Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
haya jamani tuisomeni vyema hii habari na tuangalie jinsi gani mzee misifa anavyotaka kukwepa lawama na kutaka kujisafisha kwa madudu alioyafanya.
Zitto aandika kitabu kuhusu Amina
Mwandishi Wetu Novemba 21, 2007
MBUNGE machachari wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe yuko mbioni kuandika kitabu kuhusu maisha ya mtangazaji, shabiki wa taarab na aliyekuwa mbunge machachari wa Vijana kwa tiketi ya UVCCM, marehemu Amina Chifupa.
MAREHEMU Amina Chifupa
Katika mahojiano na Raia Mwema wiki hii, Zitto alisema kwamba kitabu kuhusu maisha ya Amina aliyefariki Juni 26, mwaka huu, pamoja na kingine kuhusu ni kwa nini na jinsi gani alishinda ubunge wa Kigoma Kaskazini, viko katika hatua za mwisho.
Marehemu Chifupa alikuwa shabiki mkubwa wa muziki wa taarab, aliyefanya juhudi kubwa kuupandisha chati muziki huo akiwa mtangazaji wa Redio Clouds na hata kuongoza vyema maonyesho ya muziki huo kiasi cha kujulikana kama Mama Shughuli.
Akizungumzia kifo chake na ukaribu wake naye, Zitto alikiri kwamba alikuwa ni rafiki yake wa karibu na kwamba kitabu anachotunga kitahusu kazi zake akiwa bungeni.
Kwa hakika Amina alikuwa ni rafiki yangu wa karibu. Tulishirikiana kwa mambo mengi. Tulijifunza mambo mengi tukiwa pamoja.
Amina alikuwa ni mwanamke jasiri sana na mtu ambaye alijifunza mambo kwa haraka sana. Kweli hakustahili kufa.
Hivi sasa ninakusanya kazi alizozifanmya akiwa bungeni na kuzichapa kama kitabu. Ninataka watu pamoja na kizazi kijacho wafahamu kuwa tulikuwa na mbunge kijana mwanamke jasiri.
Rafiki yangu mmoja alipata kunitania mara baada ya kuwasilisha hoja yangu binafsi bungeni mwezi Agosti. Mama huyo alinitumia ujumbe wa simu akisema: Ujasiri wa Amina, kipaji cha uzungumzaji wa Mwalimu na kujiamini kwa Zitto.
Hii ilikuwa ni baada ya kuwasilisha hoja yangu kwa ustadi mkubwa. Hoja hiyo ndiyo iliyonifanya nisimamishwe ubunge, anasema Zitto. Akiwa bungeni, Amina aliwashangaza wengi kutokana na ujasiri wake wa kuibua mambo mazito na hata kujitolea kuongoza mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya waziwazi.
Akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu wa Mwaka 2006, Amina aliiomba Serikali kuwa makini na vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutomwonea haya yeyote. Alitaka vita hiyo iendeshwe kama zoezi la Bomoa bomoa ambalo halikuwa na huruma kwa yeyote.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ni mimi Amina ninauza nikamatwe, hata kama ni Mbunge, kama ni mume wangu anauza hata kama ni mume wa Mbunge akamatwe, kama kuna Mbunge humu ndani anafanya biashara ya dawa za kulevya jamani akamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria na sheria ziwe kali.
Kama kuna kiongozi mwingine yeyote wa nchi, sheria ni msumeno kama nilivyosema imkute kila mtu ikate kila mahali. Lakini siyo sheria ni msumeno kwenye bomoabomoa tu na mazoezi mengine, inapokuja kwenye issue ya dawa za kulevya sielewi kinachofanyika kwa kweli sielewi, alisema.
Marehemu Amina ambaye alifariki kutokana na kuzidiwa na kisukari na malaria, alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ushindi ya Dar es Salaam na baadaye akajiunga na Shule ya Sekondari ya Kisutu.
Alipomaliza kidato cha nne, Amina Chifupa alijiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Makongo.
Tangu akiwa shuleni, marehemu Amina alishaanza kazi ya utangazaji wa redio. Mwaka 2005, Amina alitwaa ubunge baada ya kufanya vyema katika uchaguzi mkuu kupitia tiketi ya viti maalum (Vijana-CCM). Hadi anafariki alikuwa na umri wa miaka 27.