Zitto Awe Mbaya Wana Kigoma Wawe Wazuri!

Zitto Awe Mbaya Wana Kigoma Wawe Wazuri!

Hivi inaingia akilini? Zitto Kabwe awe mbaya lakini waliomchaguwa kuwatumikia, ambao ni wapiga kura wake, wana Kigoma wawe wazuri?

Ni wazi kabisa, kama mnamkataa Zitto ndio mmewakataa waliomchaguwa, na wao hamuwataki na msitake kuwahadaa wana Kigoma.

Hakuna shutuma hata moja tuliyoiona kuwa Zitto ameisaliti chadema. Waionyeshe hapa. Ni uongo tu walioupika kwa Zitto kuelezea nia yake ya kutaka kugombea Uenyekiti wa Chadema, hakuna zaidi.

Wana Kigoma msichotwe akili zenu na wachache hawa wenye chuki binafsi kwa mafanikio ya mwanenu. Msikubali kabisa, amma wamrudishie hadhi yake Zitto amma wamfukuze, kwa maana hiyo wanawafukuza nyie mliomchaguwa Zitto kuwatumikia. Wasikae wakamwacha kama mwanachama tu ilimradi abaki kuwepo bungeni wapate kula ruzuku ya uwepo wake bungeni.

Amma wamfukuze uanachama amma wamuombe radhi na wawaombe radhi wana Kigoma mliomchaguwa.

Wakumbuke kuwa Zitto hakuchaguliwa na Kamati ya Mbowe, Zitto alichaguliwa na wapiga kura wake, ambao ni ninyi Wana Kigoma.

Hiki ni kisa cha "baniani mbaya kiatu chake dawa" X 2. Mara moja ya ruzuku na mara ya pili ni Wana Kigoma.

Kigoma Oyeeeeeeeeeeee! Zitto Oyeeeeeeeeeeeee!
Kwa hiyo Zitto anawakilisha tabia za watu wa Kigoma?
 
Last edited by a moderator:


Ni kwanini WAHA na WABEMBE wakawa na hasira na CHADEMA ? Au ni wewe unataka kuweka UKABILA hapo kuonyesha CHUKI uliyonayo MOYONI MWAKO ?

Yeye sio wa kwanza kuna na matatizo kwenye chama hicho; Ni kwanini yeye ndie atakayeleta MAKABILA ya WAHA na WABEMBE wachukie? Mbona AMANI KAROBOU(excuse me the last name spelling) kulikuwa hakuna Makabila yaliyokuwa na HASIRA… kwanini sasa ? Una UHAKIKA au ndio wewe Unayetaka hayo YATOKEE na kwenda kuamasisha ETHNIC CLENSING ??? IS THIS JUST BECAUSE OF POLITICS ?

Sasa inakuwa ni THREAT AGAINST HUMANITY… Kweli tutafika????

Uyo Ritz ni bogas kabisa. Ni mchochezi wa kuogopa kama ukoma.
 
Sijasoma uzi wako, ila haya ndo nayaona: Una maana ZZK ndo kigoma? Nia yako uchochezi na ubaguzi. Hayo mnatafuta pakutokea but won't help you.
 
Kwa mantiki hii unataka kuniambia Wanakigoma wapo kwa ajili ya Zitto na sio Chadema?So unataka kuniambia kama Zitto akifa kesho na wana Kigoma wafe nao au wahamie Chama chengine?Hivi Watanzania tuna akili kweli yaani mtu ati yupo kwa ajili ya mtu flani teh teh mie ni siko kwa ajili ya mtu mmoja mmoja nipo kwa ajili ya Chama na kama niliyemchagua akienda kinyume na utaratibu nitakubaliana na chombo kilichomhukumu kwa kuwa ni chombo ninachokiamini kwani mie niko kwa Chama na siko kwa mtu moja mmoja.Kama Watanzania tunakataa kuleana tutafika mbali tukumbuke tupo hapa kwa ajili ya serikali hii inayoongozwa na chama cha CCM na kwa UDHAIFU wao na kulindana ati kuoneana aibu ndio maana nchi inadidimia kama CCM kunzaia miaka ya 1990 wangechukua maamuzi magumu leo hii tungekuwa mbali sana hata katika shughuli za kimaendeleo hatuwezi kuingiza siasa.Wenzetu Kenya juzi walizindua ujenzi wa Reli mpyaa tena ya kisasa zaidi kama zile za Ulaya lakini huku kwentu viongozi wa serikali wamakalia vikao kwa nini Zitto afukuzwe Chadema hivi kwani akifukuzwa si ndio ingekuwa poa kwenu Maccm kwani nyie nyie si ndio mlisema Chadema kitakufa soon sasa badala ya kulalamika na kusema kwa nini Zitto kafukuzwa so mngeshangilia na kumkaribisha Zitto CCM ili mkiuwe kwa uzuri zaidi lakini cha ajabu kila uchao mnatoa mapovu.Shame on you Maccm.Na lazima Zitto Zuberi Kabwe afukuzwe kama kweli alikuwa mtetezi wa wanaKigoma leo hii Halmashauri ya Kigoma ingeongozwa na Meya kutoka Chadema na Madiwani wote wangetoka Chadema kwa miaka yote aliyokuwa Mbunge lakini aibu yake ana Diwani mmoja tu so what.

Tanzania hakichaguliwi chama anachaguliwa mgombea. Kumbukua hilo.

Shibuda waliomchaguwa wote ni Chadema?
Zitto waliomchaguwa wote ni chadema?
Kikwete walimchaguwa wote ni CCM?

Wasome wana Kigoa hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...usalama-wa-slaa-wajadiliwa-4.html#post7979156
 
Tanzania hakichaguliwi chama anachaguliwa mgombea. Si wote waliomchaguwa Zitto ni chadema, si wote waliomchaguwa Kikwete ni CCM. Kumbuka hilo.

Kwani CHADEMA imemvua ubunge? Au wana Kigoma ndio waliompa unaibu katibu mkuu? Mzee mwenzangu naona unazidi kuniacha kwa uzee.......
 
Kwa hiyo CCM nayo imewakataa wapiga kura wa Jimbo la Kiembe Samaki-ZNZ?CCM haitashiriki uchaguzi huo?

What a narrow mind from a lady regarded as one of JF's politics guru analyst?

What a pity!

CCM imemfukuza kabisaaaa kwenye chama, au hilo hulijui, halikumuacha, Nyinyi kinachowashinda kumfukuza hadi hii leo ni nini? au mnangoja siku 14? hazijafika tu?
 
Ngoja Dr.W.Slaa akakutane na waha na wabembe walivyokuwa na hasira na Chadema.

Huijui Kigoma utakuwa unaiskia tu! Kigoma kuna wanachama wa CDM na si wafuasi wa mtu.Kumbuka Dr Slaa alipata kura nyingi kuliko hata alizopata zitto katika ubunge wake.
 
Last edited by a moderator:
didnt see udini kwenye hoja, if i knew, i would have:bored: bothered

Tuhuma 11 alizotuhumiwa Zitto hujazisoma? ngapi mule zinaongelea "udini"? au mkuki kwa nguruwe tu? au udini wa Zitto mule ulimaanishwa kuwa Zitto ni Mkatoliki?
 
Last edited by a moderator:
Yeah kuna watu ambao wanapenda NEGATIVITY for the sake of their survival… Sidhani kuwa na CHUKI kwa baadhi ya wapinzani kutasaidia chohote

Kitu kinachotakiwa ni kutokukimbilia matabaka ambayo yapo na hayajatudhuri Nchini Mwetu kama Majirani zetu

Hiyo ya kufitinishiana labda sio sababu kwasababu wewe unataka kuongea ulichonacho cha kuchonganisha...

Siasa sio lelemama… na ukishafikia Uwezo fulani kwahiyo unakuwa tayari kugombea URAIS; Vyama vingi duniani havina mchecheto wa uongozi kama Tanzania wa kuhudhuria hiyo MIKUTANO ya VYAMA na kuwa na KADI za uanachama

Umesoma tuhuma 11 alizotuhumiwa Zitto? ngapi zinaongelea udini? au udini sio tabaka?
 
Last edited by a moderator:
we vipi?unaumwa?kwani Lowasa alivyowajibika/wajibishwa na bunge inamaana Bunge na Serikali waliwachukia wanaMONDULI?Halafu mimi sio chadema wala ccm,ila waacheni cdm washughulikie matatizo yao.mnashabikia shabikia nini?SHUGHULIKIENI Maji,elimu,zahanati,umeme,viwanda,Ajira,ufisadi,sera nzuri ya gesi,madini,madawa ya kulevya,meno ya tembo n.k. kmvp sindikeni mananasi na maembe yanaanza kuwaozea wakulima.SIO MNASHOBOKA NA MIGOGORO YA CDM,FANYENI YENU.Halafu nyie ndo tumewachoka mnoooo...mnaboa sana,kazi kulindana na kuchezea rasilimali zetu.

Lowasa alijiuzulu mwenyewe hakuwajibishwa na mtu. Kumbuka hilo. Na ndiyo anakuja kwa kazi sana kuelekea 2015, Kumbuka na hilo pia.

Umezisoma tuhuma 11 alizotuhumiwa Zitto? ni ngapi zinaongelea udini? na udini wa Zitto ni upi? Ukatoliki?
 
Huwa najiuliza hasa kwanini hawa Maccm hawayaoni yao, wamemvua Mh Mansoory Uwaziri, na baadae wamemfukuza, watuambie alifanya kosa gani? lakin tumewaachia hatukusema kitu na watu waliendelea na shughuli zao kama kawaida. CCM njama zenu zimejulikana mulikua munamshawishi zito akamate nafasi ya uenyekiti baadae akihujumu chama, hizi zenu ni mbinu za kitoto wenye akili wameshtuka.
 
Muda mwingine huwa nakaa na kutafakari kisha kujiuliza, hivi jf imenisaidia nini tangu nijiunge enzi hizo ikiitwa jambofoum?

Jibu huja tena haraka sana, imenifanya kuwa mtu mwenye fikra chanya na kujua hitaji la taifa langu Tanzania,

Lakini ukija kwa baadha ya watu humu ambao nafahamu fika ni wakongwe kama FaizaFoxy, Ritz, ZeMarpolo, na wengine, unajiuliza sana, hivi jf imewasaudia nini kuwepo kwao hapa jf? Jibu linakuja haraka kuwa wameharibikiwa akili na wanaishi kwa kuongozwa na ukubwa wa matumbo yao,
 
Hebu tuambie na sisi wananchi wa huku Zanzibar Kiembe samaki, Mh wetu Mansoory amefukuzwa kabisa na Maccm? na bado tunaimani nayo itakuaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom