai ni kwamba alijiuzulu kwa hiari yake mwenyewe, hakulazimishwa na mtu.
 
Kwani hilo na yule aliemuandikia Barua Ndugai ajiuzulu yana tofauti gani? Si yaleyale tu? Ata kwenye vyaka vyetu yapo, sawa tu na kufukuzwa kwa kina Prof Kitila Mkumbo. Kama ni hivi tuna vichaa wengi sana.
La Ndugai nenda Mahakamani na wewe kama Zitto Kabwe. Acha kulialia hapa msukule wa Magufuli sukuma gang wahedi.
 
Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha. Bila katiba mpya tena kwa njia ya machafuko, tusitegemee hatua zozote kuchukuliwa kwa hawa walevi wa madaraka.
Cc: UHURU JR

Shida ni kwamba, wanaoitaji katiba mpya ni Olmsted 2% ya watanzania wote

So utapambana kuongea mambo ya katiba mpya and hakuna mtu atakuelewa

As long as mtu mambo yake yanaenda sawa, no problem

Hata katiba ya sasa ni watu wachache ndio wanaijua
 
Zitto na genge lake Udini unawasumbua sana. Acheni siasa za kupambana na Ukristo pimbi nyie
Sasa udini Upo wapi hapo?? Hii nchi Ngumu sana, Wewe ndio mdini mkubwa kabisa. Avoid hatred to the Muslims, Hii ni nchi yetu sote
 
Magufuli aliamua kutoongeza mkataba wa Asaad. Sheria ilimruhusu kufanya hayo. Leo mahakama inasema ile sheria inapingana na katiba. Sheria yenyewe iliwekwa kabla Magufuli hajawa rais wa JMT. Sasa hapo Magufuli ana kosa gani?
Unajua sheria husika inasemaje?!

Mwanya ulikuwepo kwenye Katiba na SIO SHERIA. Hata hivyo. huo mwanya wa kwenye katiba ukasiribwa na katiba hiyo hiyo kwa kusema "...ama umri mwingine utakaotajwa na sheria"!

Sheria ikataja miaka 65 unless kama CAG anafanya kosa linalohitaji kuhundiwa tume!

Katiba ilitoa mwanya kidogo kwa sababu ilisema CAG atahudumu miaka 5 na anastahili kuongezewa miaka mingine 5. Aidha, ataendelea kubaki ofisini hadi atakapofikisha miaka 60 au kama itakavyotajwa na sheria zingine.
 
Mwanzo mzuri kwa Zitto, hongera kwake. Lakini namshauri asiishie hapo, kama kweli anajiona amekuwa mtetezi wa Katiba basi namtaka kesho arudi tena mahakamani kumfungulia Samia kesi yake kwa kupinga kwake kufanyika mikutano ya siasa kinyume cha Katiba.

Akifanya hivi ndio nitakuwa na imani nae, kinyume na hapo ameamua kujikosha tu kwa kumtumia Magufuli kwa manufaa yake kisiasa, sitachelewa kumuita mnafiki.
Usimpangie Zitto Kabwe kesi ya kufungua Mahakama Kuu. Mahakama ni haki ya kila Mtanzania kupata haki. Kwa vile wewe denooJ umeona mapungufu, nakushauri uende Mahakamani hata kesho ukaombe tafsiri hiyo.

Kwa taarifa yako hii ni kesi ya mwaka 2020 wala haijafunguliwa kipindi cha Samia akiwa Rais
 
Kimsingi, nasema kimsingi kama shauri lilianza wakati wa uhai wa yeyote ni lazima liishe hata kama mhusika hayupo au katangulia mbele zahaki, haijalishi.
Sasa kama mahakama imeona hivyo isisahau kumtendea Hassadi haki kama anavyostahili, ili idhihirishe nguvu yake kisheria na kikatiba.
Nachangia hoja.
 
Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha. Bila katiba mpya tena kwa njia ya machafuko, tusitegemee hatua zozote kuchukuliwa kwa hawa walevi wa madaraka.
Cc: UHURU JR
Magufuli alikosea katika hili ila kilichotokea hapa ni unafki tu ni muendelezo wa vita dhidi ya marehemu, wale wenye chuki na Magufuli kwao hii ni habari inayowafurahisha sana ila hakuna jipya.
 
Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
So what......? Genge la wachumia tumbo lipo front line kwa sasa..... It is very known..... Kazi njema
 
Magufuli alikosea katika hili ila kilichotokea hapa ni unafki tu ni muendelezo wa vita dhidi ya marehemu, wale wenye chuki na Magufuli kwao hii ni habari inayowafurahisha sana ila hakuna jipya.
Chuki tena?!

Yaani upande mmoja unakiri kwamba "alikosea", lakini upande mwingine unadai mwendelezo wa chuki!

Sasa ulitaka kesi ingetupwa wakati ilishafunguliwa, ama?!

Na ingetupwa vp wakati kesi ilikuwa ni dhidi ya RAIS WA JAMHURI?!

Hivi huoni maamuzi ya hiyo kesi yanatoa mwongozo kwa marais watakaofuata na huyu aliye madarakani?!
 
Back
Top Bottom