Kitabu cha Wangwe chaanika ukweli tunaotakiwa kuujua

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Wakuu wakati tukishuhudia ukiukwaji wa demokrasia ndani ya Chadema kwa kile kinachoitwa wazee wa chama wakiongozwa na Baba Mkwe wa Mbowe kumshinikiza Mh. Zitto kujitoa au la wamtoe kwa lazima katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Mwenyekiti wa Chama hicho nimeweza kupata nakala ya kitabu cha historia ya Hayati Chacha Wangwe na kwa haraka nimeweza andika sura ya saba ya kitabu hicho inayoitwa 'MKAKATI WAKE KUIJENGA CHADEMA' ili tuweze kuidadavua na kuijadili (kama kuna makosa ya uchapaji ujue ni kwa sababu ya uharaka na sikuwa na muda mwingi wa editing ). Naiweka hapa chini.

Waweza wasiliana na Jamaa kwa namba 0763632008 kupata nakala halisi.


SURA YA SABA: MKAKATI WAKE KUIJENGA CHADEMA
Unapozungumzia masuala ya chama cha siasa lazima uzingatie misingi na kanuni za uwepo wake na kuainisha nini chama hicho kinasimamia ili kama watu wana shauku ya kujiunga na kuendeleza harakati kupitia chama hicho wasiwe wajinga bali wawe na uelewa wa juu kuhusu malengo ya chama na mtindo wa uendeshaji wa chama.

Kama chama kitashindwa kutimiza matarajio ya wanachama wake ambao ndio washika dau namba moja kitakuwa kinajiweka katika hatari ya kutoweka kama washika dau watafarakana kwa kutofautiana katika mambo ya kadha wa kadha.
Kwa kujua hayo, Kamanda Wangwe alijizatiti na kuwa kiongozi mwenye hisia sana juu ya ni nini watu walio chini yake wanataka. Mara nyingi amekuwa akitofautiana na viongozi wa ngazi za juu hata serikalini lakini hajawahi kukosana na watu walio chini yake kwa sababu mara nyingi alijitahidi kuwa msikivu na kufanya waliyotaka.

Akiwa Mbunge wa Tarime, mara kadhaa amekuwa akiwauliza wanachi wanataka nini, kama ni kufukia makorongo wangeongozana moja kwa moja na kwenda kufanya kazi hiyo. Kwa sababu hiyo wananchi walimuona ni kiongozi wa watu na siku zote walimpenda na kumpa ushirikiano.

Katika historia ya maisha yake na harakati za kisiasa, chama alichofanya nacho siasa kwa muda mrefu ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hivyo aliona CHADEMA kama mlezi wake wa kisiasa na kujitoa kwa dhati katika kushirikiana na kutoa nguvu zake katika kujenga chama imara.

Kimsingi vyama vya upinzani vina jukumu kubwa sana katika kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji, utawala bora, na demokrasia katika nchi. Hivyo kuna viwango na vigezo ambavyo vyama hivyo vinapaswa kufikia ili viweze kutimiza wajibu wao.

Katika nchi yetu ya Tanzania mara nyingi viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiwalaumu watanzania kwa kuwa wagumu katika kuvipokea na kujiunga na vyama vya upinzani. Na mara nyingi zaidi wasomi ndio wanaoongoza kwa kutojiunga na vyama hivi.

Mara kadhaa watu wamewalaumu wasomi kwa kutojiunga na vyama hivyo na kujenga ushindani na chama tawala, na mwishowe kuhitimisha kwa kuwalaumu wasomi kuwa wanatanguliza maslahi yao binafsi na ndio maana hawapendi kujiunga na harakati za upinzani.

Awali hata mimi niliwalaumu wasomi na watu wote kwa ujumla kwa kutojiunga na harakati. Lakini baada ya muda na kwa kukaa na kufanya uchambuzi mzuri niligungua ya kwamba watu hawa hawapasi kupuuzwa bali kuna haja ya kufanya utafiti wa kina ili kubainisha ni nini chanzo cha yote hayo.

Baada ya kutafakari na kufanya utafiti wa kina niligunudua kuna matatizo mengi sana ambayo yanafanya watanzania wengi wawe wagumu katika kufanya maamuzi ya kuukabidhi upinzani jukumu la kuiongoza nchi, kwani watanzania wanaonekana kuwa ni watu watulivu na wenye kutazama mambo kwa mapana sana.
Ukiangalia katika historia ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi utaweza kuelewa mambo mengi sana na kuona mwitikio wa watanzania katika vyama vya upinzani ukoje ili kuhitimisha hisia kama ni kweli watanzania hawapendi mageuzi au kuna kitu kinawakwaza.

Kutofanya utafiti kwa vyama vya upinzani ni tatizo kubwa na mwisho wake inawaacha wengi wakiishia kulaumu na sio kutafuta tiba na changamoto wanayokumbana nayo katika kuendesha harakati zao ili kuwashawishi watanzania kuwaunga mkono.

Katika uchaguzi wa mwaka 1995, miaka mitatu tu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, watanzania walionyesha mwitikio wa hali ya juu katika kuyapokea mageuzi na yamkini kama isingekuwa juhudi kubwa ya Baba wa Taifa na na uwezo wa hali na mali basi mwaka huo CCM ingeangushwa.

Na baada ya mafanikio makubwa ya vyama vya upinzani katika uchaguzi huo, watanzania walipata fursa nzuri ya kuanza kuvitazama na kuvihakiki vyama hivi ili kuona kama ni kweli viongozi wa vyama hivi wanaweza kuwa suluhisho la matatizo wanayoyaona katika CCM.

Watanzania walitegemea kuona utawala bora, uwajibikaji ukweli na uwazi na demokrasia isiyopatikana CCM inapatikana na kuendelezwa katika vyama vya upinzani ili wakiamua kuvipa ridhaa viwe na uwezo wa kuleta tiba iliyoshindikana chini ya CCM.

Lakini muda mfupi baada ya mafanikio ya mwaka 1995 watanzania walianza kushuhudia uhalisia wa sura za ndani za viongozi wa vyama vya upinzani, kwani wengi waligubikwa na migogoro isiyokwisha huku ugomvi mkubwa ukiwa ni tamaa ya madaraka na ugomvi wa ruzuku za vyama.

Hali hiyo ilipelekea chama kikuu cha upinzani wakati huo cha NCCR-Mageuzi kuingia katika mgogoro mkubwa na hatimaye kila mtanzania aliyekuwepo wakati huo anajua kilichotokea, na hadi sasa chama hicho kimeshindwa kufufuka na kurudia katika hali na nguvu iliyokuwa nayo miaka ya 90.

Mara nyingi tumekilaumu chama tawala kama chanzo cha migogoro hiyo na kutoamua kujihakiki, kujihoji na kujitathmini ni nini mchango wa viongozi wa vyama vya upinzani katika kuchangia matatizo yanayovikumba vyama vyao.
Kwa msingi huo unaweza kuona ya kuwa watanzania ni kweli wana mwamko wa kutaka mabadiliko lakini wanatafuta mbadala ambaye anaweza kuleta tiba ya kilichokosekana ndani ya CCM ili kuwapa watanzania majibu ya kile wanachokitafuta siku zote.

Kwa hivyo vyama vya upinzani lazima viwapatie wananchi chaguo jingine bora ili waweze kuipumzisha CCM, japokuwa lazima tusisitize katika ubora na kiwango cha demokrasia katika chama mbadala kabla ya kukikabidhi madaraka.
Kuna matatizo mengi sana yanayovikumba vyama vya upinzani ambayo yanahitajika kushughulikiwa ili viweze kupata fursa ya kuwa halali mbele ya wananchi wa Tanzania na kupewa ridhaa ya kuwaongoza. Kwa hiyo vyama vya upinzani ni serikali inayosubiri kuingia madarakani.

Vyama vya upinzani ni nguzo ya utawala bora, utawala wa sheria na ulindaji na utetezi wa haki za binadamu katika demokrasia iloyokomaa.
Vyama vingi karibia vyote vya upinzani hapa Tanzania vinakuwa dhaifu kutokana na kukosekana kwa demokrasia ndani ya vyama vyao na mwenendo na mtazamo wa utendaji ambao ni tofauti na ule wa chama tawala.

Kwa hiyo kukosekana huko kwa demokrasia ndani ya vyama hivyo vinasababisha vyama vishindwe kutimiza malengo yao muhimu ambayo ni kukuza demokrasia yakweli.

Kutokana na kushindwa kuonesha demokrasia na utawala bora ambavyo vyama vya upinzani huuimba watanzania wengi wamekata tama na ndiyo maana wengine pia hawapendi kabisa kujishughulisha na masuala ya siasa.

Hiyo inatokana na uwezo mdogo wa kiuongozi wa viongozi wengi wa vyama vya upinzani Tanzania. Kwa hiyo kama ni kweli tunataka tuwe mbadala wa CCM ni lazima tutimize vigezo kadha wa kadha. Uendeshaji wa vyama hivi ndiyo unaoleta matatizo yote ambayo tunayaona leo, na hata ambavyo hatujaona kwa sasa yanaweza kuja dhihirika baadae.

Mazungumzo juu ya umiliki na uendeshaji wa chama ni kitu muhimu sana, chama cha siasa kinahitaji kati ya mambo yote kukubali juu ya matatizo makuu manne ya ya oganaizesheni ambayo yanawakumba viongozi wa vyama.

Moja, uwepo wa watu na makundi ndani ya chama ambao mtazamo wao na shauku yao ni lazima iweze kutiliwa umaanani na kuratibiwa vyema na kwa umakini pia.

Pili, uwepo wa tofauti kati ya watu na baadhi ya matabaka kwa maana ya namna ya kujihusisha na taarifa za juu ya uendeshaji wa chama ambazo zinaweza kupelekea kuwa na tofauti ya tabia.

Tatu, umuhimu wa kusisitiza nidhamu na mamlaka kwa viongozi wa chama kama wana nia ya kutekeleza malengo ya chama.

Nne, uanzishwaji na uimarishaji wa taratibu za uendeshaji na kikomo na madaraka ya viongozi lazima yaridhiwe na wafuasi/wanachama wa chama.

Mambo hayo manne yasipozingatiwa na kupewa kipaumbele ni lazima katika safari ya chama chochote kutatokea tofauti mbele na kupelekea migogoro.
Kwa hiyo tatizo kubwa la vyama liko kwa viongozi ambao hawaviongozi vyama hivyo kitaaluma bali kwa jinsi wanavyotaka wenyewe.

Kwa hiyo vingi ya vyama vya upinzani haviwakilishi matarajio ya watu wengi japo vinakariri kuwa vinafanya hivyo kama ambavyo vimeweza kuthibitisha kwa mienendo yao siku za nyuma na hata sasa.

Wanatekeleza majukumu ya vyama vya siasa kwa kutumia idadi ndogo sana ya wanachama. Kama mtu anaweza sema idadi ya watu haiathiri uendeshaji wa chama, mwingine atashangaa je viongozi wa upinzani wanafanya kazi kwa ajili ya nani?

Tatizo kubwa linalojitokeza katika nchi yetu ni kuhodhiwa kwa chama na watu wachache sana na kukiendesha kwa maslahi yao.

Ndiyo maana harakati za siasa za upinzani zimehodhiwa na watu wachache sana kutoka siku mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa hadi leo.

Kwa hiyo vyama ni zaidi ya viongozi wa vyama. Uongozi unaonekana ni muhimu sana wakati wa uanzishaji wa chama katika hatua za awali lakini chama kinapokuwa na kuendelea kukua, tabia zake na mwenendo wake lazima uamuliwe na wafuasi wake na sio viongozi pekee.

Kutokana na changamoto hizo za uongozi, Kamanda Wangwe alikuwa na mtazamo wa kujenga chama ambacho mhimili wake ulikuwa ni watu, na chama kitaendeshwa kutokana na matakwa ya watu.

Aliamini kuwa ili kujenga uhalali wa kuikosoa na kuirekebisha CCM ni lazima CHADEMA iwe safi ili tunapopinga juu ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi tuwe na uhalali huo kutoka moyoni hadi kwenye matendo yetu.

Katika kutimiza maono yake hayo, ilipotokea fursa ya kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti mwaka 2007 hakusita kuchukua fomu ya kugombea wadhifa huo ili kutumia nafasi hiyo kujenga chama kuanzia ngazi za chini.

Aliamini chama ni lazima kiweze kujikita katika vijiji na vitongoji ili kuweka nguzo na uwezo wa kuing’oa CCM. Kwani alijua kuwa chama ni wanachama na hivyo bila kutafuta wanachama hakuwezi kuwa na chama imara.

Hata hivyo katika kutimiza adhma yake hiyo alikumbana na vikwazo vingi kwani Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Ndg. Freeman Mbowe hakupenda Chacha Wangwe awe Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu anazojua yeye mwenyewe.

Hata watendaji wengi wa makao makuu walitishwa na wengine waliogopa kuonesha kwa wazi kuwa wanamuunga mkono Marehemu Chacha Wangwe ili aweze kutwaa wadhifa huo kwani walijua kwa jinsi chama kinavyoendeshwa katika misingi isiyo bora ilihitaji kiongozi mwenye uwezo na ujasiri wa kumwambia Mwenyekiti hapana katika baadhi ya mambo.

Kampeni za uchaguzi huo wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikuwa na ushindani sana kati ya Mh. Chacha Wangwe na mh. Said Arfi, Mbunge wa Mpanda Kati.

Kuna mambo mengi yalifanyika ambayo kimsingi siyo mambo yanayopaswa kufanywa na vyama vya upinzani vinavyopigania demokrasia ya kweli ili kuhakikisha kuwa mh. Chacha hafanikishi adhima yake.

Mchakato wa uchaguzi huo ulikuwa ni kama vile ulikuwa kati ya Mbowe na Wangwe kwani Mbowe alitumia juhudi kubwa sana kuhakikisha wWangwe hafanikiwi.

Wanachadema wengi hawakuwa na tatizo na mh. Arfi, lakini wengi hawakubaliani na jinsi Mwenyekiti anavyokiendesha chama, hivyo kwa kumpigia Mh. Arfi kura aliyekuwa akipigiwa kampeni na Mbowe waliona ni kama kumpigia Mbowe hivyo wengi wao wakaamua kumpigia Chacha Wangwe kura wakiamini kuwa atakuwa ni mkombozi wa CHADEMA katika mambo mengi ambayo yalikuwa yanafanywa bila taratibu.

Nia yake ilikuwa ni kuhakikisha kuwa chama kinaendeshwa kwa matakwa ya wanachama na siyo kuendeshwa kama kampuni ya mtu binafsi kwa maslahi ya mtu binafsi.

Baada ya kuchaguliwa na hatimaye kushika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania bara alijizatiti kuhakikisha kuwa anatekeleza wajibu wake ipasavyo ili kuwathibitishia wapiga kura waliomchagua kuwa hawakufanya kosa kumchagua.

Lakini kutokana na msimamo wake imara na usiyoyumba haukupita muda mrefu mgogoro kati yake na Mwenyekiti Mbowe ukawa dhahiri.

Kwa staili ya uongozi wa Mbowe anapenda kila kitu anachokitaka yeye watu waseme NDIYO MZEE na si kuangalia ni mambo gani yana faida kwa chama.
Mgogoro wake na mMbowe ulitokana na hoja za ukweli za Chacha Wangwe za kutaka kukisafisha chama ili kiwe na uhalali wa kupigana vita dhidi ya ufisadi ili chama kiwe na uhalali wa kukabiliana na vita hiyo nje ya chama.

Alifanya yote hayo akiwa na nia nzuri ya kushirikiana na wanachadema wengi ambao kilio chao kilikuwa ni kupanua demokrasia ndani ya chama ili kujenga chama imara kinachoheshimu misingi ya demokrasia ili baadae waweze kuwa mabingwa wa demokrasia katika nchi.

Watu wengi walikuwa wamechoshwa na namna ya uongozi wa Mbowe, ambapo toka aingie madarakani ametengeneza makundi sana ndani ya chama kutokana na staili yake ya uongozi ya ‘divide and rule’.

Viongozi wengi wa CHADEMA hasa wenyeviti wa mikoa na makatibu ni baadhi ya wanachadema ambao wanaujua vyema udikteta na uongozi mbovu wa Freeman Mbowe.

Kwa hiyo katika kujenga chama ambacho kitakuwa endelevu kwa maslahi ya watu wote na siyo NGO ya mtu Marehemu Chacha Wangwe alikuwa na agenda kadhaa, na nitaeleza baadhi ya hizo hapa chini.

Agenda yake kubwa ilikuwa ni kurejesha heshima ya wanachama wa CHADEMA na kuwathamini kwani wao ndio singi wa uwepo wa chama, hivyo alitaka mtazamo na maoni ya wanachama kuhusu namna ya kukiendesha chama yazingatiwe ili tuwe na chama ambacho wanaotoa maamuzi ya kukiendesha ni wafuasi wa chama.
Hivyo aliona njia mojawapo ya kuwajengea uwezo wanachadema wa chini ni kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya ruzuku inagawanywa mikoani ili kujenga mtandao wa chama.

Pia, alipambana na dhana ya ukabila katika chama. Na hapa lazima tukubaliane kuwa dhana hii siyo ya uongo bali tujue sio msingi wa katiba ya CHADEMA bali inatokana na uongozi mbovu wa Mbowe na usioangalia matakwa ya wengi bali unaangalia tu maslahi yake binafsi.

Alijikita pia kuhakikisha makao makuu ya chama kunakuwa na uwajibikaji na sio kuwa na watu wanaokaa makao makuu bila kujengewa uwezo wa kutekeleza wajibu wao kutokana na kutopewa nyenzo za kuendesha ofisi zao.

Alilenga pia kuleta umoja katika makao makuu ya chama kwani kuna mgawanyiko mkubwa ambapo kuna watu wachache wanaokumbatiwa na Mwenyekiti na kuwabagua watu wengine, watu hawa hupewa upendeleo na mamlaka wasiopaswa kuwa nayo kikatiba na wamekuwa sehemu kubwa ya kutengeneza makundi na migogoro ndani ya chama na pia kujiona wao wanafaa kuliko wengine.

Kwa msingi huo ili kupambana na hayo na ili kuhakikisha rasilimali za chama zinapatikana ili kuweza kupelekwa wilayani na mikoani ili kujenga chama alijikita katika kupambana na matumizi mabaya ya pesa ndani ya chama.

Alisema CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa katiba na wakati huohuo kikiwa kiaendesha kidikteta kwa kauli za NDIYO MZEE. Alisema alijua wazi kwamba viongozi wa sasa wa CHADEMA wanatofautiana sana na viongozi wa mwanzo wakati CHADEMA ikianzishwa.

Alitoa mfano, Mzee Mtei alikuwa akikieneza chama hasa vijijini miaka ya 95 kwa kutumia magari chakavu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi na wakijua CHADEMA si chama cha mjini, na hapa ndipo mwanzo wa CHADEMA kuwa chama tawala kule Tarime hadi sasa.

Ila katika uongozi huu wa Mbowe kila kitu kinaenda kwa kauli za ndiyo Mwenyekiti kasema na matumizi mabaya huku ufisadi ukikitafuna chama kwa matumizi hewa na kwa kigezo eti wanajilipa madeni ya kampeni za mwaka 2005.
Alisisitiza kuwa madeni hayo hayatambuliki katika mfumo wa chama kwani Mbowe alikuwa anakopa hizo pesa mwenyewe, anatumia mwenyewe bila kuingiza kwenye mfumo wa chama na analeta madeni kwenye chama ili alipwe.

Lakini Mh. Wangwe alimweleza kuwa kila mtu aliyegombea mwaka 2005 alikuwa ametumia pesa je kila mgombea aliyeshinda au kushindwa aje kuleta madeni ya fedha alizotumia katika kampeni ili alipwe.

Na baadae ilidhihirika kuwa sehemu kubwa ya madeni anayodai kutaka kulipwa na chama ilikuwa ni michango ya wapenzi ili kufanikisha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Kwa hiyo anapewa michango ya watu wanaokitakia mema chama, anasema amekikopesha na baada ya uchaguzi anadai kusamehe sehemu ya pesa hizo na kudai arudishiwe zingine.

Kwa kutumia mbinu hiyo watu waliona huyu ndio anafaa kuwa kiongozi wao kwani anaweza kujitolea katika chama kumbe mara nyingi anafanya usanii na watu wanaaminishwa usanii wake huo.

Mfano mzuri wa hivi karibuni ni wakati wa uchaguzi mdogo wa Tarime MWAKA 2008, kuna mdau aliichangia CHADEMA kwa kumpa Mwenyekiti milioni 44, wenyekiti akazileta kwenye uchaguzi, baada ya uchaguzi akataka kudai pesa hizo.
Kiongozi mmoja ndani ya chama akawa amepata taarifa juu ya chanzo cha pesa hizo, lilipoletwa wazo kwenye kikao cha sekretarieti kuwa Mwenyekiti alipwe pesa hizo wajumbe walihoji chanzo chake na mkurugenzi wa fedha alipogundua watu wameshitukia akasema itakuwa kikao kijacho na kikao cha kamati kuu kilipofika Mwenyekiti akasema amesamehe deni hilo na watu wakashangilia kwa vifijo huku hawajui mchezo wanaochezeshwa.

Katika hili la matumizi mabaya ya pesa pia alipinga Mwenyekiti kuwa mtia saini wa karibia akaunti zote za chama kwani hicho ni chanzo cha kutokuwa na uwazi na uwajibikaji, lakini Mwenyekiti aling’angania na hadi leo yeye na Mkurugenzi wa fedha Ndugu Antony Komu ndiyo waamuzi wa bajeti ya matumizi ya chama, hivyo sekretariet ya chama makao makuu inaweza kukaa hata miezi sita bila ya kupanga bajeti wala kujua pesa zinatumikaje ndani ya chama.

Vilevile alitofautiana na Mwenyekiti kwa kuendesha siasa za ukabila ndani ya chama. Na alisema katika wadhifa wake wa Uenyekiti Mbowe ameshindwa kuzingatia na kugawanya maslahi yanayopatikana ndani ya chama kwa usawa.
Kwa mfano nafasi tano katika sita za viti maalumu zilizopatikana mwaka 2005 zilienda katika mkoa wa Kilimanjaro huku nafasi moja pekee ndiyo ikienda katika mkoa wa kigoma kwa kisingizio kuwa aliangalia vigezo vya waombaji wa nafasi hizo.

Lakini alimweleza kuwa watu wengi waliomba na walikuwa na vigezo na sifa za kikatiba ni kwa nini hawakupata? Alitoa mfano hai wa muombaji wa viti maalumu kutoka Tarime aitwae Ester Matiko, ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa nini hakupata kama sifa ilikuwa ni usomi na kigezo cha taaluma?

Alisema Tarime ndiyo sehemu pekee kwa Tanzania nzima ambapo CHADEMA ilishinda kwa kura nyingi za udiwani, ubunge na hata urais. Hata Mbowe anakozaliwa na alipokuwa mbunge katika jimbo la Hai hawakumpa kura kama ambavyo Tarime walimpa, na hiyo yote ilitokana na juhudi za Chacha Wangwe.
Hivyo majibu ya hoja hiyo yalikuwa ya moto kwani ilidhihirika wazi kuwa hakukuwa na mgawanyo sawa ambao ulisimamiwa na yeye binafsi kwa kupindisha taratibu za chama. Kwa hiyo lawama sio kwa wabunge hao kwani kazi yao nzuri imeonekana ila ni kwa aliyetoa mgawanyo usio wa usawa na demokrasia ndani ya chama kinachopigania kukuza demokrasia katika nchi.

Pia alipambana na kuendesha chama kwa makundi kwani kuna watu ambao ni bora sana ndani ya chama na wengine sio bora kwa mtazamo wa Mbowe. Amekuwa akiendesha chama kwa kujenga makundi ya watu wanaomtii na kufaidi rasilimali za chama.

Moja ya watu hao hasa kutoka makao makuu ya chama ni John Mrema (Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri), John Mnyika (Mkurugenzi wa mambo ya nje) na Antony Komu (Mkurugenzi wa fedha na utawala).
Hao ndiyo watu watiifu na watenda kazi wazuri wa Bwana Mkubwa. Watu wengi hapa makao makuu hawapewi fursa sawa ili kuwawezesha kutekeleza wajibu na majukumu yao.

Pia katika hili kundi lake watu hawa mara kadhaa wamepewa pesa za chama bila kufuata utaratibu wa kanuni za fedha za chama na hivyo kuleta hisia za ubaguzi na mtafaruku ndani ya vikao vya sekretariet ya chama.

Kwa mfano mwaka 2008 John Mrema alipewa pesa za kulipia kodi ya nyumba bila kuidhinishwa kwa utaratibu wa mtu kuomba akopeshwe na ipite kwenye vikao vya sekretariet ili waangalie uwezekano wa kukopeshwa au la.
Lakini John Mrema alipewa pesa hizo na hata leo hajaweza kurejesha pesa hizo na pia inaonekana ni asante kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuchafua watu kupitia vyombo vya habari.

Pia Mkurugenzi huyo wa Fedha kwa kiburi na jeuri ya kukumbatiwa na Mwenyekiti anatumia vibaya madaraka yake na kunyanyasa watendaji wa chadema ili kufanya malipo mpaka mwenyewe apende na kama hakupendi huwezi kulipwa pesa hata kama itaidhinishwa na Katibu Mkuu.
Kiburi na jeuri hii imekuwa ikiwakumba hata viongozi wanaotoka mikoani kwani wengi wao huja na kuzungushwa sana na hata kupelekea wengine kulala kwenye mabenchi ya ofisini huku Mkurugenzi huyo wa fedha hawajali wala kuwaharakishia malipo yao.

Hivyo makundi haya yamekuwa yakidhoofisha utendaji wa chama makao makuu na Tanzania kwa ujumla. Nilipoteuliwa kuwa msaidizi wa Mwenyekiti nilikuja na azimio moyoni la kukisaidia chama kwa dhati.

Niliacha kazi yenye kipato kikubwa na kuja kupata posho lengo langu likiwa ni kuweka juhudi zangu katika kukijenga chama ambacho watanzania wameonyesha nia ya kukiunga mkono ili kufikia ukombozi wa kweli katika nchi yetu.
Baadaya kukaa muda mfupi niliweza kugundua uwepo wa makundi ndani ya chama na kikwazo cha utekelezaji wa majukumu ndani ya chama.
Nilimweleza Mwenyekiti kuwa bila kuondoa makundi haya tutakuwa hatujengi chama bora chenye mshikamano na umoja. Nilifikiri hajui wala hayaendelezi, wala hakutaka kabisa tuzungumze juu ya makundi hayo.

Pia nilimweleza juu ya kujenga uwezo wa Kurugenzi za makao makuu ili kuziwezesha kufanya kazi japo kwa kutengewa kiasi cha pesa ya ruzuku ili ziweze kuwa hai na kutimiza wajibu wao, lakini mwishowe alikuwa kimya na hilo halikutekelezeka.

Nilishangaa kwa nini idara hazitengewi pesa na kuona huu ni mfumo gani wa uendeshaji wa taasisi ambapo kila kitu na kila maamuzi yanatokana na mtu mmoja atasema nini na hata vikao halali vya chama vikipendekeza vingine yeye anakuja na kupinga maamuzi hayo na kufanya anayotaka mwenyewe.
Pia kamanda Chacha alipambana pia na ubadhirifu ulio katika Kurugenzi ya Vijana na Kurugenzi ya Mambo ya Nje.

Alisema ofisi ya Vijana nayo inanuka ufisadi kwani kuna fursa nyingi sana zinatokea za vijana wa CHADEMA kwenda nje kujifunza lakini ni vijana wachache sana hupata fursa ya kwenda nje na ilhali kuna vijana wengi wako mikoani ambao wanakipigania chama na wanaohitaji kujifunza lakini hawapewi fursa hizo.
Alisema ofisi hiyo ina watu maalumu wa kwenda semina na warsha mbalimbali za kimataifa na watu hao hupangwa na John Mnyika huku wengine unakuta sio wanachadema kabisa au analazimika kuchukua kadi ya CHADEMA ili kujenga uhalali wa kwenda nje ya nchi kwa kutumia fursa za vijana wa CHADEMA.
Baada ya kuonyesha nia ya kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya CHADEMA, watu waliokuwa wakifaidika na ubovu wa utawala na mfumo uliopo waliungana na kuhakikisha kuwa lazima wafanye kila liwezekanalo ili kumuondoa Kamanda Chacha kwani alikuwa amekuwa kikwazo katika kufanya urasimu wao.
Hivyo mkakati mkubwa ulikuwa ni kumchafua na kumuondolea uhalali mbele ya umma kama mtu anayepambana na urasimu ndani ya chama.

Walitaka kuwafanya watanzania waache kuzungumza hoja za msingi za Chacha Wangwe na kuanza kumzungumza Chacha Wangwe kama mtu.
Kwa hiyo jukumu kubwa alikabidhiwa John Mrema, ambaye ndio anajidai ni bingwa wa ushushushu ndani ya chama na mtu anayetumiwa na Mbowe ili kuwachafua watu kwa kupewa hata pesa za chama bila utaratibu ili kumudu kuendesha maisha yake.

Cha kwanza walihakikisha Mh. Chacha kama Makamu Mwenyekiti Tanzania bara hapati ofisi makao makuu ya chama ili kumfanya ashindwe kutekeleza wajibu wake.

Pia ulitengenezwa mkakati wa kumchonganisha na sekretariet ya chama makao makuu ili anapozungumzia matumizi mabovu ya pesa za chama aonekane anaingilia kazi ya sekretarieti.

Kwa hiyo ulitengenezwa mkakati “conspiracy” wa kumtengeza na kumuonesha Chacha kuwa anatumiwa kwa kutaka kukivuruga chama.
Alitumwa John Mrema kwenda Tarime kufanya CHADEMA ni msingi ambao ni mkakati wa kueneza chama haswa katika maeneo yasiyo na chama na mkakati huu ulianzishwa ili kuwasaidia watendaji wa makao makuu wenye nia ya kugombea ubunge ili kujenga mtandao wa chama katika majimbo yao.

Hivyo Mrema alienda Tarime bila ya kutaka Baraka za Mbunge wa Tarime kwenda kufanya kazi aliyoiita kujenga chama Tarime, huku akishindwa kwenda kujenga chama vunjo ambako anataka kugombea ubunge.
Katika safari hiyo malengo yake makubwa yalikuwa ni kummaliza Chacha Wangwe kisiasa kuanzia ngazi ya chini kabisa, yaani kuanzia nyumbani kwake mwenyewe.

Kupitia mkakati huo alifanikiwa kupata viongozi kadhaa na wengine wakakubali kutumika huku wakianza kumfanyia Chacha Wangwe hujuma, na mmoja wa viongozi hao alipewa ahadi ya kuteuliwa kumrithi katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Na baada ya kurudi Dar alisuka mkakati wa kumshughulikia Kamanda Chacha kwa kupitia vyombo vya habari. Nia kubwa ilikuwa ni kumuondolea uhalali wa yeye kupambana na ufisadi ndani ya chama na kuhamisha mawazo ya umma ya kutoziangalia hoja zake bali wamwangalie yeye kama tatizo.

Lakini kama kweli tunataka tupate mbadala wa CCM ni lazima tuangalie undani wa vyama kama vinashindwa kusimamia vyema pesa kidogo ndani ya vyama hivyo, je wakipewa hazina ya nchi kutakalika?
Hujuma nyingi sana zilifanywa zikiongozwa na John Mrema na John Mnyika wakishirikiana na mwezeshaji Mkurugenzi wa fedha tena kwa kutumia rasilimali za chama kupambana na mtu ambaye anakitakia chama mema.

Alikuwa akiandaa mikutano wanaihujumu ili isifanikiwe. Akichafuliwa na kwenda kwenye magazeti ili aweze kukanusha habari za kumchafua, John Mrema alikuwa akiwazungukia waandishi hao na kuzungumza nao na kuhakikisha kuwa habari za kufafanua kashfa dhidi yake haziandikwi kwenye magazeti.

Walijaribu kufanya hivyo ili kumvunja moyo na kusababisha aache mapambano ya kupigania haki ndani ya chama au kumfanya aamue kuungana nao ili kuendelea kukifaidi chama kwa maslahi binafsi.
Na ndipo mkakati ukawekwa ili kuhakikisha Chacha Wangwe anaondolewa katika wadhfa huo kwani amekuwa kikwazo na amewafanya wanaofaidi rasilimali za chama bila utaratibu kukosa raha.

Ikaundwa kamati ya wazee isiyo na mamlaka kikatiba katika kuchunguza tuhuma zilizoelekezwa kwake za kupeleka mambo ya chama kwenye vyombo vya habari.
Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo ya kwamba viongozi wafanye kazi kama timu moja kwa maslahi ya chama. Pili maadili, itifaki na nidhamu ziweze kufuatwa ili kuendelea kudumishwa kwa nidhamu ndani ya chama kwa mujibu wa katiba, kanuni na itifaki ya chama.

Tatu, kamati ya wazee walipendekeza uwepo mkakati wa usuluhishi kati ya Makamu bara na viongozi wenzake ili kuhakikisha wanaondoa tofauti zao. Baada ya kumaliza taarifa hiyo wajumbe walianza kuchambua taarifa hiyo.

Ikumbukwe kuwa kamati kuu ya CHADEMA iliyopo kwa sasa imeonekana kuwa dhaifu na kuwa watia muhuri kwa kila kitu anachokifanya Freeman Mbowe hata kama siyo chema wala hakina misingi ya utawala bora na uwajibikaji.

Kwa hiyo wakatumia ushahidi wa magazeti ili kuhalalisha na kuwaaminisha watanzania kuwa matamshi ya Kamanda Chacha Wangwe na maandiko ya Mzee Yusuf Halimoja yanafanana hivyo wakasema kwa ushahidi huo wa mazingira unadhihirisha Kamanda Chacha ni kweli anavujisha siri za chama kwa maadui wa chama.

Lakini watu wenye nia ya haki wanaweza kujiuliza huku wakizingatia mambo kadhaa na historia ya Chacha Wangwe.

Chacha Wangwe akiwa masikini aliweza kupigania haki za watu hadi kukubali kufungwa na kuiacha familia yake ikiteseka ili watu wapate haki. Chacha Wangwe alifungwa kwa kupambana na CCM. Maadui namba moja wa Chacha kisiasa walikuwa ni CCM, je inakuwaje leo baada ya Mungu kumbariki na kumpa Ubunge kutokana na upambanaji wake wa muda mrefu ndiyo aje kugeuka?

Kwa hiyo zote hizo zilikuwa ni njama na hujuma za kumchafua ili kumuondolea uhalali wa kupambana na kuondoa ukiritimba na ufisadi ndani ya chama.
Baada ya tuhuma hizo hakupewa muda wa kuandaa na kuleta utetezi wake, kwani kamati iliyoleta mapendekezo na tuhuma pia ilikuwa na muda wa kutosha.
Na hakuna mfumo wowote wa kutoa hukumu bila ya kumpa mtuhumiwa fursa ya kuandaa na kuleta utetezi wake mbele ya waamuzi ili waweze kufanya maamuzi ya haki.

Kwa hiyo siku hiyohiyo na muda huo huo walipendekeza ipigwe kura ya kutokuwa na imani nae, na wajumbe wa kamati kuu ambao wengi wao ni watu wasio na msimamo na ni waitikiaji wazuri wa kiitikio cha ndiyo mzee.

Idadi ya waliopiga kura walikuwa 31, waliosema asimamishwe walikuwa 24, na waliosema asisimamishwe walikuwa 7. Hivyo kwa uamuzi huo Mh. Chacha akawa amesimamishwa rasmi na kamati kuu ya chama Taifa nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti bara.

Katibu Mkuu akaelekezwa amjulishe kwa barua rasmi. Haki yake ya rufaa ielezwe wazi katika barua hiyo kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na katiba ya chama.
Baada ya kamati kuu kufikia uamuzi huo, Mwenyekiti wa Taifa aliwaambia wajumbe kuwa chama kiko kwenye mchakato wa uchaguzi na muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu ngazi ya Taifa ni mdogo sana hivyo hapataitishwa baraza kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.

Suala hilo litashughulikiwa na baraza kuu litakalofanyika kwa mujibu wa katiba, aidha Mwenyekiti pia aliitaka ofisi ya Katibu Mkuu iandae utaratibu wa kuujulisha umma uamuzi huo mgumu wa kamati kuu ya chama.

Nachojiuliza mimi hapa hakiwezi kupata majibu, aliyesimamishwa kaambiwa ana haki ya kukata rufaa lakini wakati huo huo Mwenyekiti anatangaza kuwa baraza kuu halitaitishwa ili kusikiliza rufaa ya Chacha Wangwe.

Kweli huu ndio utawala bora tutakaoupeleka serikali kuu kama tukipewa ridhaa hiyo na watanzania? La hasha huu ni uhuni katika utawala na ubabaishaji wa kiwango cha juu. Tusipojikosoa na kukubali changamoto hatuwezi kujenga chama mbadala kitakacholeta fursa ilizoshindwa CCM.

Kwa nini walikuwa hadi wakipanga kumnyima fursa ya rufaa tena kwenye chombo kilichomuajiri ili kione kama amekiuka matakwa ya ajira yake ili kiweze kumng’oa chenyewe.

Lakini pamoja na wao kutoonyesha nia ya kumpatia jukwaa la kukata rufaa, Kamanda Wangwe aliandika barua ifuatayo ili kupinga maamuzi ya kumsimamisha wadhifa huo.
Chacha Zakayo Wangwe
S.L.P 411
Tarime
10 – 07 – 2008
BARAZA KUU LA CHADEMA
MAKAO MAKUU YA CHADEMA
DAR ES SALAAM
Waheshimiwa wajumbe wa Baraza Kuu.
YAH: RUFAA DHIDI YA ADHABU YA KUSIMAMISHWA MAKAMU MWENYEKITI TAIFA CHADEMA
Kwa heshima na unyenyekevu naomba niwasilishe rufaa yangu mbele yenu ili mpitie upya uamuzi wa kamati kuu na kutengua adhabu iliyonipa tarehe 28-06-2008.
Sababu za mimi kutoridhika na uamuzi wao ni za kukiukwa haki za msingi za uanachama wangu, ubinadamu wangu, upendeleo uliowazi aliofanyiwa mwenyekiti wa taifa baada ya kuwatamkia wajumbe wa kikao kwamba wasiponiondoa yeye hataendelea kuongoza chama chetu.
Maelezo
Naomba kutoa maelezo mafupi kwa kila sababu ya rufaa yangu ili siku ya kikao nijieleze mbele yenu kwa ufasaha zaidi na baadaye nijibu maswali na hoja mtakazoniuliza.
1. Mahusino yaliyoharibika kwa ajili ya uchaguzi wa nafasi Makamu Mwenyekiti Taifa:-
Desember 19, 2007
Wakati wa uchaguzi wa Makamu Mwekiti Taifa,uongozi wa makao makuu ulimpendelea na kumfanyia kampeni mgombea mwenzangu Mhe. Said Arfi na niliposhinda waliendeleza chuki hizo mpaka waliposhinikiza kamati kuu kunisimamisha uongozi (siku ya kujieleza nitatoa uthibitisho wa jambo hilo).
Kutokupewa mashitaka /tuhuma juu yangu ili nijitayarishe kabla ya vikao vya mashitaka kwa mfano kamati ya wazee na hata kamati kuu.
Nilishitukizwa mbele ya vikao hivyo na kuambiwa nijitetee kwa tuhuma zilizoletwa mbele ya vikao hivyo. Hii ni ukiukwaji wa haki za binadamu kama ilivyo ainishwa katika katiba ya jamhuri ya muungano wa TANZANIA KUWA SI RUHUSA mwananchi kushitakiwa na kuadhibiwa bila kupewa nafasi ya kujitetea na kama ilivyo katiba ya CHADEMA.
2. Kamati ya wazee isingeweza kunitendea haki kwa sababu:-
(a) Wote wanahusiana na Mwenyekiti wa Taifa ambaye ndiye mshitaki wangu mkuu.
(i) Mzee Mtei ni baba mkwe wake, mzazi wa mkwe wake bwana Mbowe
(ii) Wengine waliobaki a ni wajumbe wa kamati kuu walioteuliwa na Bwana Mbowe mwenyewe.
(b) Kamati hiyo iliniita na kunihoji mwenyewe bila kupewa mashitaka na chama makao makuu na hivyo ilikua kamati ya uchunguzi na kutunga mashitaka baada ya kuwa chombo cha usuluihishi.
(c) Katika uchunguzi wake kamati ya wazee ilileta tuhuma nyingi juu yangu bila kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kuondoa mgogoro au kueleza mwenye makosa ni nani. Haikuleta ushaidi wala vielelezo vya mlalamikaji.
Kamati kuu ilipokea tuhuma hizo na kunisomea bila kwanza kunipa muda wa kuyasoma ya kujitayarisha kwa utetezi. Hapo haki isingeweza kutendeka wala uamuzi wa haki kutolewa… Hivyo mshitaki wangu mbele ya kamati kuu sio Mwenyekiti Taifa na makao makuu ila ni kamati ya wazee ambao ni wajumbe wa kamati ambayo haina mamlaka kikatiba (kamati ya wazee). Hivyo kamati batili ilifanya uchunguz,ikanishitaki kwa yenyewe na kutoa mapendekezo. Walikua Polisi Washitaki na Hakimu. Vyovyote vile uamuzi wao ni BATILI kikatiba,kisheria na kwa misingi ya haki za binadamu hata mbele ya Mungu kwa mujibu wa vitabu vitakatifu vya dini zetu.
(d) Kwa mujibu wa katiba chama toleo la 2004, Hakuna kikao cha kamati ya wazee chenye majukumu ya kupeleleza au kuchunguza masuala kama haya na kuyawasilisha kamati makuu kama ilivyofanyika katika shauri langu. Mwenyekiti Taifa au makao makuu hawana mamlaka ya kuunda kamati ya wazee ili ifanye kazi ya uchunguzi kwa masuala kama hayo. Hivyo kamati hiyo ya mzee Mtei na uamuzi wao kwa mujibu wa katiba ya chama inavyotumika hivi sasa-Toleo la 2004.
(e) Idadi ya kura zilizopigwa hazikutosheleza mahitaji ya kifungu /ibara 6.3b(f) ambayo inataka kura ya kunisimamisha wawe theruthi mbili ya kura zilizopigwa kwani:-
1. Kura zilizopigwa zilikua 31
2. Kura za hapana 7, hivyo jumla zilikua 24
3.Wajumbe wa mikoa mitano hawakuwa wajumbe halali na hivyo kura halali zilikuwa 19 tu wakati theluthi mbili ya 31 ni 21
4. Hata hivyo wajumbe watano waliokua katika kamati ya wazee ambao walikua washitaki (prosecutors) wangu hawakupaswa kupiga kura kwani walisimama badala ya walalamikaji. Hivyo kura zinazobaki ni 14 na kwa ajili hiyo uamuzi wa kamati kuu haikufikia theluthi mbili ya kuniondoa . Uamuzi uilitangazwa ulikua batili.
Maombi;-
(1) Kwa sababu nilizozitoa hapo juu uamuzi wa kamati kuu ulikua msingi wa haki na katiba na hivyo Baraza Kuu liufute kwani ni batili.
(2) Baraza Kuu liamuru nirudishwe katika nafasi ya Makamu Mwenyuekiti bila masharti yoyote.
(3) Pamoja na yaliyotangulia kama balaza kuu litaona ni vema liunde kamati ya uchunguzi upya itakayo fanya kazi kwa haki na uwazi na kuleta mapendekezo katika baraza hili ya namna ya kutatua migogoro hiyo iliyojikita ndani ya chama.
Wanachama na wananchi walioko jimboni Tarime, Jimbo ambalo linaloongozwa na CHADEMA, wameguswa sana na wametaharuki kwani kwa imani walioyonayo katika chama chetu , hawakutarajia maamuzi kama haya yasiyozingatia haki, katiba ya nchi na ya chama. Hili linaweza kutuathiri vibaya katika chaguzi zilizo mbele zetu.
Kwa kuwa nilichaguliwa kihalali na Balaza kuu hili, naamini kuwa maamuzi mtakayoyafikia yatanitendea haki na kujali maslahi ya chama chetu.

Nawasilisha

Chacha Zakayo Wangwe (MB)

Mwanachama.

Wakati anasimamishwa wadhifa huo mimi nilikuwa nchini Uganda lakini kupitia mtandao wa internet niliweza kupata taarifa hizo na nikampigia simu ili kujua ukweli ni upi juu ya tuhuma zilizoelekezwa kwake na kama ni za kweli kwani kwa jinsi nilivyokuwa nikifahamu moyo na nia yake ya kupambanna nilishangaa kusikia leo hii anaweza kufanya uamuzi wa namna hiyo.

Yeye alinijibu kuwa hana ugomvi na chama kwani siku zote amekuwa mstari wa mbele katika kuyatoa maisha yake ili kuijenga CHADEMA kuanzia ngazi za chini kabisa. Ila alisema alipoonyesha wasiwasi juu ya madeni yasiyoisha ikaundwa tume ya kampeni za kutokuwa na imani na yeye.

Alisema wapo wanachama kama yeye ambao kama wakipewa nafasi za uongozi ndani ya chama watafanya vizuri zaidi ya hawa wengine. Akasema pengine aweke wazi kuwa yeye ni kiongozi shupavu asiye na hata chembe ya woga katika kutetea na kusimamia maslahi ya mwanachama wa CHADEMA tena asiyependa siasa za kisanii.

Ukweli huo ndio uliomfanya Mbowe kuwa mstari wa mbele katika kupiga kampeni na baadae kura ya kutokuwa na imani na yeye. Alisisitiza kuwa yeye binafsi alikuwa anaamini chama cha siasa mtu muhimu ni mwanachama na si Mwenyekiti au Katibu.

Alisema hakuniambia hayo ili kufanya niamini kuwa anataka kuwa kuing’ang’anizi kwenye wadhifa aliovuliwa, bali alipenda nifahamu picha halisi ya uendeshaji wa siasa ya CHADEMA na kisha niweze kugundua uhalisia wa mgogoro ulivyo.

Alisema Mbowe alimng’oa katika wadhifa aliokuwa nao kwa hila kwa sababu zake binafsi na si kwa sababu za chama kama chama, na anajitahidi kuzunguka mikoani yeye na watu wake kwa siri kuendelea kumchafua kuwa hafai.

Alisema ni kweli alikuwa hafai kwa wafuja ruzuku ya chama, kweli hakufaa kwa mafisadi ndani ya chama, ila alifaa kukiendesha chama katika ngazi ya taifa katika nafasi yoyote na siku zote. Alisema anafaa kwa sababu amefukuzwa kwa kusema ukweli hivyo akageuka mwiba katikati ya majipu, akatolewa.

Aliendelea kusema anafaa kwa sababu hayuko tayari kukaa ofisini kama mafaili ila anafaa kwa sababu yeye ni mpambanaji, kamanda shujaa, aliye tayari kuwajibishwa kwa ajili ya kuwatetea WANADEMOKRASIA hususani WANACHADEMA nchi nzima.

Alisema kuliendesha taifa kama Tanzania hakuhitaji siasa za kisanii, fitina, na chuki. Kinachotakiwa ni nani abadilike alete mabadiliko katika siasa ili aweze kukabidhiwa dola na alete mabadiliko.

Alisema wananchi wamechoshwa na siasa zetu ndiyo maana wanaziita siasa za kisanii. Wanahitaji mabadiliko, CHADEMA ni chama cha kidemokrasia lakini huko anakoelekea Mbowe tayari ameiondosha demokrasia ndani ya CHADEMA kwa kumtoa katika wadhifa wa umakamu mwenyekiti kwa kupiga kampeni ndogo ya wajumbe 31 tu, tena kwa kumtuhumu kuwa anavujisha siri za chama.

Anasema alipokuwa Makamu Mwenyekiti ndipo fedha zilipoanza kwenda mikoani kwa viwango halali na ndipo ukarabati wa makao makuu ya chama ulifanyika na kuyaboresha ili yalingane na hadhi ya chama.

Alisema baada ya yeye kusimamishwa kwenye wadhifa aliokuwa nao alipata simu nyingi sana za wanachama na hata baadhi ya watendaji makao makuu wakimwambia kuwa kama Mbowe hayuko tayari kufanya nae kazi wao wako tayari kufanya nae kazi, na bado wanamhitaji katika uongozi taifa.

Alisema kimsingi, tusiposhikamana kwa sauti moja, lengo moja na kwa msimamo, ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi kitaendelea kushika dola hadi utimilifu wa dahari. Alisema chama kisipokuwa madhubuti hakiwezi kushika dola, hakiwezi kuaminika na wananchi.

Alisema CHADEMA ni lazima tufike mahali tubadilike, tujue tuna lengo la kuiongoza Tanzania na si vinginevyo.alisema baada ya kulewa katika kuwafichua mafisadi sasa tumejisahau. Aliamini kuwa nguvu ya umma ndiyo nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Aliamini siku zote kuwa katika chama chochote cha siasa, mwanachama ndiye bora kuliko kiongozi. Aliamini kuwa msingi bora wa chama hujengwa na watu makini.

Alihoji ni kwa nini chama kimeshindwa kupiga hatua kimaendeleo? Alisema makao makuu ya sasa ya chama yalinunuliwa na uongozi uliopita wakati chama kikipata ruzuku ya milioni tano, je imeshindikanaje uongozi unaopata zaidi ya milioni 65 na misaada lukuki kutoka ndani na nje ya nchi umeshindwa hata kununua nyumba ya ofisi Dar Es Salaam au hata mikoani.

Alisema haamini kama Mbowe anaweza kuleta mabadiliko ya kweli kwani yeye binafsi hajabadilika na akahoji kama kweli yeye ana matatizo je ni kwa nini pia Mbowe alishindwa kufanya kazi na Dr. Kaborou na Shaibu Akwilombe?
Alihoji ni kwa nini ashindwe kufanya kazi na wenzake?

Katika kipindi chote cha uongozi wa Mbowe kama Mwenyekiti wa chadema amegombana na Makamu wake wote wawili na Naibu Katibu Mkuu. Je ni kweli kuwa watu wote hawa wana matatizo?

Je yeye ni mtimilifu kuliko hawa wengine? Katika chama kinachosaka kupata wanachama kwa gharama kubwa je suluhisho la kutofautiana ni kufukuzana?
Mbona katika CCM, Spika wa Bunge anaweza kuwa na uhuru wa kumkosoa Rais wa nchi waziwazi tena katika Bunge lakini hatujasikia Rais amefanya hila za kumtimua Spika, kwani kama akiamua kufanya hivyo hawezi shindwa tekeleza.

Anaposema hawezi kufanya kazi na Fulani anamaanisha hicho chama ni mali yake binafsi? Kwa nini yeye asijiudhuru nafasi yake hiyo kama hawezi fanya kazi na mtu aliyeaminiwa na wanachama na wakamchagua ili atetee maslahi yao?
Alisema alitaka kuwa Mwenyekiti ili aondoe makundi ndani ya chama na kujenga chama chenye ukomavu na uvumilivu wa kisiasa na kiuongozi kwani ni lazima kiongozi awe msikivu kuliko kulazimisha anayoamini ndio uwe msimamo wa chama.

Alisema haamini Mbowe kama ni kiongozi mzuri kwani hasikilizi watu bali anataka wao ndio wamsikilize,
Alisema kwa mfano alikuwa kinyume na matumizi ya helkopita katika uchaguzi lakini akaanza kuonekana mbaya. Alisema hakuona sababu ya kutumia helkopita wakati wanachama wa vijijini hawakijui chama wala sera zake huku viongozi wa wilaya na mikoa wakishindwa hata kutoa durufu (photocopy) za vipeperushi vya chama kwa kukosa ruzuku.

Alisema katika chama cha siasa ni lazima viongozi wawe na uvumilivu na kuchukuliana, kushirikiana na hata wakati mwingine kukubali kuacha msimamo wako na kukubaliana na wenzako. Alisema demokrasia ya kweli inataka makubaliano ya kukubaliana ili kujenga mahusiano na uvumilivu.

Alisema mbowe hana uvumilivu. Na hata Mahatma Gandhi alisema kuwa “kutokuwa mvumilivu pekee ni aina ya fujo na kikwazo kwa ukuaji wa moyo wenye demorasia ya kweli” (Mahatma Gandhi famously argued, “intolerance isitself a form of violence and an obstacle to the growth of a true democratic spirit” (cf. UNDP,2002)).

Baada ya kuwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA makao makuu niliweza kujidhirisha juu ya mengi sana na pia kujifunza mambo mengi sana.
Ni kweli watanzania tumekuwa watu wa kuwalaumu sana watu wengi wanaojitoa katika vyama vya upinzani na kujiunga na CCM au vyama vingine vya upinzani.
Kwa sasa siwezi kuwalaumu wala kuwahukumu bila kusikiliza upande wa pili kwani siasa za Tanzania zimejaa uchafu, fitina na chuki. Hivyo tusipobadilisha mwenendo wetu hatuwezi kufika mbali.

Ni lazima viongozi wajifunze uvumilivu na wakubali changamoto za uongozi na sio kuwafukuza viongozi na wanachama kwa sababu eti wamekuwa na mtizamo tofauti na wa kwake juu ya uendeshaji wa chama.
Ni lazima katika mazingira ya ukuaji na ujengaji wa demokrasia ya kweli maamuzi ya wanachama yaweze kupewa kipaumbele la sivyo watanzania hawataviamini vyama vya upinzani na wataona ni bora waendelee kubaki kuongozwa na CCM.
Kwa hiyo suluhisho la yote haya ni kujenga chama imara kama taasisi chenye demokrasia kubwa ndani ya chama chenyewe. Ili lengo la kukuza na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vya siasa vya upinzani liwe dhahiri kabla vyama hivyo havijawa mabingwa wa demokrasia katika taifa, haki za binadamu, na utawala bora.

Kwa hiyo mtazamo wangu kwa sasa ni kwa sisi sote tujidhatiti katika vyama vyetu, sio kwa jinsi vilivyo leo bali kwa vyama vyetu kwa jinsi vinavyotakiwa na vinavyopaswa kuwa. Sisi sote tunajua kuwa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinaweza kufanya vyema zaidi, kwa mfamo kwa kuonyesha kuwa wako karibu na kuonyesha uhalisia wa siasa katika maisha ya watu wa kawaida sana na haswa kufanya siasa ya kidemokrasia kuwavutia vizazi vichanga (young people).

Tunaweza kufanya vyema zaidi kwa kuhakikisha siasa inakuwa juu ya “sera na si majina ya watu” ukweli na sio maneno yasiyo kweli na ya uongo. Tunaweza kudhihirisha kuwa kanuni zinapewa nafasi katika siasa, kama tunavyojua kuwa siasa bila kanuni na utaratibu zinabaki kuwa ni kugombania madaraka na vyeo tu.

Kwa hiyo ni matazamio ya watanzania kuwa CHADEMA itaimarisha utamaduni wa demokrasia ndani ya chama. Tunaweza kuzuia matumizi mabaya ya pesa katika siasa zetu, tuwe wawazi na wawajibikaji katika uongozi wetu na kuinua ushiriki wa wanawake na makundi mbalimbali katika chama.

Katika Luka sura ya 12, mstari wa 48, biblia yangu inaniambia kuwa: “na kila aliyepewa vingi,kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”
Kwa hiyo wote tuliopata kusoma kitabu hiki na ukurasa huu naweza kuwachukulia ni moja ya waiopewa vingi. Na jukumu letu na jukumu tunalobeba kwa hakika ni kubwa sana: kuwakilisha watu wetu, kufanya kazi kwa matakwa yao, tusaidie kujenga “maisha bora kwa wote”, na naweza kuongezea kufikia kiwango cha juu cha demokrasia kama kilichowekwa na Jumuiya ya Madola katika azimo la Harare kama lilivyowekwa kwa ajili yetu wote.

Hivyo pamoja na kwamba Kamanda Chacha hatunaye tena, ni heri kama tukiendeleza yote mazuri aliyotazamia kukifanyia CHADEMA kwa maslahi ya watanzania wanyonge na si kuudanganya umma wa watanzania kuwa alikuwa akitumika kukihujumu chama kwa niaba ya maslahi ya wanasiasa wanaogeuza chama kama mtaji na kijiwe cha biashara zao.

Na mwisho nasema kuwa kwa wanachadema wote tuliosoma tutakuwa tumepata meseji yenye nia ya kujenga na si kubomoa, kwa hiyo “message sent”. Kilichobaki ni hiyo meseji kuingia na kuwa sehemu ya maisha na mienendo yetu katika kujenga chama na si makundi kwa niaba ya mtu Fulani tutakuwa tunaandaa anguko la chama kama tulivyoshuhudia katika vyama vingine vilivyokuwa maarufu na vikaanguka.
Tuwakatae kwa moyo mmoja watu wanaotumika kugawa chama katika makundi kwani watu hao hawafai kwa mustakabali wa CHADEMA, bali yamkini wametumwa kuivuruga CHADEMA. Lazima kanuni, taratibu na katiba zizingatiwe katika kujenga chama endelevu.
 
du sijawahi kujua kuwa mbowe na mzee mtei ni mtu na mkwewe du hii kali
 
Kama tunataka maendeleo ya dhati kwa nchi zetu za kiafrika hususani Tanzania, suala la demokrasia ni lazima liwekwe kando kwa miaka kadhaa ili tuweze kuweka misingi na taratibu ambazo ni imara na zenye kuleta tija kwa maendeleo ya mtu na taifa kwa ujumla. Huu wimbo wa demokrasia unatumiwa ndivyo sivyo, na matokeo yake tunazidi kurudi nyuma badala ya kusonga mbele kwani kila uovu ama jambo baya linalofanyika kwa sasa wachache hujitahidi kulifunika kwa kigezo cha demokrasia.

Kimsingi kwa nchi kama Tanzania tunahitaji kuendeshwa kwa amri ama kushurutishwa zaidi ya kuacha mwanya kwa kila mtu kujifanyia atakavyo. Ombi langu ni kama angepatikana mtu mwenye ule moyo wa utaifa ambao uko kwa dhati rohoni mwake, akachukua uongozi wa nchi yetu kwa miongo kadhaa bila kuangalia mataifa ya nje yanasema nini, ili tuweze kuondokana na hii hali ya kulinda uchafu na uozo ndani ya jamii na taifa kwa ujumla kwa kisingizio cha demokrasia. Wakati mwingine inabidi hata bakora zitumike kuhakikisha mambo muhimu yanafanyika kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla.
 
Mkuu taffu69 umenena,

Nchi zinazotaka kuendelea huwa hazikumbuki demokrasia,huu wimbo huwa tunaimba sisi nchi maskini na tusiotaka kuendela,eti usawa wa kidemokrasia katika kuchagua,huu upuuzi tunaletewa na mataifa yaliyoendelea ili sisi tubaki maskini wao waendelee kutunyonya,yaani kura ya msomi na mweledi au mfanya biashara mkubwa ambaye sera ya nchi ikibadilika iwe sawa na ya yule asiye jua hata sera wala ilani ya chama inasemaje na inamaanisha nini?

Hii ndio kutoitendea haki hiyo kitu inaitwa uchaguzi,lazima watu wa aina hizi tofauti watakuwa na mawazo tofauti kuhusu uchaguzi, kwanini wanachagua chama fulani, kwanini wanamchagua fulani na sio fulani, kwanini wanadhani akichaguliwa huyu atakuwa bora kuliko huyu, ndio maana nchi kama marekani huwa wana kura za uzito kutokana na majimbo yao mpaka unaambiwa mgombea fulani ananguvu kwa sababu anaungwa mkono na jimbo fulani na lina kura nyingi kwenye kitu inaitwa electoral commission,ambayo inakuwa na watu kadhaa wanawakilisha kura za majimbo yao.

Sisi bwana tumeng'ang'ania ushindi wa wingio wa kura tu hatujui wala hatujiulizi hao wengi waliotupigia kura wanauelewa gani katika sera tulizozitoa katika kampeni.

Anyway nilisahau kwamba hii ni nchi ya ujamaa na kujitegema na kwahiyo suala la usawa wa bianadamu ni la muhimu kuliko maendeleo
 
Mkuu tuwekee chote basi tukisome

Ningependa sana Mkuu lakini naogopa kuwa kwanza nitakuwa naiba kazi ya mwandishi bila ridhaa, pia kutype kitabu chenye kurasa zaidi ya 120 kinachoelezea maisha ya Hayati Wangwe toka utotoni, shuleni, kufanya kazi, harakati zake kisiasa, hadi kuwa Mbunge n.k ni mzigo mkubwa ambao unaweza sababisha niache muda wangu mwingi wa kazi na naweza hatarisha hata kibarua changu.
kimsingi ni kitabu kizuri sana na kina mambo mengi sana tunayoweza kujifunza kama watanzania.
Awali sikuwahi kujua kama Chacha Wangwe alikuwa Rasta Man, cover la kitabu hicho kimepambwa na picha kubwa ya enzi akiwa na Rasta Ndefu hadi kiunoni.
msambazaji yuko hapahapa Dar, mtafute kwa 0763 632008 na waweza pata nakala yako.
 
Ningependa sana Mkuu lakini naogopa kuwa kwanza nitakuwa naiba kazi ya mwandishi bila ridhaa, pia kutype kitabu chenye kurasa zaidi ya 120 kinachoelezea maisha ya Hayati Wangwe toka utotoni, shuleni, kufanya kazi, harakati zake kisiasa, hadi kuwa Mbunge n.k ni mzigo mkubwa ambao unaweza sababisha niache muda wangu mwingi wa kazi na naweza hatarisha hata kibarua changu.
kimsingi ni kitabu kizuri sana na kina mambo mengi sana tunayoweza kujifunza kama watanzania.
Awali sikuwahi kujua kama Chacha Wangwe alikuwa Rasta Man, cover la kitabu hicho kimepambwa na picha kubwa ya enzi akiwa na Rasta Ndefu hadi kiunoni.
msambazaji yuko hapahapa Dar, mtafute kwa 0763 632008 na waweza pata nakala yako.

Msambazaji wa hiki kitabu ni wewe na hili ni tangazo la biashara.
 
..all i know ni kwamba siwezi kumnunulia mwanangu kitabu cha maisha ya Chacha Wangwe.
 
Kuna hoja zingine zilizoandikwa humu zinahitaji ufafanuzi kidogo ili kujenga upinzani wa kweli na mikakati mipya.
- Ni kweli wajumbe wa mikutano wanatoka mikoani na hulala kwenye mabenchi ktk ofisi za CHADEMA?
- Ni Kweli watu wanapewa safari za mafunzo nje ya nchi wasio wanachama wa Chadema? na kuachwa watu wa mikoani ambao watafaidika zaidi na mafunzo hayo?
- Ni kweli makamu mwenyekiti wa CHADEMA alikuwa hana ofisi makao makuu ya chama? Je wadhifa wake na majukumu yake yanahitaji awe na ofisi?
- Kulikuwa na haja ya kukodi helikopta wakati makao makuu ya wilaya hawana hata mashine ya kurudufia?
- Ni kweli kuna mfadhili alitoa milioni 44 za kwa uchaguzi na Mbowe akadai ni yeye amekopesha chama?

Ili kuimarisha mapambano dhidi ya ufisadi, lazima CHADEMA iwe imara. Hoja zinapoletwa zijibiwe, vinginevyo itakuwa kama CCM wanaosema kila siku, " leteni ushahidi" au "tume imeeundwa" au " uchunguzi unaendelea"
 
watanzania Bwana watu wa ajabu maana tunataka mabadiriko alafu hatutaki kubadirika, ulipokuja waraka tukasema tujadiri content, leo kimeletwa kitabu hamtaki kujadili content mnamshambulia mletaji wa mada mmmh yaani nimeishiwa nguvu kabisa
 
Kuna hoja zingine zilizoandikwa humu zinahitaji ufafanuzi kidogo ili kujenga upinzani wa kweli na mikakati mipya.
- Ni kweli wajumbe wa mikutano wanatoka mikoani na hulala kwenye mabenchi ktk ofisi za CHADEMA?
- Ni Kweli watu wanapewa safari za mafunzo nje ya nchi wasio wanachama wa Chadema? na kuachwa watu wa mikoani ambao watafaidika zaidi na mafunzo hayo?
- Ni kweli makamu mwenyekiti wa CHADEMA alikuwa hana ofisi makao makuu ya chama? Je wadhifa wake na majukumu yake yanahitaji awe na ofisi?
- Kulikuwa na haja ya kukodi helikopta wakati makao makuu ya wilaya hawana hata mashine ya kurudufia?
- Ni kweli kuna mfadhili alitoa milioni 44 za kwa uchaguzi na Mbowe akadai ni yeye amekopesha chama?

Ili kuimarisha mapambano dhidi ya ufisadi, lazima CHADEMA iwe imara. Hoja zinapoletwa zijibiwe, vinginevyo itakuwa kama CCM wanaosema kila siku, " leteni ushahidi" au "tume imeeundwa" au " uchunguzi unaendelea"

Haya maswali yalishajibiwa sana hapa. Chukua muda tu kusoma topic zote za JF utayapata.
 
Well, wanaoendesha hizi fitna tunawajua na wewe inajulikana wazi upo pande ipi ! Unaweza danganya watoto, lakini sio watu wazima wenye akili timamu na wanaojua hizo propaganda zenu...

Endelea kufaidi hayo"matunda" ya mafisadi, lakini ipo siku zitawatokea puani..

Umejitahidi kweli kusambaza haya mabandiko kila kona ya "mujini"....
 
Well, wanaoendesha hizi fitna tunawajua na wewe inajulikana wazi upo pande ipi ! Unaweza danganya watoto, lakini sio watu wazima wenye akili timamu na wanaojua hizo propaganda zenu...

Endelea kufaidi hayo"matunda" ya mafisadi, lakini ipo siku zitawatokea puani..

Umejitahidi kweli kusambaza haya mabandiko kila kona ya "mujini"....

Halafu cha kuchekesha zaidi, ni pale anapoleta unafiki kuwa hana uhusiano na msambazaji wa hiki kitabu. Kuna sehemu ya matangazo ya biashara kwenye hii forum. Angeenda moja kwa moja pale na kuweka hili tangazo lake kama matangazo mengine ya biashara huko.
 
Nitarudia kusema hivi mnapoandika habari nzito kama hizi ni bora sana mfikiriew kwanza WATU na MAZINGIRA.. watu ni pamoja na mila, desturi miiko na kadhalika.. sasa Imagine leo mtu anajitokeza hapa JF kuelezea maisha yake ya shida au kuandika kitabu chenye kuelezea maisha ambayo wananchi zaidi ya asilimia 80 ndio maisha yao ya kila siku..

Kila unachosoma kuhusu Lawama za viongozi Wadanganyika ni kuonyesha kwamba wao wanastahili Special treatment kwa sababu fulani zisizo na msingi na kibaya zaidi malalamishi yao wanayapeleka kwa wananchi walalahoi ambao hata hizo Hotel hawajawahi kulala. Malalamiko yote ya Mheshimiwa wamgwe sii matumizi ya fedha hizo kwa kuwanufaisha wananchi ila ni haki ya mtazamo wake ktk mgao wa fedha na madaraka baina ya viongozi wa Chadema..

Hakika inachosha sana kusoma habari kama hizi.. It's all about them.
 
Kama tunataka maendeleo ya dhati kwa nchi zetu za kiafrika hususani Tanzania, suala la demokrasia ni lazima liwekwe kando kwa miaka kadhaa ili tuweze kuweka misingi na taratibu ambazo ni imara na zenye kuleta tija kwa maendeleo ya mtu na taifa kwa ujumla. Huu wimbo wa demokrasia unatumiwa ndivyo sivyo, na matokeo yake tunazidi kurudi nyuma badala ya kusonga mbele kwani kila uovu ama jambo baya linalofanyika kwa sasa wachache hujitahidi kulifunika kwa kigezo cha demokrasia.

Kimsingi kwa nchi kama Tanzania tunahitaji kuendeshwa kwa amri ama kushurutishwa zaidi ya kuacha mwanya kwa kila mtu kujifanyia atakavyo. Ombi langu ni kama angepatikana mtu mwenye ule moyo wa utaifa ambao uko kwa dhati rohoni mwake, akachukua uongozi wa nchi yetu kwa miongo kadhaa bila kuangalia mataifa ya nje yanasema nini, ili tuweze kuondokana na hii hali ya kulinda uchafu na uozo ndani ya jamii na taifa kwa ujumla kwa kisingizio cha demokrasia. Wakati mwingine inabidi hata bakora zitumike kuhakikisha mambo muhimu yanafanyika kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Katika mambo yaliyowahi kuyafurahisha macho yangu, na akili yangu ni hayo mawazo yako hapo juu!

You clearly pictured what is in my mind. Demokrasia ni njia ya kuficha wovu na si kuleta maendeleo hata. Mataifa makubwa yamekuwa yakitumia "democrasia" kubomoa, au kudhoofisha nchi masikini kwa kupandikiza viongozi wao. Na ndio maana china wao wameipa demokrasia mtazamo tofauti kidogo.

Nchi kama Libya, Cuba zisingekuwa hapa zilipo leo kama wangetumia democracy kama sisi watanzania na wajinga wengine masikini kama sisi!
 
Mkuu tuwekee chote basi tukisome
Naona kwa ombi hili linafaa lipandishwe kwenye magorofa ya wakuu wa JF ili watazamae kama ipo nafasi kwenye madroo yao wafungue sehemu ambapo vitabu mashuhuri na muhimu kwa dondoo vitakuwa vinawekwa as online library ya JamiiF ,ni wazo tu ,huwezi kujua pengine uwezo upo ila hawajafikiria na hapa tunasaidiana mawazo kwa misingi flani flani. Kwa mfano kule juu kuna bongo fleva,taarab zilipendwa cjui injili naona zote hizi hazina maana kwani ni vitu ambavyo vimejaa kwenye mitandao mingine au hata webu zingine ,hivyo nafasi zile zingeweza kuwekwa kama library na kujazwa vitabu kibao hata vya bulicheka na mkewe au hekaya za abunuwasi au alfulelaulela au vile vya akina makumazan na msolopagazi vitabu ambavyo siku hizi vimekuwa ni adimu sana kuvipata madukani ,yaani sijaviona kabisa nilijaribu kuvitafuta nikapata vilivyoungua ungua na kalatasi zingine hamna.
 
"Yaliyopita si ndwele tugange yajayo". Naupenda huu usemi hasa katika hili la kutubandikia aliyowahi kuandika ama kusema Marehemu Chacha Wangwe. CHADEMA wanahitaji mshikamano wa hali ya juu iwapo wanayo nia ya kweli ya kutaka siku moja waongoze nchi hii. Kuna usemi mwingine pia ambao una mantiki katika jambo hili - "Usione vinaelea vimeundwa".

Vyama vingi imara vimeweza kufikia uimara wake kwa kuepuka migongano isiyo ya lazima. Hoja moja ya kipuuzi ambayo nimewahi kuisoma dhidi ya uongozi wa CHADEMA ni 'ukabila'!

Tanzania ya leo viongozi wa vyama vya siasa wanaotumia neno 'ukabila' wanajiondolea moja kwa moja sifa ya kuwa viongozi bora. Hivi Mwalimu Nyerere juhudi zote alizozifanya za kujitahidi kuondoa ukabila zilikuwa in vain?

Leo hii katika Tanzania makabila mbali mbali yameweza kuishi popote nchini bila matatizo yoyote lakini cha kushangaza suala la ukabila linaibuliwa kwenye vyama vyetu vya siasa eti ndio kigezo cha shutuma dhidi ya kiongozi wa chama! Kiongozi yeyote anayemshutumu kiongozi mwingine kwamba ana 'ukabila' hafai hata kidogo kuwa kiongozi kwa sababu analirudisha taifa letu nyuma!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom