benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe
"Azimio sio Mkataba wa uendeshaji (concession agreement) wala sio Mkataba wa Uwekezaji (HGA). Azimio la Bunge ni ruhusa tu ya kuanza kujadiliana hiyo mikataba mingine. Azimio hili litakufa kibudu pasipokuwa na makubaliano yatakayofikiwa ndani ya miezi 12. Tunaweza kuboresha na kufaidika iwapo tukiamua. Tazama A GLASS HALF FULL sio A GLASS HALF EMPTY"
"Kampuni ya uendeshaji wa Bandari itakayoundwa Kwa Mujibu wa Makubaliano ya Tanzania na Dubai imilikiwe Sawa kwa Sawa kati ya DP World na TPA. Wao wana Fedha na teknolojia, Sisi tuna Bandari. Tuunde 50-50 JV. Tukijenga uwezo wetu wa ndani tutaweza kuwanunua na tukawa 100%. Tulifanya hivyo Uwanja wa KIA. Pale KIA tulikodisha kwa Kampuni ya Afrika Kusini na Uingereza. Baadaye Serikali ikachukua Hisa na hatimaye KADCO sasa inamilikiwa na Serikali. Uendeshaji wa Huduma za Bandari ( operatorship ) unaweza kufanywa na Sekta Binafsi (rejea msimamo wa kisera wa ACT Wazalendo ktk picha ). Mamlaka ya Bandari kisheria ni LANDLORD. Njia sahihi kwa Bandari ya Dar ni Kampuni ya Uendeshaji kumilikiwa 50-50 kati ya TPA na Mwekezaji!"
"Tunaweza kujadiliana kwa staha. Huna sababu kuhamaki na kuita Watu majina mabaya. Kilichopitishwa na Bunge ni Azimio ya Ushirikiano baina ya Nchi Mbili ambalo lisipotekelezwa kwa miezi 12 litajifia. Azimio lina matobo mengi ambayo ni muhimu yazibwe kwa Serikali yetu kutaka ‘addendums’. Jambo muhimu na kubwa ni kuwa kuna Mkataba wa Uwekezaji (HGA) Hata majadiliano bado na huu ndio haswa utakaoamua aina ya Uwekezaji utakaofanyika. Huo Ndio utaunda Kampuni hapa nchini ambayo Ndio itaingia hayo makubaliano ya kuendesha Bandari. Hapo ndipo tunapaswa kutaka umiliki Sawa wa Kampuni hiyo ya uendeshaji. Ni muhimu Sana katika masuala mazito kama haya kutofautisha UKWELI na HISIA. Feelings Hata Mbwa anazo. Mwanadamu anafanya maamuzi kwa kutazama FACTS. Hata hivyo, ninatambua, ninaelewa na ninathamini FEELINGS zako na za wengine katika jambo hili. Bahati mbaya Mie sio mtu anayetazama mambo kwa hisia bali natazama mambo kwa ukweli."