Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Ameandika Zitto Kabwe:
"Mahakama Kuu imetoa hukumu kuwa Rais wa Tanzania anaweza kushtakiwa kwa makosa ya uvunjaji wa Katiba. Jaji Lameck Mlacha ametoa hukumu hiyo katika hukumu ndogo kwenye shauri nililofungua kumshtaki Rais @MagufuliJP kwa kumvua uCAG Prof. Assad. Shauri la msingi linaendelea"-Zitto Kabwe.
====
Leo Machi 18, 2020, Mahakama Kuu Nchini imeeleza kuwa Rais wa Tanzania anaweza kushtakiwa kwa makosa ya uvunjaji wa Katiba
Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama hiyo ametoa hukumu hiyo katika hukumu ndogo kwenye shauri lililofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe dhidi ya Rais Magufuli
Zitto alifungua shauri Mahakamani hapo akidai Rais Magufuli alivunja Katiba baada ya kumteua Charles Kichere kuwa CAG akichukua nafasi ya Prof. Mussa Assad
Katika shauri hilo ambapo Zitto anadai CAG haondolewi kwenye nafasi hiyo mpaka astaafu, Serikali ilipeleka mapingamizi sita ambapo leo Mahakama imeyakataa. Shauri la msingi linaendelea