Kwanini vifo vya Amina Chifupa na mumewe Medi Mpakanjia vilikuwa vina maswali mengi kuliko majibu?

Andre-Pierre

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
328
1,209
Nimepitia jukwaani nikaona picha ya Amina Chifupa nikakumbuka namna alivyofariki na kutuachia maswali mengi.

Hayati Amina Chifupa alisema ana list ya wauza “poda” na atawataja hadharani bungeni. Mpaka anaenda kaburini hakuweza kuitaja kwani aliumwa mfululizo.

Miaka kadhaa baadae, mume wa Amina, mfanyabiashara Medi Mpakanjia ambaye mtaani inasemekana nae alikuwa anauza “poda” nae akafariki ghafla tu! Maswali yakawa mengi na kukosa majibu.

Ikimbukwe mwanzoni mwa miaka ya 2000 hawa walikuwa ni miongoni mwa mastaa waliokuwa wanatikisa Bongo.

Kwanini vifo vyao vimeacha maswali mengi?
 
Back
Top Bottom